Tambi za mayai

Tambi za mayai

Ritz

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2011
Posts
51,303
Reaction score
40,190
Wanaukumbi.

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana nanimlo uliokamilika.

Licha ya utamu wa chakula hiki,kitu kingine ninachopenda ni muonekano wake hasa ambavyo mayai hutengeneza kama matone madogo madogo na kushikana na tambi.
Mahitaji

  • Tambi ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa
  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraia ladha yake zaidi.
 
Hili pishi nalizimia sana sana hasa linapochanganywa na prawns kidogo na vineger kwa mbali na kaglass ka red sweet wine wee acha tu
 
Mie hupika chicken pasta .. .natumia chickrn breast

Shukraan Ritz
 
Last edited by a moderator:
Hili pishi nalizimia sana sana hasa linapochanganywa na prawns kidogo na vineger kwa mbali na kaglass ka red sweet wine wee acha tu

Na soya sauce ila praws unapenda sana si mara ya kwanza kukuskia kutaja. . Hata na mie napenda sana seafood nahisi nna nyota au nyau lol
 
Ritz kumbe nawe umo kwenye mambo yetu ya maakulat. Hongera sn. Na Asante kwa ku share
 
Last edited by a moderator:
Kudos Ritz hii menu naipenda hatari..
 
Last edited by a moderator:
Nikirudi hoi akili ya kwanza hufikiria tambi na mayai haina stress kupika ni fasta na tamu....
 
Na soya sauce ila praws unapenda sana si mara ya kwanza kukuskia kutaja. . Hata na mie napenda sana seafood nahisi nna nyota au nyau lol

Farkhina seafoods zinanitoaga roho kwakweli
 
Dah, shukran, yaweza kuwa ftari yangu. Imevutia
 
Wanaukumbi.

Tambi za mayai ni moja kati ya vyakula ambavyo napenda kuandaa pale ninapokua ninaharaka au sina muda mrefu wakukaa jikoni.pishi hili huchukuca muda mfupi sana nanimlo uliokamilika.

Licha ya utamu wa chakula hiki,kitu kingine ninachopenda ni muonekano wake hasa ambavyo mayai hutengeneza kama matone madogo madogo na kushikana na tambi.
Mahitaji

  • Tambi ½ paketi
  • Vitunguu maji 2 vikubwa
  • Karoti 1
  • Hoho 1
  • Vitunguu swaumu(kata vipande vidogo) kijiko 1 cha chakula
  • Carry powder kijiko 1 cha chai
  • Njegere zilizochemshwa ½ kikombe
  • Mafuta kwa kiasi upendacho
  • Mayai 2
  • Chumvi kwa ladha upendayo
Njia
1.Chemsha maji yamoto yanayotokota,ongeza chumvi na mafuta kidogo,weka tambi kwenye maji hayo chemsha adi ziive.Chuja maji yote ili kupata tambi kavu
2.Katika bakuli piga mayai kisha weka pembeni
3.Katika kikaango,weka mafuta,vitunguu maji ,vitunguu swaumu,hoho, karoti na carry powder,kaanga kwa pamoja katika moto mdogo kwa muda mfupi kwani mboga hazitakiwi kuiva.
4.Ongeza tambi na njegere katika kikaango,geuza kila mara ili kuchanganya .
5.Ongeza mayai kwenye tambi kisha geuza kwa haraka bila kupumzika adi mayai yaive na tambi ziwe kavu.Tayari kwa kula

  • Katika hatua hii ongeza moto uwe wa wastani,moto ukiwa mdogo mayai yatafanya tambi zishikane na kufanya mabonge.
Unaweza kula tambi hizi na mboga yoyote upendayo au laa ukala zikiwa kavu na kufuraia ladha yake zaidi.

bonge la msosi aise.
 
Cjui kupika chochote ila leo ntasuprise watu home kwa ili pishi.
 
Back
Top Bottom