Tambua haya wakati unaachana na Umasikini

Infinite_Kiumeni

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2023
Posts
382
Reaction score
687
Badilisha tabia ya umasikini
Tabia iliyokusaidia kuishi wakati wa umasikini ndo inayoendelea kukufanya maskini.
Maisha yakibadilika ni muhimu na tabia yako ibadilike.

Hauwezi kuua umasikini
Unachoweza wewe ni kujitoa kwenye umasikini. Hata kama ukitaka kumsaidia mtu. Utambue kwamba huyo mtu naye ana uchaguzi wake, ana vitu apendavyo na huwezi kumfanyia maamuzi.

Usijihukumu ukishindwa kuua umasikini kwa wengine. Hivyo, usimlazimishe asiyetaka we jitoe mwenyewe utakutana na unaofanana nao.
.
Umaskini una gharama zaidi uhuru wa kifedha
Sababu unakua hujafungamana na kitu, upo huru. Umaskini unamfanya mtu ajali zaidi vitu vya kuja na kupita tu. Wanajifunga kwenye vitu kama gari, saa, feni, simu au chochote ambacho kipo tu.

Mtu atatumia pesa hovyo asiitwe/ asionekane maskini.

Ni kama wanauhudumia umaskini zaidi.
.
Usifikirie pesa kwa woga kwamba hutopata
Ukifikiria hivyo utapata shida sana kuzipata na utaona hela ngumu. Hata vitabu vitakatifu vimesema unapata unachofikiria zaidi.

Mawazo yako mengi yakiwa ya woga juu ya hela na kwamba hutopata, basi utazawadiwa hicho hicho, kuipata hela kwa ugumu.
.
Chanzo cha umaskini ni ujinga
Ujinga ni kutojua kitu, wala sio tusi. Wengi hatufundishwi kuhusu hela tukiwa tunakua. Tunaona tu wengine. Kisha tunawaiga wanavyotumia hela. Ni muhimu uongeze ujuzi wako kuhusu hela. Mana ulipo ni kwa sababu hujui usichokijua.

Wengi wanaamini hawana kingine cha kuchagua
Wanaamini umaskini ndio nafasi pekee waliyonayo. Na Mungu ndo amewaumba wawe hivyo, kwaiyo inabidi aendelee kuwa maskini.

Wengi wanawaponda wanaotaka kuwasaidia
Wengine wanawachukia wanaotaka kuwasaidia. Wengine wanawaona kama ni maadui. Wengine wanakatisha tamaa wanaojaribu kujitoa kwenye umaskini. Hivyo, uwe makini usije ukapoteza nafasi ya kusaidiwa sababu ya ujinga wa kimaskini.

Unaweza kuona ni ngumu kubadili mawazo
Kutoka kufikiria umaskini kwenda kwenye kufikiria uhuru wa kifedha. Au kubadili mawazo ya kufikiria “nataka kutoka kwenye umaskini”. Hayo mawazo hayatokutoa kwenye umaskini.

Sababu yatakufanya utengeneze tabia za kujilinda na umaskini badala ya tabia za uhuru wa kifedha. Wengi huona ni pagumu hapa na wanakata tamaa.

Mazingira nayo yanachangia umaskini
Kama umelelewa kimaskini. Hata ukikua utazungukwa na maskini. Sababu ni rahisi kuelewana.
Pia ukizungukwa na maskini ni ngumu kuuepuka.

Unaweza ukaachana na umaskini
Huo uwezo unao. Basi tu umeaminishwa vibaya. Au maisha uliyopitia na misukosuko yake imekufanya uamini vibaya. Mpaka unajiona ni muhanga wa umaskini.

Lakini kiukweli unaweza kuchagua kuachana nao.

Na kujitengenezea tabia mpya za ushindi badala ya kujiona mnyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…