KERO Responded TAMISEMI tembeleeni waajiriwa wenu kwenye vituo vya kazi hasa ajira mpya hawapokelewi vizuri

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Serikali hasa TAMISEMI watoe tu uhamisho hata kama hajamaliza miaka mitatu, haswa kwa hawa watumishi wapya!

Kuna baadhi ya wilaya za pembezoni kama mkoa halmashauri zao, watumishi wapya wanapokuja hawapokelewi vizuri vituo vyao vya kazi.

Watumishi wapya wanapoleta chachu nzuri ya maendeleo hasa katika taaluma, wazee wa zamani wanasema wanatumia experience kuliko taaluma, hasa upande wa afya MADMo wanatumia experience kwenye vituo baadala ya kupewa wataalamu waliokuja.

Pamoja na kuweka watu kwenye huduma au unit wenye sifa ila wanawekwa watu wasio na sifa kwenye hiyoo huduma kisa experience?

Mazoea ni mengi sana TAMISEMI, tembeleenI watumishi wenu kwenye vituo vyao vya kazi hasa upande wa afya ni hovyo kweli mpangalio.

Pia soma ~ Ridhiwani Kikwete: Kuna matumizi mabaya ya madaraka katika Ofisi za Umma, Watumishi wanalalamika
 
Twende pole pole bila kuumizana tutafika TU 😂, sehemu nzuri
 
Nani ajisumbue? Hakuna anayejali. Nafikiri Bora utaliwe na mkoloni mweupe kuliko Hawa manigger
 
Boss experience ni muhimu sana hilo huwezi kulipinga. Unatakiwa ukae chini ujifunze uonyeshe uwezo uwashawishi watu kwamba unaweza wakuachie kitengo. Unadhani ni rahisi kufika na kukahidhiwa idara au department? 😁
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…