TAMISEMI ingilieni kati manyanyaso haya ya wilaya ya Songwe

Njaa kali30

Member
Joined
Jul 18, 2021
Posts
47
Reaction score
28
Kwa heshima na taaadhima ninaomba malalamiko haya yawafikie tamisemi na wizara ya elimu.

Imekuwa tabia ya muda mrefu sana kwa watumishi wanaofanya kazi katika halmashauri ya songwe kukaaa kituo kimoja kwa mda mrefu mfanyakazi anaweza kukaakituo kimoja zaidi ya miaka 13.

Wafanyakazi wamekuwa wakiomba kuhamishiwa vituo vingine lakini cha ajabu wamekuwa wakikataliwa mimi nina zaidi ya miaka 15 kwenye kituo kimoja nimeomba kuhama nakataliwa imekuwa kama kazi za kukomoana. Mazingira yenyewe magumu balaaa ukipitwa ngari moja kulipata jingine mpaka siku inayofuata jamani hebu tamisemi na wizara ya elimu itusaidie.

Pili wilaya hii pamoja na kuwa matokeo mabovu ni wilaya ambayo watu hawaendi likizo wala kupumzika. Kwani kazi zote muhimu ufanyika wakati wa likizo ambapo mfanyakazi hutakiwa kupumzika. Sasa wakubwa wanakwambia muda huo ndio watu hutakiwa kuwafanya kazi wamekuwa kama mabosi wa kihindi ukisimama wanadhani hufanyi kazi bora akutume uchezee aharubu zake ni hatari sana.

Tamisemi tukumbukeni wakati wa mapumziko watu wapumzike kweli na silonglongo
 
Hayo siyo manyanyaso kwani pia kuhamahama ni usumbufu mkubwa. Mfanyakazi anayehamahama mara nyingi anashindwa kujiwekea msingi imara wa maisha baada ya kustaafu.

Unapaswa kutafuta fursa hapo ulipo ili kujiwekea msingi wa maisha ya baadaye.
 
Ivi Ileje unaweza kuwekeza nini kule??very interior
 
Ileje ni wilaya pekee iliyopakana na nchi mbili za Zambia na Malawi nyanda za juu kusini. Ileje inafunguka kupitia Tunduma kwenda Zambia na pia Isongole kwenda Malawi na Zambia. Njia zote mbili ni za barabara ya lami, yaani kutoka Mbeya -Mpemba kwenda Tunduma na Isongole.

Biashara za aina zote kama mazao, bidhaa za viwandani, usafiri na usafirishaji zote zinafanyika. Hivyo karibu ileje uwekeze hata biashara ndogo ya nyumba za kulala wageni na huduma nyingine za kijamii.

KARIBU SANA ILEJE
 
Lakini mtoa mada anaizungumzia songwe na sio ileje au nimekosea
 
Ivi Ileje unaweza kuwekeza nini kule??very interior
Nilishafika kule, wekeza kwenye kilimo bossi, fuga hata kuku wa kienyeji kwa wingi kabisa uza mayai na kuku huko mjini.
Hii inalipa sana.
 
sasa kama uko mazingira mabovu sana, Si uanze kuwa mkorofi tu.

kwenye vipindi 32 vya wiki gonga 16,

kuwa na bifu na Mwl mkuu na mratibu.

tafuta waganga saba waje ufanye igizo la kuzindika kiti unachokalia.

ndani ya wiki utahamishwa kwenda kituo kingine.

lkn na wewe, miaka 15 hujapapenda tu?

kama VP kaweke makazi ya kudumu unapopenda kisha huko kituoni uende j3 asubuhi na unaondoka ijumaa mchana.

usafiri nunua pikipiki. naamini utazingatia ushauuri Wa mwisho, Wa kwanza utakudhuru
 
Kwa heshima na taaadhima ninaomba malalamiko haya yawafikie tamisemi na wizara ya elimu.

Imekuwa tabia ya muda mrefu sana kwa watumishi wanaofanya kazi katika halmashauri ya songwe kukaaa kituo kimoja kwa mda mrefu mfanyakazi anaweza kukaakituo kimoja zaidi ya miaka 13.

Wafanyakazi wamekuwa wakiomba kuhamishiwa vituo vingine lakini cha ajabu wamekuwa wakikataliwa mimi nina zaidi ya miaka 15 kwenye kituo kimoja nimeomba kuhama nakataliwa imekuwa kama kazi za kukomoana. Mazingira yenyewe magumu balaaa ukipitwa ngari moja kulipata jingine mpaka siku inayofuata jamani hebu tamisemi na wizara ya elimu itusaidie.

Pili wilaya hii pamoja na kuwa matokeo mabovu ni wilaya ambayo watu hawaendi likizo wala kupumzika. Kwani kazi zote muhimu ufanyika wakati wa likizo ambapo mfanyakazi hutakiwa kupumzika. Sasa wakubwa wanakwambia muda huo ndio watu hutakiwa kuwafanya kazi wamekuwa kama mabosi wa kihindi ukisimama wanadhani hufanyi kazi bora akutume uchezee aharubu zake ni hatari sana.

Tamisemi tukumbukeni wakati wa mapumziko watu wapumzike kweli na silonglongo
Wasalimie Kamsamba
 
Back
Top Bottom