Tamko la Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

Tamko la Jukwaa la Walimu na Wanafunzi-Tanzania.

Civilian Coin

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2012
Posts
2,305
Reaction score
4,380

MAPROFESA na MADOKTA(PhD) WA TANZANIA NDIO CHANZO CHA UBOVU WA ELIMU YA TANZANIA.

Kutokana na wanasiasa na wadau mbalimbali wa elimu kumsakama Waziri Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii inatokana na Viongozi wetu wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile wanachokisema. Tanzania tuna Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena wengine wa siku nyingi lakini hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu ya Tanzania zaidi wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya kutoa ufumbuzi wa namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.

Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni malumbano yasiyokuwa na tija. Hata tume inayotazamiwa kuundwa na waziri mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi kabla hata tume haijaanza kazi. Tunajua Maprofesa na Madokta(PhD) wanauwezo mzuri wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu hata kutunga Vitabu vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao cha elimu lakini tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake wakati tuna wasomi wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu bali tuwe Taifa la kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.

Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya siasa. Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado serikali inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni midogo sana na haiendani kabisa na mazingira wanayoishi. Mwalimu mwenye degree analipwa takribani 500,000/= na usheee, diploma takribani 300,000/= na ushee na mwenyecheti takribani 200,000/= na ushee unategemea nini hapo?

Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli mtu una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf , ukatwe CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame .

Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara ya walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na wanaishi maisha ya kifahari kuliko sisi walimu. Tulitegemea wabunge wange wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili wafanye kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Mwalimu hata angejituma vipi kama mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana lazima awaze kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana hata motisha.

Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.

Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015
 
pole sana mwalimu, mi nadhani hilo la mshahara na marupurupu ndio la kulilia zaidi, khs wasomi wetu kutotafuta njia bora ya kuishauri sirikali hilo ni gumu kidogo kwani sio mara moja wadau mbalimbali hasa haki elimu wameshakuja na mawazo kadhaa ya kuboresha elimu yetu lkn serikali yetu sikivu imeziba masikio, khs mitaala hiyo ndio usiseme maana mbatia nusu atolewe meno bungeni kwa kudai serikali haina mitaala, khs 3500 hm ni ndogo sana mwl jaribu kuongeza ongeza.
 
Nauli ya sh 800 kwa siku unapanda baiskeli?

Si kama anapanda baiskeli,jamaa kajaribu kufanya makadirio ya chini tu ili walau waone minimum expenditure mbali na ile max angeitaja,suppose mwl anatoka g/mboto-tandika nauli 400 kwenda na 400 kurudi, ila kwny chakula lazma kajiunderestimate maana chps kav tu na ugali dagaa ndo 1200 na c rahs kula hvyo kila cku,bdo mtoto huwez sema ni m1,average fanya wa3 bado hujadaiwa mchango wa mlinzi shule ya mtoto,uji na michango ya mitihani ya jumamosi..kiukweli hali ni ngumu,serikali yetu haina utu kwa walimu.Chama chenu CWT chenyewe hakiwathamini,jengo lile la Mwalimu pale Ilala mkachanga wee mwisho wa cku hamuambulii chochote..viongoz wenu wakiitwa chemba kidogo wanawasahau,la-haullah! Mungu awasaidie sana.
 
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?

Inategemea upo wapi.

2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=

Unaishi na mwanao chumba kimoja?

3.Chai asubuhi 800/=

We mchumi,tushee umaskini

4.chakula mchana 1200/=

Ugali dagaa kwa mama lishe napo lazima umpige sound

5.kodi ya umeme 10,000/=

Varies

6.maji ya kununua ya madumu 300/=

Ni zaidi ya hapo mkuu labda kama we ni msela

7.Nyumbani uache 3500/=

Kama una watoto inabidi ukapime DNA huenda mmoja akawa wa muuza genge mwingine wa mtu wa buchani

8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=

True
 
tUNAOMBA HILO JUKWAA LA WALIMU LIWE NDIO CWT MPYA NA MULIWEKEE MKAZO ILI HAKI ZA WALIMU ZIONEKANE
 
Hiyo pesa ya kuilipa tume ingesaidia kununua vitabu. Tatizo kubwa la waalimu wamezidi upole, chukueni hatua
 
MAPROFESA na MADOKTA(PhD) WA TANZANIA NDIO CHANZO CHA UBOVU WA ELIMU YA TANZANIA.

Kutokana na wanasiasa na wadau mbalimbali wa elimu kumsakama Waziri Kawambwa na Baraza la mtihani la Taifa hii inatokana na Viongozi wetu wa Tanzania kutokufanya tafiti ya kile wanachokisema. Tanzania tuna Maprofesa na Madokta(PhD) wengi tu tena wengine wa siku nyingi lakini hatuoni mchango wao katika kuboresha elimu ya Tanzania zaidi wanaungana na wanasiasa kuendeleza porojo badala ya kutoa ufumbuzi wa namna gani tutaiokoa elimu ya Tanzania.

Tulitegemea kuona Maprofesa na Madokta(PhD) kuibuka kwa nguvu kubwa kuitaka serikali iunde mtaala wa elimu wenye tija kwa elimu ya kitanzania na wao wakishiriki kutoa mchangoa wao badala yake ni malumbano yasiyokuwa na tija. Hata tume inayotazamiwa kuundwa na waziri mkuu tulitegemea Maprofesa wangekuwa wa kwanza kutoa ufumbuzi kabla hata tume haijaanza kazi. Tunajua Maprofesa na Madokta(PhD) wanauwezo mzuri wa kuandika mtaala wa elimu na sera nzuri ya elimu hata kutunga Vitabu vizuri vya kufundishia kutokana na kiwango chao cha elimu lakini tumewaachia Kina Nyambari watunge vitabu na watu wake wakati tuna wasomi wa ngazi ya juu kabisa, tusiwe Taifa la kulaumu bali tuwe Taifa la kujenga na kuona uchungu wa watoto wetu.

Hata kama tume ya waziri mkuu itapita bado suluhu haitapatikana kutokana na wanao jua ukweli wamekaa kimya au kuamua kufanya kazi ya siasa. Sambamba na mitaala na mfumo mbovu wa elimu wa nchi yetu bado serikali inatakiwa kujitahimini juu ya mishara ya walimu kwani ni midogo sana na haiendani kabisa na mazingira wanayoishi. Mwalimu mwenye degree analipwa takribani 500,000/= na usheee, diploma takribani 300,000/= na ushee na mwenyecheti takribani 200,000/= na ushee unategemea nini hapo?

Kimsingi mishara ni midogo sana na kila siku kodi za nyumba zinapanda vyakula vinapanda, umeme unapanda kila mara nauli za daladala, kweli mtu una weza kuishi? Huo huo mshahara ukatwe kodi ,ukatwe Nssf , ukatwe CWT, chama cha kutetea haki za wafanya kazi wachukue chao.
1.Nauli kwa siku 800 kwa siku sita ni Tsh ngapi?
2.kodi ya chumba kwa mwezi 30,000/=
3.Chai asubuhi 800/=
4.chakula mchana 1200/=
5.kodi ya umeme 10,000/=
6.maji ya kununua ya madumu 300/=
7.Nyumbani uache 3500/=
8.Mtoto apate nauli ya shule na kula kwasiku 2000/=
9.Bado matumizi ya matibabu japo hili linatokea mara chache
Tunaomba mlitazame .

Lakini hutasikia wabunge na wanasiasa wanapiga kelele kutetea mishara ya walimu ila wao kujiongezea posho wanajipigia kelele sana na wanaishi maisha ya kifahari kuliko sisi walimu. Tulitegemea wabunge wange wasilisha hoja binafsi ya kutetea mishahara ya watumishi ili wafanye kazi kwa moyo wote lakini utafikiri hawaoni, daima tunajua mwenye shibe hawezi kumkumbuka mwenye njaa. Mwalimu hata angejituma vipi kama mshahara haukidhi ni vigumu kufundisha kwa kujituma maana lazima awaze kufanya biasahara nje ya kazi ukizingatia mwalimu hana hata motisha.

