DOKEZO TAMISEMI iangalieni hii shule ipo Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Retina

JF-Expert Member
Joined
Mar 6, 2015
Posts
1,039
Reaction score
1,163
Leo tarehe 01/07/2023, nilienda kutembelea shule ya sekondari yenye kidato cha I-vi Nasibugani high school , shule hii ipo tarafa ya Kisiju, kata ya Msonga halmashauri ya wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani, ipo km 48 toka halmashauri ya wilaya ya Mkuranga, kijana wangu amechaguliwa kusoma tahasusi ya CBG. Ilibidi nifunge safari kimya kimya mpaka Nasibugani huko Mkuranga.

Hii shule unaweza kusema imetelekezwa, haina miundo mbinu ya kukidhi wanafunzi kusoma, licha kidato cha tano na sita tangu 2015.

1. Kuifikia hiyo shule haina barabara rasmi. Kutoka Mkuranga unapanda basi hadi kituo kinaitwa mavunja, ukitoka mavunja unapanda pikipiki mpaka eneo la wazi kipindi cha masika wanafunzi wanavushwa na mtumbwi hii ni hatari sana.

2. Haina miundombinu ya maji, kuna tanki moja na kisima kimoja ambacho hakikidhi mahitaji ya wanafunzi

3. Haina umeme wa gridi ya taifa licha ya umeme huo ukiishia kijijin, mita 800 toka shule.Tangu 2015-2023 shule inatumia miundo mbinu ya umeme wa jua ambayo ni mibovu baadhi ya mabweni hayana solar wakati shule imezungukwa na mapori.

4. Shule haina hospital inayokidhi mahitaji ya wanafunzi kiafya. Kituo cha afya kipo km.10+ toka shule,barabara ni ile yenye swamp ambayo kwenye masika haipitiki, kwa dharura haifai.

TAMISEMI njooni muione hii shule.
 
Nimesoma hapo mkuu pazur mno, acha woga kama kijana wako ni wakiume hapo patamfaa askari huyo.
 
Kuna dokezo lingine limetolewa..
Huenda wamepuuza au hawajasoma.

Wapigieni simu.
 
Back
Top Bottom