Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Zab 124:8 SUV
[8] Msaada wetu u katika jina la BWANA, Aliyezifanya mbingu na nchi.
Kwa akili zetu za kawaida tunaweza tukawa tunafikiri msaada wetu wa uhakika tunaweza kupata kwa wazazi wetu, ndugu zetu, marafiki zetu na watu wengine wengi tunawaona sisi ni watu wetu wa karibu na wana uwezo mkubwa kiuchumi kutusaidia.
Tunaweza tukajivuna tuna watu wa kutosha kwa kila eneo tutakalohitaji msaada wao, tukabaki na majivuno hayo, tukaona dunia hii haiwezi kututisha kwa lolote kutokana na watu wanaotuzunguka wa kuweza kutusaidia lolote tunalolihitaji kwao.
Napenda ufahamu hili, msaada wetu wa kweli haupatikani kwa wanadamu, bali unapatikana kwa Mungu, ikiwa wewe ni muumini na umewekeza imani yako kwa watu, ujiandae kulia machozi mengi.
Ikiwa unategemea vitu vya dunia hii kama kinga yako, au juhudi zako binafsi, utakuwa haupo sehemu salama kabisa, umeegemea kwenye sehemu ambayo sio salama kwako. Unapaswa kuelewa msaada wako wa kweli unatoka kwa Mungu muumba wa mbingu na nchi.
Kuhitaji msaada kama wanadamu ni jambo ambalo haliwezi kukwepeka hata kidogo, tunamhitaji Mungu katika maeneo tofauti tofauti, zipo nyakati za dhiki na majaribu magumu. Kama mwandishi wa zaburi hii ametambua msaada pekee wa uhakika unapitikana kwa BWANA, na wewe unapaswa kuamini hivyo.
Kushinda changamoto kwa kutumia mali zako, akili zako au elimu yako, uwe na uhakika kuna wakati hutoweza kushinda, sio kila changamoto inaweza kutatuliwa na uwezo wako wa kifedha, na elimu yako au ujuzi wako, mengine yanamhitaji Mungu mwenyewe aweze kukusaidia.
Weka imani yako na tegemeo lako kuu kwa Bwana Yesu, moyoni mwako iwe wazi kuwa chanzo kikuu na cha kwanza kuweza kutatua matatizo yako au changamoto zako ni BWANA pekee, na sio mwanadamu.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia yako
Mungu akubariki sana