Matokeo ya kidato cha nne yawe changamoto kwa serikali na si kutafuta mchawi bali mchawi mkubwa ni mshahara mdogo na walimu kuthaminiwa.

Mwl.DEOGRATIUS KISANDU
Mwenyekiti wa JUKWAA LA WALIMU NA WANAFUNZI-TANZANIA.
25/02/2015
nako FB wametoa maoni yao kama hivi;
Novatus Mutoka, Fetty Peach, Mathias Margwe and 12 others like this.

Real Musty Dulla umeongea cream tupu.....kule mjengoni wote wapo kwa maslahi yao tu......wanasahau mwalimu ndo funguo ya mafanikio na bila mwalimu wao wasingekua hapo walipo leo hii
8 hours ago via mobile · Like

Hassan Kikoti - HAPO JE MWALIMU ATAKUWA NA MOYO WAKUFUNDISHA? HILO SIO TATIZO LA KUFELI KWA WATOTO WETU,
8 hours ago · Like

Sudat Lism Elimu ikichanganywa na siasa ndo matokeo yake haya
8 hours ago via mobile · Like

Raphia Mkingule maprofesa na madoctor wamekuwa wafanya biashara badala ya kufungua shule na asasi mbalimbali za elimu wanafungua bar!!
8 hours ago via mobile · Like

Raphia Mkingule jiulize leo mjini kuna bar na guest house ngapi zq maprof!hatukatai lakini nini mchano wenu kwa jamii??hatuwalaumu lakini umefika muda sasa tujaribu kuangalia vipaumbele vya taifa hili,wapi duniani uliona elimu inapuuzwa??wapi ulona mtu muhimu kama Mwalimu anadharaulika....wala msisingizie maendeleo ya technologia yamepotosha maadili mlitegemea kuishi nyuma ya jua milele?get the l
8 hours ago via mobile · Like

Ericque Richard Mongi SALUT BROTHER, MUCH RESPECT TO YOU.
8 hours ago via mobile · Like

Luccy Joseph · Friends with Sillas Mbuya and 12 others
umeongea sana kaka.
8 hours ago via mobile · Like

Derick Mkuwa Tuko pamoja kwa hilo Mwenyekiti, JUWAWATA!
7 hours ago via mobile · Like

Gloria Semazina Pamoja saaaana. Aluta continua!!
7 hours ago via mobile · Like

Mathias Margwe Kwa kweli hii nimeipenda sana kaka D. Pio, hii sauti itasikikaaaaaaaaaaaa????? kwa vipiiiiii???
5 hours ago · Like

Fetty Peach Ifike kunakohusika isiishie fb tu
about an hour ago via mobile · Like

Mosses Benjamin Umeongea sana chukua book yaani 1000 chukua maji unywe upoze koo big up sana
55 minutes ago via mobile · Like

Novatus Mutoka exactly kaka,
32 minutes ago · Like
 
Kwakweli swala la elimu kuwa katika hali tunayoiona sasa ni jambo lisilokubalika hata kidogo.Nimesikia kuwa PM kaunda tume ngoja tuiache ifanye kazi yake kwanza lakini naomba mambo yafuatayo yazingatiwe.Kwanza kabisa Naomba serikali iongeze mishahara kwa kada ya watumishi(Walimu).Aidha hili liende sambamba na kupunguza mishahara kwa kada ya watumishi wengine wenye mishahara mikubwa,kama vile makatibu wakuu wizarani,wakurugenzi na Mawaziri.(2)Naomba pia Ongezeko la mishahara liende sambamba na Mabadiliko ya sheria ya utumishi wa Umma,kwamba ajira itolewe kwa mkataba wa miaka mitatu au mitano,na baada ya hapo mkataba ndo uwe subject renewal.Lakini huu utaratibu wa sasa mtu akishapata kazi basi mpaka miaka 60,yaani amefundisha hajafundisha,amefanyakazi hajafanya lakini mshahara huko palepale,hatuwezi kupata ufanisi hata kidogo.3.Hoja yangu ni kwamba kama Raisi na Madiwani na Madiwani,wanapewa miaka 5 badae tunapiga kura iweje Mtumishi wa Umma?Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom