DZUDZUKU
JF-Expert Member
- Nov 8, 2012
- 3,909
- 2,115
Habari ndugu wana jf.
Toka enzi za baba wa taifa watu walikuwa wakiiamini serikali na kuona serikali ndio chanzo chao kikuu cha habari, lakini kutokana na sijui niite uzembe/ukosefu wa uadilifu, kila siku miaka inavyo kwenda watu wanazidi kupunguza imani na serikali yao.
Serikali imekuwa ikitamka mambo isiyo tekeleza au hata kama watatekeleza basi hawatekelezi kwa wakati sahihi.
Kuna mambo mengi lakini mimi nataka niligusie kidogo hili suala la ajira kwa walimu.
Serikali kupitia tovuti yake ya TAMISEMI ilitangaza kutoa majina ya ajira mpya za walimu 2013/2014 mwezi wa tatu tarehe 15, lakini matokeo yake hawajafanya hivyo.
Kuto toa hayo majina sio tatizo sana, tatizo linakuja pale ambapo majina hayo ambayo ilibidi yatangazwe serikalini tunayakuta kwenye blog mbali mbali na sio kwenye tovuti ya serikali, HII NI AIBU kubwa kwa serikali.
Inakuwaje taarifa muhimu kama hii ianze kupatikana facebook au kwenye blog badala yenu?
Mmejishushia hadhi yenu na imani kwenu.