Tamko la ACT Wazalendo kuhusu mlipuko wa Corona

Tamko la ACT Wazalendo kuhusu mlipuko wa Corona

Zitto

Former MP Kigoma Urban
Joined
Mar 2, 2007
Posts
1,562
Reaction score
10,888
Tamko la Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Juu ya Ugonjwa wa Corona

Ndugu Watanzania

A: Utangulizi

Dunia imekumbwa na ugonjwa wa Covid - 19 (maarufu zaidi kama Corona). Nchi yetu kama sehemu ya dunia haijasalimika na kadhia hii. Machi 2, 2020 wakati nikitoa hotuba yangu kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya ACT Wazalendo niliitaka Serikali ifanye tathmini juu ya athari za kiuchumi za ugonjwa huu, na kwa kuwa katika kipindi husika hatukuwa na maambukizi yaliyoripotiwa nchini, nilitaka tathmini husika ijikite kwenye athari za kukosekana kwa malighafi viwandani (Hasa kutoka nje ya nchi), masoko ya bidhaa zetu nje, bidhaa za vyakula tunavyoagiza kutoka nje, athari kwenye sekta ya usafirishaji, utalii nk, na mjumuisho wa hayo kwenye uchumi wetu.

Juzi Serikali imethibitisha uwepo wa virusi vya Corona hapa Tanzania, na mpaka jana idadi ya wagonjwa iliyosemwa imefikia watu Sita (6), Mmoja kutoka Zanzibar, na watano kutoka Tanzania Bara. Hatua kadhaa za kujaribu kukinga na kupunguza kasi ya maambukizi zimetangazwa kuchukuliwa, ikiwemo kuhamasishaji kunawa kwa sabuni kwenye maji yanayotiririka, kutumia vitakasa (Sanitizers), kuacha kupeana mikono, kuvaa barkoa (masks), kupunguza mikusanyiko, kutenga maeneo maalum kwaajili ya wanaogundulika kupata maambukizi, kufunga shule na vyuo, nk.

Taarifa hii ya uwepo wa wagonjwa nchini inakazia juu ya wito wetu ACT Wazalendo wa Machi 2, 2020, juu ya umuhimu wa kufanya tathmini ya athari za kiafya, kiuchumi na kijamii zitokanazo na janga hili la Corona, pamoja na kuja na hatua za haraka, za kati na za muda mrefu za kuchukua ili kupambana na athari hizo.

B: Hatua za Haraka za Kuchukua Kupunguza Maambukizi Nchini

ACT Wazalendo inaishauri Serikali kuchukua hatua zifuatazo kushughulikia suala hili la kujikinga na maambukizi mapya ya virusi vya Corona:

1. Kuzuia safari za kwenda au kuingia nchini za watu kutoka nchi zilizoathirika zaidi na virusi vya Corona, nchi hizo ni China, Italia, Iran, Uhispania, Ujerumani, Uingereza, Canada, Marekani, pamoja na nchi yoyote ambayo itaonekana kuwa na maambukizi zaidi.

2. Kuwahimiza watu wote waliosafiri kutoka kwenye nchi zenye maambukizi zaidi ya vizuri vya Corona ndani ya wiki tatu zilizopita kujitokeza na kufanyiwa vipimo kubaini kama wana maambukizi ama la. Wale wote watakaokutwa na maambukizi wawekwe kwenye uangalizi maalum pamoja na kuwapima watu wote waliokuwa na miingiliano nao.

C: Hali ya Chakula Nchini na Sukari Viwandani

Tunayo maradhi ya Corona tayari, lakini kabla ya chochote ni Lazima kwanza watu wetu wawe na uwezo wa kula chakula. Nchi yetu (Kwa maana ya Wakala wa Hifadhi ya Chakula Nchini) ina chakula cha kula kila Mtanzania kwa muda wa siku Tatu (3) tu. Sera za Serikali ya awamu ya tano za kutokutoa hela kwaajili ya kununua chakula cha akiba ndio msingi wa uwepo wa akiba ndogo kiasi hicho. Tayari kabla ya uwepo wa Corona athari za uwepo wa akiba ndogo ya chakula kwenye ghala la Taifa zilishaanza kuonekana kwa mfumuko wa bei mkubwa utokanao na kupanda kwa bei ya bidhaa za chakula nchini. Uwepo wa Corona unafanya hali iwe mbaya zaidi, tayari kuna taharuki ya ununuzi wa dharura, jambo ambalo limepandisha bei ya bidhaa nchini.

