LGE2024 TAMISEMI: Msifiche taarifa toeni lakini mlinde amani

LGE2024 TAMISEMI: Msifiche taarifa toeni lakini mlinde amani

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
24,941
Reaction score
28,869

Dkt. Grace Magembe naibu katibu mkuu OR TAMISEMI awapa ukweli waandishi wa habari na serikali kwenda kijiditali katika kuelimisha umma wakati wa semina ya kuwajengea uwezo Waandishi wa Habari wasambaze taarifa sahihi na hasa kipindi hiki kuelekea 27 November 2024.

Dkt. Grace Magembe anasisitiza taarifa ziwe zinalenga zaidi wananchi wasikie wagombea wananadi sera gani, na kutambua umuhimu wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji pia kuzingatia weledi taaluma na haki kwa wagombea wa vyama vyote bila upendeleo.

Dr. Grace Magembe asisitiza habari zizingatie amani, upendo na siyo kuchochea taharuki.
 
Kazi kweli kweli uchafuzi wa mchakato wa uchaguzi 2024 usilete taharuki ?
 
CPA Amos Makala na timu ya waandishi wa propaganda toka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam inaoongoza chawa kutoa habari za taharuki kuwa vyama pinzani havijajipanga wala kujianda kwa uchaguzi wa tarehe 27 November 2024
 
CPA Amos Makala na timu ya waandishi wa propaganda toka Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM mtaa wa Lumumba jijini Dar es Salaam inaoongoza chawa kutoa habari za taharuki kuwa vyama pinzani havijajipanga wala kujianda kwa uchaguzi wa tarehe 27 November 2024
Makala ni shida ya akili tangu kitambo sn namjua
 
13 November 2024
Mbeya, Tanzania

UCHAGUZI 2024 : Mgombea wa CHADEMA anashikiliwa na Jeshi la Polisi Mbeya

View: https://m.youtube.com/watch?v=8IjvFy3z0Aw
Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mbeya kamanda Hamad Mbeyale akiongea kuhusu uchafuzi wa mchakato wa Uchaguzi wa serikali za mitaa 2024, kuwa wagombea wa CHADEMA 300 wakati wa uteuzi wamewekewa pingamizi na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ... kwa kutumia kanuni za kufikirika zisizokuwepo ktk miongozo, kanuni na sheria za TAMISEMI ..

PIA Kwa mfano zengwe jingine mmoja wa wakata rufani dhidi ya kuenguliwa amekamatwa na vyombo vya dola ili asiweze kufuatilia rufani ya kuenguliwa mfano mgombea nafasi ya uenyekiti katika kijiji amekamatwa na Polisi...

Katibu wa CHADEMA mkoa wa Mbeya kamanda Hamad Mbeyale anasema mizengwe hii dhidi ya wagombea wa CHADEMA ...ili wasipate haki ya kugombea na pia wananchi kutopata nafasi ya kuchagua viongozi wa ngazi za mashinani 2024 ni kinyume na katiba ya nchi pia zile 4R na maombi ya Dr. Emmanuel Nchimbi kwa rais Samia Hassan kuhusu wagombea waruhusiwe kushiriki uchaguzi huru usio na mizengwe ...
 
Back
Top Bottom