Tamko la ACT Wazalendo kuhusu mlipuko wa Corona

Mbona hajatoa bei elekezi ya sanitaiza huku mitaani tunalanguliwa.
 
Ni kweli sekta nyingi zitaathirika lakini kupanga ni kuchagua lazima tuchague sekta moja ambayo ni muhimu zaidi kiuchumi, Tuilinde hiyo sekta naungana na Zitto sekta ya kuilinda kwa udi na uvumba ni sekta ya Utalii, hii ndo ina mchango mkubwa zaidi kwa pato la Taifa (about 25%)

Ingependeza kufidia sekta zote lakini uwezo wa serikali ni mdogo kwa hiyo inabidi ifidiwe sekta ambayo kama ikifa basi tutaathirika zaidi.

wanaotaka na sekta nyingine zifidiwe nao wajenge hoja waonyeshe umuhimu wa sekta hizo kufidiwa ili kwa resources hizi ndogo tulizonazo serikali iweze kuprioritize. Wasidismiss hoja nzuri ya ACT iliyowasilishwa Zitto eti kwa kuwa hawakusemea sekta zote.
 
Jinga wewe usinione fala kuandika hivo na sijamaanisha hivo...
jiheshimu usi abudu maandishi.

Uwe fala usiwe fala hilo utajua ww, lakini nina hakika wakati mwingine utaheshimu maoni ya wengine na hutathubutu kuleta vitisho vya kipuuzi.
 
Nani anaogopesha watu kuhusu Corona?? kwanini?

Someni screenshot hizo mafuta ya ndege, mafua ya nguruwe, ebola na vingine vilikuwepo,, kwanini Corona ndo ipewe big head??
Who is behind??

Sent using Jamii Forums mobile app
 

1.Zitto ameonesha umuhimu sekta ya utalii
2.Ni jukumu LA Serikali kulinda uchumi wa nchi kama haina iseme tu siyo kusema Serikali haikuleta hili janga.
3.Shule na vyou vimefungwa nchi mzima kwa siku 30,je baada ya hizo siku corona itakuwa imeisha.
4.Kazi ya mwanasiasa ni kupiga siasa kwa mtindo unaopenda bila ya kuvunja sheria za nchi,na wewe Fanya siasa za maana basi hizo za kusema Serikali haikuleta majanga.
 
Ndugu zito hongera kwa tamko lenye ushauri..

Lets talk about majority not minority sio unakomalia wenye nacho tu.
CHEAP POLITICS HIZO

Joselela.
Mkuu naomba nikinzane na ww kidogo

1. Kaongelea sekta ya utalii sababu ndio foreign-based sector kuliko zingine, yaani fedha za kigeni nyingi tunategemea kupitia Utalii hivyo italii ukiyumna foreign currency reserve pale BOT itatetereka.

2. Anaposema mishajara ilipwe hata kama income ni sifuri, pesa hazitoki kwa wafanyabiashara pekee bali support ya serikali kupitia hyo stimulus package.

3. Stimulus package sio lazima ipelekwe kwa wote ila serikali inaangalia vipaumbele, kilimo,madini, ujenzi shughuli zinaweza endelea ila utalii umekwama sababu watu hawasafiri kabisa kutokana na obvious reasons hivyo sekta hii itatatetereka zaidi kuliko zingine at least directly.

4. Issue hapa sio serikali kuwa na pesa au lah ila ndio kazi ya reserves pale BOT ambazo ni zaidi ya dollar billion 4. Ni wakati wa crisis kma hizi ndio zinatuma na sio eti pesa za kodi ndio zinategemewa serikali kuendesha nchi.

5. Reserve ya BOT inaweza kusustain uchumi wa nchi kwa miezi mitano kama sikosei so by then lazima corona itakua tu imepata suluhu au angalau sekta zimesimama even thou kodi haikukusanywa kabisa.

6. Issue ya kutoa stimulus package ni Multiplier effect mfano anayeachishwa kazi hatoweza mlipa housegirl, hatowezi nunua king'amuzi, hatomlipia mtoto ada n.k hivyo shule na biashara tajwa zitakosa mauzo na zitaporomoka hivyo ajira moja sio minority kama unavyosema bali inaweza poromosha uchumi kwa sehemu yake kwa chain of events zinzoitwa spillover effects.

7. Anyway huu ni ushauri tu hakukuwa na haja ya kuita cheap politics, kwenye negotiation huwa unakuja na demands za kufikirika ili mnapozidi jadiliana mnapunguza hadi mnabaki kwenye more realistic clauses na mnapata muafaka so hii sio fallback position mpaka umshambulie hivi eti Afrika haiwezekani!! Mbona elimu bure pesa zimetolewa unadhani nchi developed zote zina elimu bure??

8. Stimulus package ni kuchochea uchumi maana serikali ikiacha makampuni yakifa uchumi utaproomoka sasa kodi watatoa wapi?? Ila stimulus itarudi tu maana income tax inakatwama/payee kuna corporate tax then matumizi yao tu watu binafsi yanakatwa kodi so unakuta mpaka 50% ya pesa waliotoa itarudi tu TRA.

Nakushauri ukasome Topic ya Money and banking kuanzia Money supply, monetary policy, Multiplier effect n.k ndio urudi kumchallenge

Natanguliza shukrani
 
Kwa hiyo kama serikali haina uwezo wa kuwafidia watu kwa kuwa idadi yao ni kubwa,vipi kama ikitokea hali imekua mbaya kama ya China au Italy,je serikali iache kila mtu abaki na hamsini zake ?
 
hakuelewa,kila kitu kwa sababu tu kasema mpinzani basi anataka kukipinga.
 
Mimi nakuunga mkono, pia naongeza msisitizo sekta ya usafiri wa anga pia ifiriwe kwenye hiyo stimulus package.
 
Ushauri mzuri sana, lakini bahati mbaya hakuna atakayekusikia under this Satanic regime!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi Mgonjwa wa Corona karipotiwa mmoja, mkaja na mbinu ya kufunga shule zote na vyuo, kuzuia mikusanyiko isiyo ya lazima, tunawe na mikono tukasema sawa..

Walipofika wagojwa 3 mkasema tuendelee kunawa mikono.

Wakafika 12 bado tunawe mikono
Wakafika 23 tunawe mikono
Wakafika 49 tunawe mikono
Wakafika 53 tunawe mikono
Wamefika 88 tunawe mikono

Hivi hamuoni maambukizi yanazidi, nyie mbinu yenu ni hiyo tu ya kunawa mikono.

Hivi hakuna mbinu nyingine?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hata nao hawajui wafanye nini..

wanategemea msaada pekee "kutoka juu angani"
 
Swali zuri, ninaamini the ana akili na strategy, maana tuliwachagua, ngoja watakujibu, And wakijibu please tag me
 
Kaa nyumbani kwako wewe na familia yako, jiepushe na mikusanyiko.
Mwisho kabisa nawa mikono.

Usitegemee serikali ikusemee kila kitu kinachohusiana na maisha yako. Tumia kariongo yako zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…