Pia, Nchi yetu ina nakisi ya uzalishaji wa bidhaa mbili muhimu sana, mafuta ya kula na sukari (Ile ya matumizi majumbani pamoja na ile ya viwandani). Uzalishaji wetu wa ndani hautoshelezi mahitaji ya bidhaa mbili hizo, na hivyo tunatumia wastani wa shilingi bilioni 800 kununua kutoka nje ya nchi. Ni dhahiri kuwa mnyonyoro wa ununuzi na usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nje utakuwa umetibuliwa, hasa kwa kuwa tunatoa bidhaa hizo kutoka Asia na Amerika ya Kusini, mahali ambako athari za Corona ni kubwa kuliko huku barani Afrika.

Tunashauri yafuatayo:

1. Serikali inunue chakula cha dharura cha kuhimili zaidi ya mwezi mmoja kutoka kipindi cha siku tatu cha sasa, na chakula husika kihifadhiwe na kugaiwa bure ama kwa bei nafuu mno pale athari za janga la Corona zitakapodhizi na kuathiri hali ya chakula nchini.

2. Serikali ina wajibu wa kueleza hatua inazochukua kuhakikisha hakuna uhaba wa bidhaa za Mafuta ya Kula na Sukari (ya matumizi ya kawaida na ile ya Viwandani).

3. Serikali ifanye haraka kurudisha fedha za wamiliki wa Viwanda zitokanazo na VAT Returns za Uagizaji wa Sukari viwandani. Fedha hizo ni nyingi (karibu shilingi trilioni moja), na ni malimbikizo ya zaidi ya miaka minne sasa, wenye viwanda wanazihitaji sasa kuliko wakati mwengine wowote.

4. Bunge la Bajeti lijadili tathmini ya hali ya chakula na uzalishaji wa bidhaa za chakula nchini, lipitishe fedha za dharura za ununuzi wa chakula cha akiba, pamoja na kupitisha unafuu wa kikodi kwa waagizaji wa chakula na bidhaa kutoka nje katika kipindi hiki cha dharura.

C: Uwezo wa Sekta Yetu ya Afya (Kibajeti na Rasilimali Watu)

D: Athari za Corona Kwenye Sekta ya Utalii

Tunajua mapendekezo ya kuzuia watu kutoka nchi zenye maambukizi makubwa ya virusi vya Corona nchini yataleta mtikisiko kwenye sekta ya utalii nchini, hivyo kwa upekee tuna mapendekezo kadhaa ya kujaribu kupunguza makali ya kiuchumi yatokanayo na hatua hizo za kuzuia watu kuingia nchini.

Uchumi wa Tanzania unategemea kwa kiasi kikubwa sana ufanisi wa Sekta ya Utalii nchini, 25% ya mapato yetu ya fedha za kigeni yanatokana na sekta hii, wastani wa Dola za Marekani 2.5 bilioni kwa mwaka, na kwa sababu ya upana wake sekta hii ina ajira zaidi rasmi na zisizo rasmi kwa wananchi wetu, kuanzia wafanyakazi wa mahoteli, wauza bidhaa kwenye mahoteli, wapishi, watembeza watalii, madereva nk. Ni mnyororo mpana wa shughuli za kiuchumi ambao utaathirika sana kutokana na maambikizi haya ya virusi vya Corona.

ACT Wazalendo tunaishauri Serikali kufanya yafuatayo:

Kjhggg 1. Serikali ikutane na Wafanyabiashara wote kwenye sekta ya Utalii, pamoja na Vyama vya Wafanyakazi kwenye sekta husika. Lengo liwe ni kupata tathmini ya Pamoja ya madhara ya mlipuko huu kwa sekta ya Utalii na huduma zake.

2. Serikali itengeneze mpango maalum wa kuhakikisha ajira za wafanyakazi katika sekta ya Utalii hazipotei, kwa aidha kutoa Unafuu|Msamaha wa Kodi zote ama kwa kuwafidia (stimulus package) wafanyabiashara gharama wanazoingia kwa kuwalipa mishahara wafanyakazi katika kipindi ambacho hawatakuwa na biashara. Lengo ni kuzifanya biashara husika zisife.

3. Serikali kuja na mpango maalum wa kuhakikisha mabenki yenye mikopo ya wafanyabiashara na wafanyakazi wa sekta ya utalii yanatoa kipindi maalum cha msamaha wa kulipa mikopo hiyo kati ya miezi sita na mwaka mmoja. Lengo likiwa ni kupunguza mikopo chechefu (NPL) pamoja na kuzuia kupotea kwa mali za wafanyabiashara na wafanyakazi walio kwenye sekta ya Utalii.

D: Hitimisho

Kwa wakati husika bado athari za Maambukizi ya virusi vya Corona hayajagusa kiundani sekta ya afya, na hivyo ni vigumu kujua athari na mapungufu yetu ya kimaandalizi. Ni matarajio yetu kuwa Serikali italeta bungeni mpango Kazi wa kuonyesha utayari wetu wa kupambana na janga hili, pamoja na Bajeti ya dharura ya utekelezaji wa mpango Kazi husika.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo
Dar Es Salaam
Machi 20, 2020
 
Vipi kuhusu mikusanyiko ya watu na mikutano ya kisiasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi?
 
Ndugu zito hongera kwa tamko lenye ushauri..

1.Naona umekomakia suala la utalii as if ugonjwa umeerupt nchini tu,Tanzania soko la utalii Nchini halitegemei watali wa ndani kwa asilimia kubwa jambo ambalo unalifahamu,hivyo kwa kuwa wateja wa utalii ni watu kutoka nje na ugonjwa huu umeikumba sehemu kubwa ya dunia kwa maana ya nchi mbalimbali na nchi nyingi zimeweka mazuio ya kutoka au kuingia nchini mwao ili wasiweze kusambaza zaidi virusi hivyo.

Ninachotaka kusema ni kwamba hatakama serikali itakutana na wadau wa utalii bado wadau hawatakubali kuwalipa wafanyakazi wakati workdone ni zero,income zero and everything ni zero hivo hakuna yeyote ambaye anaweza lipa mshahara wakati income hakuna hata wewe huwezi.

Hivo kuitisha mkutano na wadau ni kupoteza muda ambapo ungeweza kushauri angalau serikali ijikite zaidi kuhamasisha watu wajikinge na ungewapa changamoto serikali iongeze pesa za tafiti vile vile ungewashhauri watanzania wasikae sehemu moja katika mikusanyiko isiyo ya lazima badala yake watembele maeneo ya hifadhi mbalimbali ili hao unaotaka walipwe waendelee kulipwa vilevile wananchi wanakuwa wamejiweka karantini na kuwaongezea hamasa ya kutembelea maeneo ya kitalii.

2.Serikali itawafidia wangapi hiyo stimuli package kwa kuwa wanao athirika sio sekta ya utalii pekee,sie wa sekta ya usafirishaji pia tunaathirika kama hufahamu hilo,hivyo sekta nyingi tu itabidi zifidiwe as if serikali imeleta corona la utadhani serikali imependa hili janga litokee au kana kwamba serikali inafurahia kutokea hii issue.

Inaonekana wewe binafsi umefurahi ili ufanye cheap politics zako.

3.Eti unataka kipindi maalum cha msamaha about how long? unajua corona itadhibitiwa lini? thinking za kipuuzi hizo mkuu maanake ikiendelea kwa miezi,miaka serikali itajiendesha vipi hata hiyo stimulus package itatoka wapi au hujui serikali inategemea kodi iliifanye yote hayo unayoyataka kwenye mabenki serikali inakusanya kodi ili ije itoe hiyo stimulii package.

Everything mnafanya siasa tena cheap politics za kutaka kuonekana mnafaa wakati hicho kitu hakiwezekani kwa nchi zetu za third world,hebu tujikite kwenye kushauri mambo yanayoendana na dharula.

Watu ni muhimu sana kuliko hayo,hata yakifa hayo unayosema ya utalii kwa kutegemea watu tutasimama tena kwani ndio rasilimali muhimu kuliko zote dunia kinyume watu wengi wakifarikili hivyo vyote ni useless.

Lets talk about majority not minority sio unakomalia wenye nacho tu.
CHEAP POLITICS HIZO

Joselela.
 
Walioathirika sio sekta ya utalii tu, kuna wafanyabiashara wengi wananunua bidhaa China nao wameathirika sana, wanaosafirisha mazao nje, wafanyabiashara wa sekta ya madini hakuna wanunuzi, karibia sekta zote zimeathirika
 
Siku nyingine lete full article sio nusu nusu kama ulivyofanya tunaweza kukubebesha lawama usizo sitahili,
you are a leader act smart,work smart.
 
Asante, tamko zuri, nadhani kati ya vyama 21 Tanzania vyenye usajili wa kudumu, ni ACT Pekee ndio wametoa tamko rasmi kama tamko la Corona.
Hii ni dalili nzuri ya chama kinachojiandaa kushika dola.
P
 
Asante, tamko zuri, nadhani kati ya vyama 21 Tanzania vyenye usajili wa kudumu, ni ACT Pekee ndio wametoa tamko rasmi kama tamko la Corona.
Hii ni dalili nzuri ya chama kinachojiandaa kushika dola.
P
IMG-20200320-WA0001.jpg
 
Siku nyingine lete full article sio nusu nusu kama ulivyofanya tunaweza kukubebesha lawama usizo sitahili,
you are a leader act smart,work smart.

Acha kutoa matisho ya kishamba, yeye ametoa ushauri naona unamshambulia na kutaka atoe maoni yake kwa utashi wako. Ni vyema ukajikita kutoa ushauri wako badala ya kujifanya una hoja kumbe vitisho vya kipuuzi tu. Zito hatoi maoni ili kukufurahisha, bali anatoa maoni yake kutokana na mtazamo wake. Kama umezoea kumtisha mkeo ni huko huko nyumbani sio hapa jukwaani.
 
Acha kutoa matisho ya kishamba, yeye ametoa ushauri naona unamshambulia na kutaka atoe maoni yake kwa utashi wako. Ni vyema ukajikita kutoa ushauri wako badala ya kujifanya una hoja kumbe vitisho vya kipuuzi tu. Zito hatoi maoni ili kukufurahisha, bali anatoa maoni yake kutokana na mtazamo wake. Kama umezoea kumtisha mkeo ni huko huko nyumbani sio hapa jukwaani.
endelea kukurupuka ukikua utaacha,ni wap nimemtisha,mimi sina akili za type ya kina lema au wewe.
 
endelea kukurupuka ukikua utaacha,ni wap nimemtisha,mimi sina akili za type ya kina lema au wewe.

Peleka upuuzi mbali, heshimu mawazo ya mwingine, mambo ya kuanza kusema sijui anafanya siasa ni hoja za kipuuzi. Hata kama anafanya siasa ulitakaje kwa mfano? Ngiri jike ww. Toa maoni yako na sio kumshambulia mtu. Huwezi kuchangia hoja kaa kushoto.
 
Peleka upuuzi mbali, heshimu mawazo ya mwingine, mambo ya kuanza kusema sijui anafanya siasa ni hoja za kipuuzi. Hata kama anafanya siasa ulitakaje kwa mfano? Ngiri jike ww. Toa maoni yako na sio kumshambulia mtu. Huwezi kuchangia hoja kaa kushoto.
Duh... Hivi hii ni nini? Msongo wa mawazo ama nini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwami nyiribambe
Zitto samahani naona wafuasi wako wananishambulia.
 
Back
Top Bottom