Tambua vyakula vinavyosababisha ugonjwa wa saratani

Tambua vyakula vinavyosababisha ugonjwa wa saratani

Katika utafiti nilioufanya nimegundua kuwa fungus ndio kiini kikuu cha kansa.vyakula na vitu vingine vinachangia kwa % ndogo sana licha wengi hawatakubali hasa watu wa magharibi kwa kuwa ndo mchezo wao.
 
tambua vyakula vinavyosababisha ugonjwa wa saratani

utafiti mbalimbali uliokwishafanywa unaonyesha kuwa magonjwa mengi ya saratani (cancer) yanatokana na vyakula tunavyokula kila siku katika maisha yetu. Katika siku za hivi karibuni, ongezeko la magonjwa haya limekuwa kubwa kwa sababau vyakula vinavyosababisha magonjwa hayo, ndivyo vinavyoliwa sana kuliko vile vinavyozuia.

wiki iliyopita tuliwaorodheshea baadhi ya vyakula vinavyoaminika kusaidia kuzuia magonjwa ya kansa ambapo wiki hii tunawaletea orodha ya vyakula vinavyoaminika kuongoza kwa kuwa chanzo cha magonjwa hayo hatari:


vyakula vya kukaanga

vyakula vingi vinavyotayarishwa kwa kukaangwa kwenye mafuta yenye moto mkali huwa na madhara kiafya na miongoni ma madhara hayo ni pamoja na kusababisha kansa ya kwenye mfuko wa uzazi. Vyakula hivyo ni pamoja na chips na vyakula vingine vinavyopikwa kwa kukaangwa kwenye mafuta.

vyakula vyenye chumvi nyingi

vyakula vyenye chumvi nyingi vimebainika navyo kusababisha kansa. Vile vile inaelezwa kuwa chumvi huwa kama chakula kwa bakteria wa kansa tumboni. Kansa ya tumbo inadaiwa kuua watu wengi nchini japan kutokana na jamii hiyo kupenda sana vyakula vyenye chumvi nyingi. Miongoni mwa vyakula vyenye chumvi nyingi ni vile vya kusindika, kama vile nyama za makopo, maharage, n.k

sukari

matumizi mabaya ya sukari yanaelezwa kusababisha kansa. Kama tujuavyo, kuna aina mbalimbali za sukari lakini sukari hatari zaidi ni zile zinazowekwa kwenye vinywaji mbalimbali, zikiwemo soda, juisi za ladha ya matunda ambazo huwa na kiwango kingi cha ‘fructose’ ambayo inaelezwa kusababisha saratani ya kongosho.

Vile vile sukari kwa ujumla wake hairuhusiwi kutumiwa na mtu ambaye tayari amegundulika kuwa na kansa kwa sababu chakula cha chembechembe za saratani mara nyingi huwa ni sukari. Kwa matumizi mengine ya kawaida, sukari inatakiwa kutumiwa kwa kiwango kidogo sana katika vinywaji au vyakula tunavyotumia, tofauti na baadhai ya watu wanavyoweka sukari nyingi ili kupata utamu zaidi.

nyama iliyoiva sana
upikaji wa nyama kwa muda mrefu na kwenye moto mkali (high temperatures) husababisha aina fulani ya kemikali inayojulikana kitaalamu kama ‘heterocyclic aromatic amines’. Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na chuo kikuu cha utah (university of utah), umeonesha kwamba watu wanaopenda kula nyama zilizoiva sana, wako hatarini zaidi kupatwa na saratani ya njia ya haja kubwa (rectal cancer). Hivyo inashauriwa unapopika nyama, usipike kwenye moto mkali na kuiva kupita kiasi.

pombe
unywaji wa pombe kupita kiasi nao unaelezwa kusababisha aina nyingi ya saratani, kwa wake kwa waume. Aina ya saratani zinazodaiwa kusababishwa na pombe ni pamoja na satarani ya mdomo, ini, utumbo na koromeo, ambazo ndizo zinazoua watu wengi hivi sasa nchini marekani.


