Na we binti Maringo ujifunze kumezea, huna dogo!!!!mchanga wa macho!....wee si ulisema umesoma shaban Robert?..how come tena ukasoma Tambaza?....juzi hapa kwenye matangazo uliandika unamtafuta shori mmoja ulisoma naye shaban robert ulikuwa unamtamani lakini unakufa kisabuni||
Tulikuwa na mchizi mmoja kitaa, ni full bhange full vurugu!!! Tukienda disko la uswazi na isipopigwa "Jamaican in NewYork" ya .....(nishamsahau), jamaa lazima alete fujo na disco haliendelei hadi Jamaican in NewYork ipigwe!!! Uzuri ni kwamba kitaa kwenyewe kulikuwa na manunda kibao wa Tambaza ambao alijivuna wangemlinda!!!Nipo hapa nimeboreka, najaribu ku-reminisce matukio mbalimbali ya maisha yangu. Wangapi hapa walishuhudia hii shughuli kwa namna moja ama nyingine? Unakumbuka nini kuhusu tukio hili?
It will always be in my memory,
Vurugu ya mwisho tuliingia Azania na chupa za mafuta yas petrol kama mabomu, nikiwa form two.
Tukarusha mabomu mawili laboratory ya Azania, wakawahi kuizima.Mara Azania wakatoka na makwanja , tumo ndani ya senyenge zao! Kilichotokea baada ya hapo inabaki historia.
Nilikimbia jangwani mabondeni huko nikakutana na tope linanuka vibaya sana, kuna wanafunzi wa azania walikuwa huko walikula kibano.It was war-like zone
Lakini nakiri afadhali walituhamishia mikoani, maana nisingemaliza salama, umri wa kubalehe ule na kufuata mob saikoloji ungetumaliza.
Ulikuwa ukituleta darasani moto wa kuotea mbali!! makonda walikuwa wanaheshimu Tambaza bwana
Label ya shule ilikuwa kali mpaka leo sijaona mfano wake, yangu ilikuwa kijani-group two!
SAMBUKILE-TAMBAZA!!!!!!!!!!!!!!!
haaaaaa, mkuu bruurei ulikua azaboy kumbe??Nasikia mnaa Hawanga kajifia zake, kweli?
Sidhani kama ni sahihi kusema azania walikuwa legelege, hawakuwa watu wa fujo lakini vurugu zilivyozidi walistep up, matukio aliyosema 'Waberoya' nayakumbuka, ilikuwa lazima mtembee kwa makundi, hasahasa mida ya kwenda nyumbani. Siku moja naelekea nyumbani mida ya mchana, nimeshaachana na washikaji niko mwenyewe, nikakutana na kundi la wanafunzi wa tambaza wakaanza kuniapproach, sikukimbia wala nini, nikasimama. Bahati wakaona wanajeshi (mnakumbuka kipindi kile wananunua chakula na vinywaji kwenye fence ya kambi pale upanga), wakageuza na kuondoka zao.
Kipindi hicho hicho migomo ya walimu ndiyo imepamba moto, kama sikosei. Companero nakumbuka kwa mbali Azajangwa, ilikuwa ni wanafunzi wa azania wanahook up na wanafunzi wa jangwani, right?
jmushi1, buza namkumbuka kwa mbali. azania walikuwa na jamaa mmoja hivi alikuwa anabeba chuma, amejaza hivi, baadaye alikuja kuwa bouncer casino ya pale newafrica hotel, sijui yupo wapi siku hizi, nadhani na yeye alikuwa anakaa sinza. Ila nakubali, tambaza walikuwa wababe. Hawakuwaga hata na timu ya kutisha ya mpira, labda basketball enzi za kina kelvin twissa, kiasi.
Nyie wote mlikuwa rough na wahuni katika enzi zile ni st.Joseph[Forodhani] pekee ndiyo ilikuwa shule ya wastaarabu. katika maisha yangu ya shule hiyo sikuwahi hata siku moja kuona mwanafunzi akivuta sigara lakini kwa azania na tambaza ilikuwa siyo ajabu. ninakumbuka hata wakati wa sherehe za kitaifa kule uwanja wataifa zikitolewa soda kwa kila shule lakini jamaa hawa walikuwa wanachukua hata za kwetu .
Ahsante sana kwa kukumbushia enzi zile
It will always be in my memory,
Vurugu ya mwisho tuliingia Azania na chupa za mafuta yas petrol kama mabomu, nikiwa form two.
Tukarusha mabomu mawili laboratory ya Azania, wakawahi kuizima.Mara Azania wakatoka na makwanja , tumo ndani ya senyenge zao! Kilichotokea baada ya hapo inabaki historia.
Nilikimbia jangwani mabondeni huko nikakutana na tope linanuka vibaya sana, kuna wanafunzi wa azania walikuwa huko walikula kibano.It was war-like zone
Lakini nakiri afadhali walituhamishia mikoani, maana nisingemaliza salama, umri wa kubalehe ule na kufuata mob saikoloji ungetumaliza.
Ulikuwa ukituleta darasani moto wa kuotea mbali!! makonda walikuwa wanaheshimu Tambaza bwana
Label ya shule ilikuwa kali mpaka leo sijaona mfano wake, yangu ilikuwa kijani-group two!
SAMBUKILE-TAMBAZA!!!!!!!!!!!!!!!
Nawakumbuka wavuta bangi wa shule hizi mbili...........Nipo hapa nimeboreka, najaribu ku-reminisce matukio mbalimbali ya maisha yangu. Wangapi hapa walishuhudia hii shughuli kwa namna moja ama nyingine? Unakumbuka nini kuhusu tukio hili?
Unakumbuka yale mambo mnatoka zenu mkoa kwa kukodi mabasi?
Si tulikuwa tukichukua gogo la TAZARA(kama unakuja dar nakumbuka wanafunzi tulikuwa tunalipa nusu sijui siku hizi), enzi hizo ilikuwa ubabe kwenda mbele,kuna siku tulikutana na watoto wa mwakaleli sec. humo kwenye gogo ilikuwa noma.
watoto wa Sangu,Meta na mbeya day wanatukumbuka vizuri(iyunga).
Ilikuwa mkisikia mmetangazwa kwenye vyombo vya habari kuwa mmefanya vurugu basi kwenu ilikuwa raha kweli.
Dah! kweli noma.
Vurugu za Azania Vs Tambaza zilianza zamani sana. Tulikuwa na Mwalimu mmoja pale Azania aliitwa Mzee Meja na siku moja alitusimulia jinsi alivyokuwa refa kwenye mechi kati ya Tambaza na Azania na jinsi Tarzani Kesi (aliyekuwa Mchezaji wa Yanga baadaye) alivyokuwa mmoja wa watukutu wa Tambaza.
Hata hivyo enzi niliposoma mimi Azania Tambza hawakuwahi kutushinda kwenye Umiseta na hata ngumi, nakumbuka miaka ya mwanzo mwa 1990 au mwisho wa 1980s walikuja kucheza na Azania pale Aznaia tukawaunga na wakaanzisha vurugu, tuliwachapa sana na wakakimbia, walichofanya vijana wa Tambaza ni kutuvizia barabarani tukienda kupanda daladala huo ugomvi ulichukua muda kuja kuisha. Mwisho wa vurugu zilikuwa katikati ya miaka ya 1990s ambapo Aznaia waliwapiga sana Tambaza hadi kupelekea kufutwa kwa O'Level pale Tambaza nasikia kwenye ugomvi huo kuna wanafunzi walikufa ingawa haikutangazwa.