SoC01 Tambua Nyakati: Usibaki unapotakiwa kuondoka

SoC01 Tambua Nyakati: Usibaki unapotakiwa kuondoka

Stories of Change - 2021 Competition

Musa Meizon

Member
Joined
Aug 3, 2021
Posts
13
Reaction score
53
Ukweli ni kwamba, ni jambo kubwa sana kutambua NYAKATI, ni muhimu kujua muda gani ufanye Nini? Uwe wapi? na hatima au matokeo ni Nini?

Habari yako Mpenzi msomaji. Leo napenda kukuepusha na hatari ya kutotambua nyakati katika MAHUSIANO YA KIMAPENZI. Watu wengi wanapoteza muda kubaki na wenza ambao ilibidi wawaache kitambo au wajiepushe na Mahusiano hayo kabisa.

Mwisho wa Mahusiano yasiyo na malengo ni hasara tupu na maumivu yake hayaelezeki na huleta majuto sana. Hivyo ni muhimu kutambua uko mahali salama au laa na ujue ni maamuzi yepi yanafaa kwa muda muafaka.

Nitaanza na wanawake Kisha wanaume. Ili kujua mwanaume uliyenae anakuchezea/anakupotezea muda mtazame katika haya matatu:

1. MUDA: Kama Kuna kitu wanaume wote hufanana basi ni katika matumizi ya muda. Wanaume kwa asili hupenda kutumia muda wao kufanya jambo wanalolipenda. Hawawezi kuigiza katika hili, kama hakupendi hatokupa muda wake, ukiona kila ukiwa nae ni muda mtafanya MAPENZI tu baada ya tendo mnaachana jua anakuchezea, ila kama anakupenda hata kama hamfanyi mapenzi atataka kukaa nawewe. Ukiona kabla hamjaonana anauliza UKO KWENYE SIKU ZAKO? Jua umechemka! Mwanaume anajali sana muda na huutumia kukaa na anao wapenda iwe rafiki au Mpenzi.

2. TABIA: Pia katika hili wanaume wote hufanana. Mwanaume akipenda humchukulia mwanamke wake kama mke mtarajiwa hivyo suala la tibia ataanza kulitilia maanani zaidi. Ukiona hakukemei, hajaribu kukubadili baadhi ya tabia wala kukuambia anapenda mwenendo gani basi unatumika.

Ndio maana Kuna kabila flani wanawake wanatumia kigezo cha Mwanaume kumpiga Mpenzi wake kama ishara ya mapenzi ya kweli.

3. USIRI: La mwisho, wanaume wanasemekana kufanana, na hili pia linaunga mkono imani hiyo, mwanaume akiwa na mwanamke anaye mpenda huwa HAMFICHI hata siku moja. Ukiona Mwanaume wako anaficha Mahusiano yenu jua unatumika. Wanaume wana hurka ya kujivunia wakipata wanachokipenda. Kama hata rafiki zake hawakujui wala Ndugu na jamii jua atakuacha siku yoyote.

Inatossha upande wa wana wake, tuje kwa Wanaume sasa. Yatazame yafuatayo kujua mwanamke uliyenae anakupenda au anakutumia:

1. HESHIMA: Namba moja kabisa, mwanamke akipenda huheshimu sana. Wanawake huheshimu kwani humchukulia kama mumewe mtarajiwa. Ukiona heshima haipo jua mapenzi ya kweli hayapo. Kiashiria kizuri cha heshima ni kutofanya jambo usilolipenda mfano; mavazi usiyoyapenda, marafiki usiowapenda au hata kauli usizopenda.

2. USIKUVU: Wanawake pia hufanana katika haya, kisayansi Wanawake wanakumbukumbu zaidi ya Wanaume hivyo huwa na usikivu mkubwa kwa wale wawapendao ili kuweka kumbukumbu juu ya Yale watayoambiwa. Ukiona mwanamke wako unamuambia jambo moja mara kadhaa analipuuza na kusahau jua hakupi usikivu na ni ishara hauko MOYONI mwake.

3. FURAHA : Hili la mwisho na ni jepesi kuligundua, angalia sana furaha ya mwanamke wako akiwa na wewe. Imegundulika kwamba mwanamke akipenda huwa mwenye Furaha sana akiwa karibu na mwanaume ampendae. Hivyo kama mwanamke wako hajawahi hata kutabasamu ukiwanae basi jua umemkwaza au hana hisia zozote Kwako kwani mara nyingi mwanamke huwa na Furaha na ni mwepesi kumfurahisha endapo kakupenda.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom