LGE2024 TAMISEMI: Ujasiriamali ni kazi halali, si sahihi kuwaengua Wagombea kwa kigezo hicho

LGE2024 TAMISEMI: Ujasiriamali ni kazi halali, si sahihi kuwaengua Wagombea kwa kigezo hicho

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) imesema ujasiriamali ni kazi halali inayotambulika kiserikali, si sawa kutumika kuwaengua wagombea kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Hayo yamesemwa leo Jumanne, Novemba 12, 2024 na Mwanasheria wa Tamisemi, Mihayo Kadete wakati akijibu maswali kwenye kikao kazi na wahariri kinachofanyika jijini Dar es Salaam.

Kadete amesema si sahihi mgombea kuenguliwa kwa kigezo tu amejaza kazi halali ni mjasiriamali; na mtu aliyeenguliwa akate rufaa kwa kuwa hiyo ni kazi halali.

Kadete amesema mgombea ambaye hajajiandikisha kupiga kura kwenye eneo lake ni moja ya sababu ya kukosa sifa ya kugombea katika uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 27, 2024.

"Mtu akatwe kwa kukosa sifa na si kukatwa kwa kudhamiria bali akatwe kwa haki," amesema Kadete.

Semina hiyo ya siku moja ya masuala ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 imeandaliwa na Ofisi ya Rais -Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

MWANANCHI
 
Tengeneza tatizo mwenyewe, then unalitatua, kujijengea uaminifu.
Poor CCM.
 
Ujasiriamali sio ujasiriamwili kama nilivyodhania mimi. Najua wagombea wengi wa kike CCM wamepita japo walijaza ujasiriamwili kwenye fomu zao
 
Back
Top Bottom