nyama na mafuta

utafiti uliofanywa na chuo kikuu cha havard nchini marekani, umegundua kwamba watu wanaopenda kula nyama kila siku wako hatarini kupatwa na saratani ya utumbo kuliko wale wanaokula mara moja moja. Pia baadhi ya mafuta ya wanyama na yale yanayowekwa kwenye ‘baga’ au ‘cheese’ huweza kusababisha kansa.
Vile vile ulaji wa vyakula vilivyotengenezwa kwa kuchanganya na nyama zilizosindikwa au kuhifadhiwa kwa matumizi ya muda mrefu husababisha saratani pia. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘soseji’ ambazo hupendwa na watu wengi. Pia mikate ya nyama ‘hot dogs’ nayo ni chanzo cha magonjwa ya saratani.

vyakula vya unga mweupe

vyakula vyote vinavyopikwa kutokana na unga uliokobolewa na kuondolewa virutubisho vyake vyote na kuwa mweupe, vinaelezwa kuchangia magonjwa ya saratani kwa kiasi kikubwa. Vyakula hivyo ni pamoja na ‘donati’ (doughnuts), maandazi, mkate mweupe, n.k
mwisho, licha ya kuepuka ulaji wa vyakula vilivyotajwa hapo juu, unatakiwa kuzingatia ulaji wa vyakula asilia vitokanavyo na mimea, mboga za majani na matunda kwa wingi kila siku. Utaona kwamba adui mkubwa wa afya zetu ni vyakula vyote vya kusindika na vile vya kutengenezwa viwandani au vile ambavyo wakati wa utayarisjaji wake huondolewa virutubisho vyake vya asili.
source

sasa tule nn?
 
Mi niliacha kila kitu nikawa nakuka mchemsho wa samaki na mchicha. Nikaambiwa mchicha unaweza kuwa unalimwa mfereji yenye sumu. Pia samaki wanavuliwa na sumu. Tangu siku hiyo sichagui mlo nakula kila kitu ya nini kujinyima??. Kufa kupo tu hata kwa ajali

Umenichekesha sana, ila ni kweli unayosema, hizi mboga za majani tunazokula ukipita huko mabondeni zinakolimwa yale maji wanayotumia kunyweshea ni hatari sana, tunaambiwa majani ya chai ni sumu, maji tunayokunywa ya chemchem tu ndio salama otherwise haya mengine yana kemikali, chips zina madhara, pombe, mikate[white breads-hii mikate tunayokula] maandazi, vitumbua, nyama nk, nk mweee hatuponi aisee. Bado madereva wa mabasi wanavyotumaliza sasa . MGANGA MUNGU
 
Naongezea kwenye post ya MziziMkavu .Ukiachilia mbali vyakula na vya kunywa,vyanzo vingine vya saratani ni;
Matumizi ya mara kwa mara ya dawa za hospitali kama vile antibiotics,dawa za kutuliza maumivu kama diclofenac,VIDONGE VYA UZAZI WA MPANGO,vidonge vya ARVs na mionzi mikali.

umefanya vizuri kuongezea hiyo kitu mkuu. asante sana.
 
Basi mseme tusile tu nyama, isiyoiva ni tegu/minyoo iliyoiva kansa.
Mi kwa imani yangu kansa hutokana na cell misbehaviour tu. Narudi, narudi
 
Ukiotea buffet la kempiski, hyatt au southern sun hayo yote unasahau. We bana wee msosi kitu kingine bana. Mtoe na dem wako atleast twice uone kama atakuacha. Lol
 
Nilitegemea na kuku wa kizungu (broilers) watakuwemo. Kumbe hawaenezi kansa ngoja niendelee kujinona tu.
 
Mzizi mkavu thanjs kwa darasa sasa watu wataishije??na hizo ndo common food world wide.what is the solution the??
 
Mbona kama vyakula vyote vimetajwa kuwa vina madhara....me nafikiri hoja ile ya too much is harmful ipo sahihi.maana kila siku tafiti zinakuja na majibu ya kuwa kila binadamu anachofanya ni sumu...
 
Back
Top Bottom