Elections 2010 Tamko kwa Tanzania Wote

Mkombozi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2008
Posts
844
Reaction score
476
Kutokana SISIMU kuchafua na kuhatarisha amani kwa kutuma msg za vitisho kwa baadhi ya numba za simu.Naomba wote wasizingatie hizo Msg na waendelee kumchagua kwa kishindo Dr Slaa.Sisimu imeona inashindwa na kutishia wananchi kwa msg.Number +3588108226 imetumika.Kura zote ziende kwa Dr Slaa.Sisimu ikishinda maisha yatakua magumu sana
 
Hiyo ni namba ya wapi tena?...yaonyesha MAKAMPUNI ya simu taratibu nayo yanaDANGANYIKA SASA!
Na ujumbe wa vitisho unasemaje?
Tuma huo ujumbe ili kuongeza mashiko ya bandiko!
 
Ujumbe unasema hivi. Slaa ni mropokaji na mgomvi anatukanah vyombo vya ulinzi na usalama.Anataka damu imwagike ili mradi aingie Ikulu.Tumkatae kugeuza nchi yetu kua somalia.

Pamoja na kwmba imetoka +3588108226 ila utagundua kabisa imetumwa na chama gani na lengo lake ni nini
 

Hivi ni msg ngapi ambazo nanyi mmekuwa mnazituma tena zikiwa na taswira za kibaguzi???

Mnapochagua strategy kumbukeni kuwa wenzenu have more determination and resources za kufanya campaign za aina hizo tena zikawafikia mamilioni ya watanzania na sio persona sms ambazo ndizo mnaweza kuafford.

Wakati nashutumu siasa za kibaguzi na vitisho zinazoendana na msg hizi kiasi kwmba sijawahi kuforward hata moja kati ya makumi nilizozipata na katika nyingene mnazoanzisha kila kukicha katika mitandao kama huu wa jamiiforum, naamini kuwa katika haya hakuna victim.....u r all perpetrators.

Stop agonizing, Be the change u claim you want to see.....
 
Yaani Slaa katungiwa jambo jipya tena!!!...watatunga sana, lakini tushaamua, hatuelewi lingine!
 

I wish ningipata hizo msg ambazo 'sisi' tumeandika za namna hii.
 
Hiyo ni namba ya wapi tena?...yaonyesha MAKAMPUNI ya simu taratibu nayo yanaDANGANYIKA SASA!
Na ujumbe wa vitisho unasemaje?
Tuma huo ujumbe ili kuongeza mashiko ya bandiko!

Hii code ni ya Ireland
 
Yaani Slaa katungiwa jambo jipya tena!!!...watatunga sana, lakini tushaamua, hatuelewi lingine!

Mi yaani hat a wanikate mikono ntapiga kura kwa miguu..siambiwi kit mwaka huu
 
Uchaguzi hauwezi kuwa kitu cha kufa au kopona mpaka tuanze kuzushiana mambo ya hatari kwa usalama wa taifa letu.Na kwa hili mamlaka ya mawasiliano ni lazima inahusika.Jamani baada ya uchaguzi maisha yataendelea.CCM maji yamewafika shingoni.
 

Omary, mimi pia sipendi sana mambo ya ubaguzi na nadhani watanzania wengi hawafuatilii hayo, with exception of some few radicals. Jamii yetu imechanganyika sana na watu wachache tu wasiojua ndio wanadhani unaweza kushinda au kupata kitu kwa sababu ya upendeleo. Ninaamini kabisa hakuna mtu anayeweza kushinda uchaguzi kwa sababu ya aidha kabila lake, dini yake au vitu kama hivyo. Ubaguzi tulionao Tanzania, hasa katika siasa ni UKEREKETWA WA VYAMA! Ni kweli kuna watu wanaingiza hisia za kibaguzi katika kufutia wagombea wao, lakini nadhani ni suala la kupingwa kama sio la kupuuzia.

Issue inayokuja kwenye hizi ujumbe zinazotumwa ni uchochezi, sio hii tu bali zote. kwa nini hawa wanaotuma ujumbe wasitume ujumbe wa kuelezea uzuri wa mgombea wao badala yake wanashambulia wengine? Ukituma ujumbe kusema fulani ni nyoka, au atachochea instability katika nchi nadhani ndio suala baya. hapo unapandikiza chuki au kujenga mazingira ya kuruhusu watu fulani kuanzisha vurugu baada ya uchaguzi. Mi nahsauri kila mtu anayefanya kampeni ni vyema azungumzie zaidi mazuri ya mgombea wake, japo inawezekana kuongelea mazuri kwa kusema mabaya ya mtu mwingine, lakini sio kutukana au kutoa uzushi.
 
Let me find out how I can revenge to this. I dont care how much I can loose for the revenge as far as it is for the benefit of Tanzania and innocent Tanzanians who are suffering the consequence of CCM colonization.
 

Mpiga kelele akiwa kazini
 
Sisi Watanzania hautafika muda tukaamua mambo yetu katika nchi hii yakaenda vizuri! HHivi hizo sms zinazotumwa kweli zimetoka kwa mtu aliyeingia darasani? Nafikiri yule tunayedhania ameandika kwa matakwa ya chama chake atoswe yeye pamoja na chama chake kwa kuwa hawa ni wachochezi wakubwa na wanatafuta uongozi kwa maslahi yao binafsi. Kwa mtu yeyote mwenye akili ya kawaida anajua anayetuma sms hizo hana chochote na hawezi kuwafanyia chochote Watanzania.
Kwanza wanataka wanafunzi wa elimu ya juu wasipige kura; upumbavu wa wazi kwa kuwa ni kuvunja katiba kumnyima mtu haki yake ya kuchagua kiongozi anayemtaka.
Pili wameona wameelemewa, badala ya kutafuta strategy reasonable, wameamua kuzusha kitu cha kipumbavu kabisa ambacho kinaweza kuwafanya watu wazidi kuwachukia wale wale waloandika.
Maswala ya uendeshaji nchi yachukuliwe kwa makini zaidi na siyo mtu akae ashauriwe na mke wake asubuhi aamue kuwapa Watanzania sumu ambayo haina mchango wowote katika maendeleo yao! WATANZANIA MSIDANGANYIKE, CHAGUENI MTU MNAYEMTAKA
 
Kadri wanavyotunga uongo ndivyo wanavyonifanya nizidi kuhamasisha watu kumpigia Dr Slaa kura na chama chake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…