TAMISA :Watanzania tunataka wanufaike na pesa za manunuzi sekta ya madini, walau kufikia asilimia 30 ya trilioni 3.1 kila mwaka

TAMISA :Watanzania tunataka wanufaike na pesa za manunuzi sekta ya madini, walau kufikia asilimia 30 ya trilioni 3.1 kila mwaka

informer 06

Senior Member
Joined
May 11, 2024
Posts
184
Reaction score
170
Mwenyekiti TAMISA, Peter Kumalilwa amesema kwamba kutoka taarifa ya Wizara ya madini kupitia Waziri, Anthony Mavunde kuonesha kwamba kiasi shilingi trilioni 3.1 kimekuwa kikitumika kila mwaka katika manunuzi yanayofanywa na wawekezaji kwenye madini, amesema kwamba wamejipanga kuhakikisha wanapandisha asilimia kwenye kiwango kinachobakia ndani kwenye manunuzi hayo.

Hayo yameelezwa leo Mei 14, 2025 Jijini Dar es Salaam, na Kumalilwa ambapo amesema kwamba Waziri Mavunde amekuwa akiongelea kuwa katika sekta ya madini kuna kiasi cha shilingi trilioni 3.1 ambayo inatumika kila mwaka katika manunuzi ambayo angependa Watanzania wanufaike nayo.
1c35943e-514b-48ab-a05c-44165e0d7b9e.jpeg

Amesema kuwa wadau hao wanaosadia watanzania wanaotoa huduma kwenye sekta ya madini, imejipanga kuhakikisha inahamasisha na kuchochea uwekezaji ambao utachangia kiwango cha fedha kinachobakia nchini kwenye manunuzi kinaogezeka.

“Kuna migodi mikubwa nchini kama mitano, ambayo wao kila mwaka wanafanya manunuzi ya shilingi trilioni 3.1, ambapo sisi Watanzania tunanufaika kwa karibu asilimia 10 tu, kiasi hiki ni kidogo sana,” amesema Bw. Kumalilwa.

Kwa kulitambua hillo ameeleza kwamba TAMISA imeweka mikakati ya kuhakikisha Watanzania zaidi wanaanzisha viwanda vya madini na kushiriki kikamilifu katika sekta hiyo ili kuweza kunufaika japo na asilimia 30 ya kiasi hicho shilingi trilioni 3.1 za manunuzi ya sekta ya madini.

“Kwa sasa hivi sisi Tanzania tunasheria ya local content, kwa wakati wangu kama Mkwenyekiti wa TAMISA nitahakikisha Watanzania wananufaika na shilingi trilioni 3.1 za manunuzi japo kwa asilimia 20 hadi 30,” alisema Bw. Kumalilwa na kuongeza,

“Tumekuwa tukilalamika sana kuhusu Wachina wanakuja nchini wanachukua kazi zetu, sasa sisi kama TAMISA tumekuwa tukihakikisha kwamba tunawajengea uwezo Watanzania ili waweze kushiriki katika uchumi wa sekta ya madini nchini,” alisema Bw. Kumalilwa.

Awali akitangulia kuzungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Kamati ya TAMISA, Masoko na Mawasiliano, Dk. Sebastian Ndege amesema kwamba Waziri wa madini Anthony Mavunde anatarajiwa kuzindua Kamati ya Chama cha Wasambazaji wa Sekta ya Madini Tanzania (TAMISA), uzinduzi ambao utaambatana na kufanyika kwa Kongamano la Kuwaunganisha Watanzania waliopo katika sekta ya madini Mei 16, 5 2025 Jijini Dar es Salaam.
1a2f2ec3-f029-43e4-a402-b483aa8d5812.jpeg

Ikumbukwe TAMISA ilizinduliwa Septemba 15, 2024 na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, ikuwa na malengo makuu ya kutetea wasambazaji wa sekta ya madini, kuboresha uwezeshaji wa biashara, kutetea haki za wasambazaji na kuendeleza utafiti na ukuaji wa teknolojia.
 
kwenye tittle kuna tamesa, kwenye content kuna tamisa, which is which threader?

halafu huyu peter kumalilwa ndo peter andrew kumalilwa au ni mwingine?
 
Back
Top Bottom