Taiq
Member
- Feb 14, 2023
- 99
- 90
Habari za leo?
Ndugu zangu nimefikia uhamuzi huu wa kuuliza ni kwa nini Tamisemi haitoi majina ya watumishi waliopata uhamisho?
Jibu ninalofikiria binafisi ni kutokana na kuwepo na uvunjifu wa sheria za uhamisho na hivyo basi wahusika kuamua kuficha uvunjifu huo.
Hivi karibuni kumekuwepo na vitendo vya ukiukwaji wa kisheria na taratibu za uhamisho. Vitendo hivyo vimekuwa vikilatibiwa na baadhi ya watumishi wa umma na hasa wanaohusika na uhamisho. Baadhi ya vitendo hivyo ni:-
1. Uhamisho wa watumishi wanaobadilishana vituo vya kazi umekuwa janga. Mfano mnabadilishana na mwenzio, lakini mmoja anahamishwa na mwingine anabakishwa. Na hili limewezekana tu kwa kuwa hakuna majina ya uhamisho.
2. Baadhi ya watumishi wanahamishwa hata bila ya kutimiza vigezo vya kitumishi. Mfano mfanyakazi ameajiliwa mwezi wa sita na mwezi wa saba anahamishwa. Hili limewezekana kwa sababu hawatoi majina na pia uhamisho huo ni nje ya mfumo.
3. Kitendo kingine kinahusu tamisemi ofisi namba 46 kuwa na majibu mepesi na yasiyo na uthibitisho kwa wanaotembelea ofisi hiyo. Mfano mtumishi aliomba uhamisho na hakujibiwa. Anapoenda tamisemi kufuatilia huonyeshwa orodha ya waliohama na anapoona jina lake kwenye orodha hiyo, kisha kuomba kibari chake, hujibiwa tutatuma.
Lakini mpaka hii leo vibari bado havijatumwa na wahusika wako kimya. Hivyo basi tunaomba majibu yao yawe ya maandishi ili kubakiza uthibitisho kwa mtumishi. Uthibitisho ni muhimu ili kumwezesha mtumishi kufuatilia hatua nyingine.
4. Ufutaji wa maombi ndani ya mfumo wa ESS si haki. Mwezi uliopita niliona maombi ya watumishi waliomba mwaka jana kilifutwa ndani ya mfumo wa ESS bila ya kujibiwa. Hili lilifanyika ili kupoteza ushahidi. Hivyo basi tunawaomba wahusika kurekebisha mfumo ili kuruhusu mtumiaji kuchukua hatua zote za uhamisho na kutunza nyaraka zake yeye mwenyewe. Kwa kufanya hivyo itasaidia yeye binafisi pale ambapo haki haitatendeka.
Mwisho naiomba serikali ilejeshe utaratibu wa kutoa majina ili kuokoa muda unaotumiwa na watumishi kufuatilia na pia kurahisisha ufuatiliaji wa haki za waombaji ambao hayakujibiwa na vibari vyao pia havikutumwa.