Tambua vizazi (Generation) vilivyopata kutokea duniani.

Tambua vizazi (Generation) vilivyopata kutokea duniani.

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Generation au Kizazi inawezekana haujui lakini kisayansi, kisiasa, kijamii, kidini, kibiashara na kiutafiti kina maana kubwa sana kwani ndio huamua kwenye kizazi husika nini wanataka kwa kuangalia mienendo yao ya maisha. Bila kujua mienendo yao basi kila kitu kingeshindwa kufanyika kwa ukamilifu. Mfano bila kuangalia watu wa kizazi hiki wana matumizi makubwa ya Internet na Mitandao kama JF, Facebook, Whatsapp, Snapchat, Instagram etc basi tarajia biashara yako kufeli fikia malengo yake.
Leo Mark zuckerbergh anaitwa na US Congress kujielezea ni kutokana na mtandao wake (Fb) kutumika kuamua chaguzi mbalimbali duniani. Unaweza jiuliza kivipi?, hebu chukulia mfano wa hawa waganga feki kwenye simu zetu au sms za kubet na Biko au 3 mzuka haya yote ni matokeo ya mienendo ya Kizazi chetu. Kivipi? ni kwamba watu wana nunua online data zako au taarifa unazoweka mtandaoni wanakuangalia mtindo wako wa kusearch vitu online na posts zako then wanaitengeneza biashara au tangazo lao kufuata mtindo wako-unadhani utaepuka hili? (Hii biasshara inafanyika sana lakini sio kwa watu wote na kampuni zote).
Vifuatazo ni baadhi ya vizazi vilivyopata tokea toka binadamu tulipojitambua.
  1. Arthurian Generation (1433–1460)
  2. Humanist Generation (1461–1482)
  3. Reformation Generation (1483–1511)
  4. Reprisal Generation (1512–1540)
  5. Elizabethan Generation (1541–1565)
  6. Parliamentary Generation (1566–1587)
  7. Puritan Generation (1588–1617)
  8. Cavalier Generation (1618–1647)
  9. Glorious Generation (1648–1673)
  10. Enlightenment Generation (1674–1700)
  11. Awakening Generation (1701–1723)
  12. Liberty Generation (1724–1741)
  13. Republican Generation (1742–1766)
  14. Compromise Generation (1767–1791)
  15. Transcendental Generation (1792–1821)
  16. Gilded Generation (1822–1842)
  17. Progressive Generation (1843–1859)
  18. Missionary Generation (1860–1882)
  19. Lost Generation (1883–1900)
  20. Government Issues Generation (1901–1924)
  21. Silent Generation (1925–1942)
  22. Baby Boom Generation (1943–1960)
  23. Generation X (1961–1981)
  24. Millennial Generation (1982 – 2004)
  25. Generation Z (2005 – Present)
Kizazi kijacho kimechaguliwa jina la "Generation Alpha" au "Generation Glass" hii wakiangalia kuwa ni kizazi kitakachokuwa kimesoma zaidi ya vizazi vyote vilivyopata tokea, pia ni kizazi kitakachotumia teknolojia zaidi ya vyote na ndio kizazi tajiri zaidi.
 
Natamani nifike huko but ndo ivo umri kamili wa kuishi hauniruhusu!
Nadhani hiko ndo kizazi kitakachokua kinadonlodi Nyumba, Kinasafiri kwa e mail etc
Inakuaje unakata tamaa mapema?
Umeongea Na MUNGU au roho Mt?
 
Natamani nifike huko but ndo ivo umri kamili wa kuishi hauniruhusu!
Nadhani hiko ndo kizazi kitakachokua kinadonlodi Nyumba, Kinasafiri kwa e mail etc
[emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji2] [emoji3]
 
huo ni mzunguko tu,mzunguko huo hata bado haujaanza kutoa maana ya uhai!
swali la kwanini tunaishi..?
hili ndio swali linalotaka mantiki ya uwepo wa uhai wetu(nini tunatakiwa tufanye)!,huenda kukawa kuna kitu kikubwa ambacho hatukijui kuhusiana na uhai wetu na huenda tukikijua tutaishi kwa weledi unaotakiwa na kuufurahia uhai!.

pamoja na kuwepo kwa hizo generation,mwanadamu amekuwa kiumbe anaeharibu mazingira kwa kiasi kikubwa(huku kiwango cha uharibifu kikizidi kadri anavyoendelea) je,unafikiri binadamu anastahiri kuwepo duniani..?

isijekuwa tunajidanganya kuwa tunaakili kushinda babu zetu wkt tumekuwa waharibifu wakubwa wa mazingira wkt tunajiangamiza..
hata mazao tu yamekuwa yakubustiwa! mpk upulizie dawa na mbolea za kikemikali!
samahani lkn kama nitakuwa nimetoka nje ya mada!.
 
Kuhusu kwanini tunaishi nazani unataka jibu la Kidini sababu kisayansi jibu linaeleweka!..
Binadamu anastahili kuwepo na ana evolve kadri muda unavyokwenda mbele ndio maana sasa ana ndoto ya kutawala ulimwengu mzima sio tena dunia hii!..
Ukianzisha biashara ukateka soko la mtaa wewe sio mharibifu ni umeweza teka mazingira yako so next step ni kuteka na mitaa jirani, wilaya, mikoa, nchi hata ulimwengu!.
Kipimo cha akili ni kazi kukitumia sababu mababu zetu hawakuwa na moto wakauvumbua sisi hatuna maji tumetengeneza mvua utalinganisha vipi hapa akili?..
Kila kizazi kiliishi kupambana na mazingira yake, mfano kizazi cha 18 ni tofauti na kizazi cha 23 sababu mazingira yao ni tofauti kabisa!.. Wakati 18 wanaongelea mambo ya dini 23 wanaongelea mambo ya kuwa huru na ndipo ushiriki wa wazazi kwa watoto wao unapokomeshwa kuwa ombi na kuwa lazima!.
 
Un

Unge eleza na sifa ya kila kizaz ingekua jambo la msingi Na Uzi ungependeza
 
vigezo gani vinatumika kutenganisha hizo aina ulizotaja hapo??
Life style trends, Political turbulences, Religious beliefs, Economic status, Environment capability, Age status, Technological innovations!..vigezo kama hivyo!.
Ila kuhusu kizazi ukifanya hesabu simple unakuta ni MIAKA 20-30.
Cc: Heri lee
 
Un

Unge eleza na sifa ya kila kizaz ingekua jambo la msingi Na Uzi ungependeza
Mkuu vizazi 25 kila kimoja sifa yake!. Unazani uzi ungekuwaje?..Anyway nitajie unachohitaji kujua sifa zake nikupe but kuviwekea vyote hiyo sio ripoti ni taarifa tu!..
 
Currently, five generations make up our society. Each of those five generations has an active role in the marketplace. Depending on the specific workplace, the workforce includes four to five generations. Here are the birth years for each generation:

Gen Z, iGen, or Centennials: Born 1996 and later

Millennials or Gen Y: Born 1977 to 1995

Generation X: Born 1965 to 1976

Baby Boomers: Born 1946 to 1964

Traditionalists or Silent Generation: Born 1945 and before
 
Natamani nifike huko but ndo ivo umri kamili wa kuishi hauniruhusu!
Nadhani hiko ndo kizazi kitakachokua kinadonlodi Nyumba, Kinasafiri kwa e mail etc
Dogo unakata tamaa sana na maisha kama mungu alitaka uishi miaka kumi kwa hofu yako ushapunguza miaka 8 hapo.we are all walking dead but others dont give a fuuckk!!
 
Back
Top Bottom