Ifike mahali sasa OR-TAMISEMI wapunguziwe majukumu. Kwa kiasi fulani nadhani nao ni sehemu ya kuharibu ubora wa elimu nchini. Najua TAMISEMI wanahusika na TSC, TARURA, DART, Afya, Elimu, etc yani kwa ufupi ni kama wapo kila kona, pamoja na hayo eneo ambalo unaweza kuona wamejikita na wanasikika zaidi ni Afya na Elimu.
Mimi nazungumzia upande wa elimu. Elimu inatakiwa kuwa process oriented na less results oriented. Ili tupate elimu ilivyo bora tunatakiwa tujikite zaidi katika mchakato, utaratibu na namna bora ya utoaji wa elimu, yani zaidi ya 90% ya malengo na uwekezaji wetu tujikite huko. Bahati mbaya zaidi effort kubwa sana zimewekwa kwenye matokeo. Hii inathibitishwa pale ambapo mazingira ya shule ni mabovu watu hawajali lakini matokeo yakitoka inakuwa wimbo wa taifa.
Na walioasisi na kuendeleza huu upuuzi ni TAMISEMI. Yani utendaji kazi mwingi kwao ni zimamoto, yani kila siku wao wanaandaa template za taarifa yani sijui jukumu lao la msingi hasa ni lipi. TAMISEMI wameanzisha mitihani ya shule kongwe, sasa hivi wanafuatilia taarifa za mitihani ya mock wilaya 😀😀. Tena pale wasaidizi wa Katibu Mkuu ni Dr. Musonde na Bw. Kayombo ambao wote ni results oriented. Walikuja na calendar ya ufundishaji sijui walitoa wapi ikashindikana, sasa wamekuja na KPI, yani shule mnatakiwa kila wiki muwe na vikao kuhusu kufundisha (wakilenga matokeo)
Afisa Elimu sijui ukague shule 10, sidhani kama kuna taifa lina utaratibu huu hasa wale wanaosifika kuwa na elimu nzuri. Na hapo wanajiona wabunifu. Mimi Naamini matokeo mzuri ni process, mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia. Fikiria kwa nini pamoja na kuwa kuna wanafunzi wanafaulu vizuri sana lakini kwenye soko la ajira hawafiti? Ni sababu processes walizopita katika elimu inamapungufu. Mnaanzisha mambo mengi yasiyo na tija sijui ni maeneo ya ulaji?
Nashauri sehemu kubwa ya usimamizi wa mchakato wa ufundishaji na ujifunzaji ibaki wizara ya elimu, angalau kule huwa naona wanaelewa japo wanazidiwa nguvu na hao TAMISEMI.
Kuna suala la mifumo (ffars, ASC, sensaelimumsingi, madenimis, SIS etc) hii mfumo yote inatumika shuleni na inasimamiwa na TAMISEMI, unajiuliza hawa jamaa wapo serious? Yani they can't make a single strong and comprehensive system utakao fanya kazi hizo? Kwa nini mtu asi log in and find an interface with all that features. Na katika hiyo mingine ni useless. Ni ilimradi tu walimu huko shuleni wasumbuliwe tu.
Mh. Rais angalia kwa umakini kabisa utendaji kazi wa TAMISEMI uone kama kweli inapaswa kuendeleza kuhodhi majukumu ambayo wanaaribu badala kujenga. Upendeleo sasa na rushwa kwenye nafasi za uongozi na uhamisho ni balaa tupu. Kuna upuuzi mwingi sana pale.
Kwa sababu wao ndio wasimamizi wa mamlaka za serikali za mitaa, nashauri wangebaki kuwa wasimamizi na wafuatiliaji tu, mambo mengine yote yarudishwe kwenye wizara husika. Fanya research utabaini hata watumishi walio wengi wanatamani kuondoka TAMISEMI, sasa kwa kuwa ni ngumu basi TAMISEMI wabaki kama nilivyoshauri. Waliweka sifa za uteuzi wa viongozi pia wakasema kila Halmashauri (Elimu msingi na sekondari) kutakuwa na Mkuu wa Idara na wasaidizi wake 4, waulize watekeleza hivyo nchi nzima? Hii wizara ni changamoto sana.