Tembea uone mambo usingoje kuambiwa.
Hii nchi wengi wakipenda kusema ni ngumu, kwa kweli ni ngumu sana. Ama kwa hakika huenda hata sheria zinazotumika kunakoitwa mjini ni tofauti mno na za huko shamba.
Nimeyaona ushirombo ambako labda Waziri Bashungwa hata hajui wizara yake kuwa imeshikwa mateka vilivyo.
"Kwamba mabasi ya abiria hulazimishwa kuingia stendi za uchochoroni hata kama hayashushi au kupakia abiria hapo, hili ndilo chanzo chote cha mzizi wa fitna."
Zaidi sana sera hii lazimishi mbona ina yake mambo hapo ushirombo - kwake Mh. Dotto Biteko?
"Hapo bila shaka rasmi kazini kuibia watu, pana midume 2 yenye njaa kali ya rushwa iliyopitiliza. Hii huendesha gari - Toyota Harrier nyeupe wakiita tako la Nyani, namba za usajili DQJ XYZ.
Miwili hiyo huyavizia na kuyakimbiza mabasi yanayodaiwa kutosimama hapo ushirombo au eti kutoungia stendi.
Ajabu ni kuwa midume hiyo haina uniform wala vitambulisho, ikitumia gari binafsi!
"Kwa maneno matupu ikidai eti ni mifanyakazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ushirombo."
Yasemekana ni jadi yao kuwatishia wenye mabasi kwa faini za papo kwa papo za 250,000/= au rushwa za 50,000/= eti kwa kutokuingia stendi.
Kupisha usumbufu ndugu hawa yasemekana wamekuwa wanavuna mapesa kweli kweli. Itakuwa bila shaka hata yale makali ya vita kule Ukraine kwao ni hadithi tu.
Yote tisa. Dar - Kagera bus halina abiria wa kupanda au kushuka. Kulikoni kulazimishwa kuingia stendi uchochoroni?
Kulikoni nchi na tamisemi kuwepo mianya ya kugeuzwa shamba la bibi?