Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Lengo la huu uzi ni kutaka tu kuwakumbusha ndugu zangu wa Tamisemi. Baada ya Mh. Rais kuiagiza Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) kuajiri walimu 6000 kutokana na uhitaji ulio sababishwa na vifo na kuacha/kufukuzwa kazi kwa baadhi ya walimu, natarajia zoezi linalo fuata ni kwa hii Wizara husika kutekeleza agizo la Rais Mh. Samia Suluhu Hassani.
Ombi langu kwa Tamisemi ni moja tu! Watoe kipaumbele kwanza kwa walimu zaidi ya 3000 wanao jitolea kwenye shule zetu kwa miaka nenda huku wakiwa na matumaini ya kukumbukwa siku moja katika ajira rasmi za serikali.
Kiufupi walimu hawa wenye elimu ya stashahada na shahada za elimu, wanafanya kazi ya kujitolea katika mazingira magumu sana mashuleni huku wakilipwa posho kiduchu tu ya laki 1 mpaka laki 1 na nusu na wakuu wa shule, lakini pia ile Taasisis ya TAESA kwa mwezi!
Walimu hawa kimsingi ni viumbe wenye moyo sana! Hivyo naomba ikiwapendeza, muwape kipaumbele! Badala ya kujaza ndugu zenu, mashemeji zenu, wake zenu, waume zenu, watoto wenu, ndugu zenu na wale walio wapa rushwa! Huku mkiwaacha watoto wa maskini wakiendelea kuishi kwa matumaini ya kukumbukwa na serikali siku moja. Mkumbuke hawa walimu wengi wanatokea mazingira magumu kiasi cha kuaamua kujitolea!
Nawasihi sana safari hii muache ule ujanja ujanja wenu wa kuchomekea majina hewa, au kurudia majina ya watu kwa makusudi, ili baadae mje mchomekee majina mengine kwa malango wa nyuma. Wapeni nafasi hao walimu elfu 3 kwanza, halafu hao elfu 3 wengine, mnaweza sasa kuangalia vipaumbele vyenu.
Nb: Mimi si mmoja wao. Ila nimeguswa na hawa walimu, pamoja na wale wahitimu wa kada nyingine ambao wanajitolea kufanya kazi serikalini, huku wakilipwa posho ya laki 1 na nusu na hao TAESA kwa ajili ya nauli.