Tamisemi yaitaka Udart kurejesha huduma ya usafiri kabla ya Juni 01

Tamisemi yaitaka Udart kurejesha huduma ya usafiri kabla ya Juni 01

mkiluvya

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2019
Posts
809
Reaction score
729
1590589898081.png

Waziri wa Nchi , ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Selemani Jafo amemuagiza wakala wa mabasi yaendayo haraka UDART kuhakikisha usafiri wa mabasi hayo unarejea kama kawaida kabla ya Juni Mosi, mwaka huu na kuondoa kero ya sasa inayowakumba abiria wanaotumia usafiri huo.

Selemani Jafo amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na msongamano mkubwa wa abiria kwenye vituo vya mabasi hayo kutokana na watu wengi kuanza kurejea kwenye shughuli zao mbalimbali kufuatia kupungua kwa ugonjwa wa corona.

“Ni kweli, baada ya Rais wetu, Dk John Pombe Magufuli kueleza matumaini makubwa ya idadi ya maambukizi kupungua nchini, watu wamerejea kwa kasi katika shughuli za kiuchumi, hii imechangia msongamano pale Kimara nyakati za asubuhi hasa tukikumbuka pia kuwa ni ‘level seat’,” amesema Jafo akizungumza na gazeti la Habarileo.

Jafo amesema kuwa wasimamizi wa mradi huo wamemueleza kuwa mbali na idadi ya watu kuongezeka, lakini idadi ya magari yanayotoa hudumu nayo imepungua, kwani mabasi marefu 30 yapo katika matengenezo.

Aidha, ameagiza magari hayo kufanyiwa matengenezo haraka, kwani kutokana na maisha kuanza kurudi katika hali kawaida, na vyuo kufunguliwa, usafiri huo utahitajika sana kuhakikisha watu wanawahi kwenye shughuli zao.
 
Wana JF huu mradi ni shida bora wangerudisha Daladala zetu kwanza ili tupate unafuu. Au kwa kuokoa jahazi waruhusu mabasi kutoka kwa mtu mwingine kwa mda mpaka hapo hapo UDART wakishatengeneza mabasi yao. Sasa tarehe moja june ndo itakuwa balaa maana wanafunzi wa vyuo nao wataongezeka. Or else watafute mtoa huduma mwingine alete mabasi maana naona kuna nchi jirani yetu ameanza kutengeneza mabasi mazuri sana hata yana pakuchagia simu yangetufaa sana.
 
Lini walisitisha kutoa huduma?.... au warejee huduma kama zamani kwamba wajaze mbanano?
 
Hata majamaa aisee.
Yani ule msongamano w kimara kivukoni ndio wanadhani kuwa ni maisha ya watz wanayoyataka?
Hiki ni tatizo la akili
 
Hata majamaa aisee.
Yani ule msongamano w kimara kivukoni ndio wanadhani kuwa ni maisha ya watz wanayoyataka?
Hiki ni tatizo la akili
Tatizo wanalofanya ni kusomba abiria kutoka mbezi mwisho wanarundika hapo Kimara. Hili ni kosa kubwa sana bora afadhali mbezi tunapanda kwa kupanga foreni sasa kimara ndo balaa na eneo lenyewe pakupandia dogo. Wafute huo utaratibu wa kusomba abiria kutoka mbz mwisho na kuwaleta kimara waache uroho wa ile Tsh.400 kwa kila abiria inayoongezeka mabasi mengine yawe yanatoka Mbezi mwisho hadi route ya Kko-Gerezani au Posta kwa Tsh.650 ni sawa tu. Kama wanaona itatia hasara watutoze Tsh.1000 lakini najua nkipandia Mbezi ntashuka Gerezani-Kko au Posta kuliko shida wanazotupa kupigania tena usafiri Kimara.
Kama hawaamini kwamba tumekasirika wajaribu kuruhusu daladala zetu za zamani za moja kwamoja waone kama tutapanda hayo ya UDART? I wonder kwanini sio creative?
 
Ndio anachomanisha huyu mzaramo nyungu

Duh...

Usafiri wa hovyo sana huo. Wanajaza kama wanapakia magunia ya mkaa bhana. Ule usafiri kwa ujazaji ule kiafya haufai, sio tu kwa janga la covid-19. Ni mateso yale.
 
Duh...

Usafiri wa hovyo sana huo. Wanajaza kama wanapakia magunia ya mkaa bhana. Ule usafiri kwa ujazaji ule kiafya haufai, sio tu kwa janga la covid-19. Ni mateso yale.
Watapata wanachokitaka
 
Mungu atusaidie tu maana nijuavyo mwendokasi ni hatari sana,bora tofali zinakuwa na nafasi ila abiria wa mwendokasi namna wanavyojaa kuna watu watakuja kuregret maamuzi yao
 
Tatizo wanalofanya ni kusomba abiria kutoka mbezi mwisho wanarundika hapo Kimara. Hili ni kosa kubwa sana bora afadhali mbezi tunapanda kwa kupanga foreni sasa kimara ndo balaa na eneo lenyewe pakupandia dogo. Wafute huo utaratibu wa kusomba abiria kutoka mbz mwisho na kuwaleta kimara waache uroho wa ile Tsh.400 kwa kila abiria inayoongezeka mabasi mengine yawe yanatoka Mbezi mwisho hadi route ya Kko-Gerezani au Posta kwa Tsh.650 ni sawa tu. Kama wanaona itatia hasara watutoze Tsh.1000 lakini najua nkipandia Mbezi ntashuka Gerezani-Kko au Posta kuliko shida wanazotupa kupigania tena usafiri Kimara.
Kama hawaamini kwamba tumekasirika wajaribu kuruhusu daladala zetu za zamani za moja kwamoja waone kama tutapanda hayo ya UDART? I wonder kwanini sio creative?
Mbona Coaster zipo nyingi za buku Mbezi-Kariakoo? Nafikiri wameruhusiwa. Level seat kwa UDART ni hasara sana.
 
Haiwezekani magari yote marefu yakawa kwenye matengenezo kwa mkupuo, kuna mchezo mchafu unachezwa hapo wa kutafuta faida bila kuingia garama. Yaani wako tayari usubiri masaa mawili kituoni huku wakizunguushia magari madogo, badala ya kukufanya usubiri dakika 20 kwa kukuletea basi refu.

Migari mirefu ipo kwenye vituo kama vya Feri na vinginevyo yamewekwa tu kama kuku anayeatamia mayai, Hakuna cha matengenexo wala nini, Waziri amedanganya Umma hapo
 
Kwa mtazamo wangu, UDART walisha shindwa kuuendesha huu mradi mrefu sana. Na TAMISEMI nao waliisha shindwa kuwasimamia hawa UDART muda mrefu pia. Ni failure at all levels when it comes to mwendokasi. Kadi ndio hivyo tena haiyasemeki na vishina vya tiketi ndio wizi mtupu. Sijui nani aje auendeshe huu mradi kwa ufanisi. Kama mradi huu ni hiduma wamefeli. Kama mradi huu ni wa kibiashara, wamefeli pia.
Wahusika wa mradi huu wayatatue matitizo yaliypo kwenye mradi huu ONCE AND FOR ALL.
 
You don't need to be an angel to solve this. Wakachukue yale mabasi yanayoendelea kooza pale Ubungo ICD. hivi serekali inasubiri balozi wa marekani awafundishe hata kwenye hili
 
Shikamoo Seye (Hidaya) by Pepe Kalle and The Empire Bakuba.
Usafiri wa mwendokasi leo ndio umekuwa mgumu zaidi.
 
Ubinafishwe. ... Serkalini kun vichwa ila utafikiri wote wameishia LA saba. Waachojua ni matamko tu
 
Back
Top Bottom