DOKEZO TAMISEMI chunguzeni rushwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali katika shule ya sekondari Mvuti

DOKEZO TAMISEMI chunguzeni rushwa na matumizi mabaya ya fedha za serikali katika shule ya sekondari Mvuti

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Amri kuu ni Upendo

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
789
Reaction score
489
Nimewiwa kuandika haya kutokana na ukimya wa kile kinachoendelea katika shule ya sekondari Mvuti iliyopo Halmashauri ya Jiji Ilala katika kata ya Msongora mtaa wa Kiboga tangu mwishoni wa mwaka 2019 alipoondolewa Head Master aliyekuwepo na kuletwa Headmaster Mpya aliyepo mpaka sasa!

Je nini kinatia wasiwasi?

Tangu shule hii iletewe Headmaster mpya, miradi mingi mfululizo, tena isiyokuwa na mpangolio maalumu ilianza kumiminika. mfano mradi wa ujenzi wa madarasa takribani 30, mradi wa viwanja vya Michezo wa takribani million 50, mradi wa ujenzi wa mabweni ya wavulana na wasichana, mradi wa ukarabati wa Madara takribani 20 ya zamani, mradi wa jengo jipya la ofisi ya walimu, mradi wa Jiko la shule na sasa mradi wa mabweni mengine mawili ya wasichana na wavulana ambayo yapo kiwango cha Msingi.

Chakushangaza tangu miradi hii ilipoanza mkuu wa shule (bila shaka Kwa kushirikiana na maafisa wa juu kiasi) waliua bodi ya shule na hivyo kufanya mambo bila uangalizi wala ushauri wa bodi . (Hapa nadhani bodi iliuawa Ili kutoa mwanya wa ufujaji wa fedha za umma bila uangalizi wowote,) kumbuka shule imekuwa haina bodi ya shule toka mwaka 2020 mpaka leo hii inaendeshwa Kwa maamuzi ya mkuu wa shule pekee!!

Kutokana na kukosekana Kwa bodi wanafunzi wamekuwa wakipata adhabu za kufukuzwa shule Kwa kauli ya mkuu wa shule tu na kakikundi kadogo ka walimu pasipo kuhusisha bodi ya shule!! Je hii ni sawa?

Suala jingine Sugu ni rushwa wanazotozwa na kutoza wazazi wa watoto wanaopaswa kukaa Bweni sawasawa na maelekezo ya serikali! Ni jambo la kusikitishwa kwamba mkuu wa shule Kwa kuwashirikisha wazazi aliingiza sheria kandamizi kwa watoto waishio Bweni, kwamba kila mtoto asiyefikisha divisheni 3 katika annual examination anaondolewa bwenini ama analazimishwa kuhama shule hiyo!

Jambo hili limefungulia mlango mpana wa rushwa kwani licha ya serikali kuagiza kwamba elimu itolewe bure hapa wazazi wamekuwa wakitozwa fedha kiasi cha shilingi 500,000/= hadi 1,000,000 Ili kupata nafasi za Bweni Kwa watoto! Kibaya ni kwamba pamoja na wazazi hawa kutozwa rushwa kubwa kiasi hiki watoto wao hawana uhakika wa kusoma shule hii hadi kuhitimu kwani kila mwisho wa mwaka wale wote wasiopata divisheni 1 hadi 3 hutimuliwa bwenini bila huruma pasipo kujali kiasi kikubwa walichotozwa kiharamu Ili kupata nafasi ya bwenini, wachache wanaotoa hela kubwa tena watoto wao hurusiwa kukaa hostel licha ya kuwa walipata divisheni 4 hadi 0.

Ukitembelea shule hii pindi shule zinapofunguliwa mwezi wa 1 hakika utawaonea huruma wazazi wanavyolia watoto wao kuondolewa Bweni wakati makazi yao ni mbali sana na shule.

Ukiachilia hilo la rushwa jingine ni miradi ya kiwiziwizi. Mpaka sasa shule hii ina wanafunzi takribani 1200 huku ikiwa na madarasa zaidi 38 huku yanayotumika ni madarasa 25 yaliyobaki yote hayana matumizi. Sasa mbali na kuwa na majengo mengi ya madarasa yasiyotumika bado shule imeendelea kupokea miradi ya madarasa mengine takribani sita!

Huu ni upuuzi wa hali ya juu unaofanywa na viongozi kwani Kuna maeneo mengi dar es salaam na Tanzania Kwa ujumla shule hazina madarasa lakini mkuu wa shule na afisa elimu wa ilala (ambaye ni rafiki yake) wamekuwa wakiridhia miradi hiyo kuletwa Mvuti Ili kupata wasaa mzuri wa kupiga pesa za umma wakijua hakuna bodi ya shule.

Kwa mfano mradi wa viwanja vya Michezo serikali ilileta million 50 tangu mwaka 2023 lakini viwanja hivyo havijakamilika hadi hivi sasa na pesa ililiwa na hakuna dalili ya kuvikamilisha.

Haya ni machache tu kati ya maovu mengi yanayofanyika katika shule ya sekondari Mvuti ambayo mkuu wa shule wa sasa pengine na afisa elimu wake wanahusika nayo moja kwa moja

Nashauri ofisi ya Rais TAMISEMI itume maafisa wake wakachunguze kama si kukomesha rushwa na ubadhirifu wa fedha za umma unaofanywa na viongozi katika shule ya sekondari Mvuti.

Ndimi whistle blower
 
Back
Top Bottom