Saratani hii hutokea kwenye tezi ya thyroid iliyopo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo nahuwapata watu wa umri mbalimbali, kuanzia watoto mpaka watu wazima. Watu waliowahi kupigwa mionzi sehemu ya mbele ya shingo na wenye wazazi wenye tatizo ili wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya saratani.
Dalili Dalili hutofautiana kulingana na aina ya saratani, ingawa kiujumla zaweza kujumuisha: kikohozi Shida wakati wa kumeza chakula, vinywaji hata mate Kuvimba kwa tezi ya thyroid Mabadiliko katika sauti, sauti kufifia au kuwa ya mikwaruzo Uvimbe kwenye shingo Tezi ya thyroid kuwa na nundu au vinundu