Kwa faida ya wengi na kuondoa sintofahamu kwa wasiofahamu, Ofisi ya Rais TAMISEMI fanyeni marekebisho ya machaguo ya wanafunzi kwenye eneo la Wilaya Shule ilipo. Miaka ya nyuma hili kosa halikuwahi kujitokeza bali lilianza kuonekana kwenye selection za mwaka 2023 na mwaka huu. Nipo tayari kurekebishwa kama siko sahihi.
Nimepitia machaguo husika kwa shule kadhaa na mikoa tofauti kwa shule ninazozifahamu na nimehitimisha kwamba OR-TAMISEMI kuna kosa mlifanya katika kuonesha shule anayoenda mwanafunzi husika ipo Wilaya gani.
Mfano, Shule ya Sekondari Kilakala inaoneshwa kwamba ipo Manispaa ya Bukoba, Kagera River ya Karagwe inaoneshwa ipo Manispaa ya Bukoba, vilevile kwa Geita Girls ya Geita.