Tamko la Marekani kuhusu hali ya kisiasa, uminywaji wa sheria Tanzania

Tamko la Marekani kuhusu hali ya kisiasa, uminywaji wa sheria Tanzania

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
336
Reaction score
564
U.S. Embassy Tanzania
Kuzorotoa Kwa Haki Za Kiraia Na Haki Za Binadamu Tanzania
Serikali ya Marekani imesikitishwa sana na matukio ya mashambulizi yanayoshamiri na hatua za kisheria zinazochukuliwa na serikali ya Tanzania, ambazo zinakiuka uhuru wa raia na haki za binadamu, na zinazojenga mazingira ya vurugu, vitisho na ubaguzi. Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji watu unaoendelea na unyanyasaji wa makundi maalum, wakiwemo mashoga, na wengine wanaotaka kutumia haki zao za uhuru wa kujieleza, kushiriki na kukusanyika. Vyombo vya kisheria vinatumika kudhibiti uhuru wa raia kwa wote.
Kuzorota kwa hali ya haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Tanzania kunakwamisha maendeleo, ustawi wa uchumi, amani na usalama. Tunatoa wito kwa mamlaka nchini Tanzania kuchukua hatua za makusudi kulinda haki za asasi za kiraia, watetezi wa haki za binadamu, waandishi wa habari, wafanyakazi wa afya, wanaharakati wa kisiasa na watu wote kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, mkataba wa Afrika wa haki za binadamu na watu, na makubaliano ambayo nchi imeridhia kikanda na kimataifa.
Soma https://bit.ly/2DzXkFD
#Demokrasia
#HakiZaBinadamu

Tamko 9Nov2018.jpg
 
Mbona hawajatoa mifano ya huo uminywaji wa haki za binadam.
Mimi nimeona jamaa wamekomaa zaidi na hii "Tunahuzunishwa na hatua za ukamataji watu unaoendelea na unyanyasaji wa makundi maalum, wakiwemo mashoga, na wengine wanaotaka kutumia haki zao za uhuru wa kujieleza, kushiriki na kukusanyika. Ukiachana na hiyo ya Mashoga la msingi hapo ni hayo ya Uhuru wa Kujieleza, Kushiriki na kukusanyika full stop!
 
Mbona hawajatoa mifano ya huo uminywaji wa haki za binadam.
Are you making yourself blind, Nafikiri hata Yesu alipoongea kwa mifano/mafumbo aliwaruhusu watu kutumia akili walizopewa na Mungu kufumbua yaliyofichwa mle! Hata wewe usipotaka kufikiri ni haki zipi zinaminywa una maana kwamba aje afikiri mtu kwa niaba yako?
 
Hizi ni ngonjera, Idd Amin bila Nyerere kumfurusha angeendelea kuwaua waganda mpaka wangelibaki nusu! Marekani wacha ngonjera, chukua hatua.
Nimecheka sana hii comment yako. Mkuu unataka marekani achukue hatua gani?
 
Hizi ni ngonjera, Idd Amin bila Nyerere kumfurusha angeendelea kuwaua waganda mpaka wangelibaki nusu! Marekani wacha ngonjera, chukua hatua.
Hawana hatua wanayoweza kuchukua, Israel, Palestine,Iraq , Libya, Afghanistan, Somalia, South Sudan,China, bila kusahau Rwanda, Burundi ,DRC etc kote huko wameshindwa kufanya chochote, hawana lolote hao ni wanafiki tu. Na km ndiyo unawategemea waje huku basi huna tofauti na mtu anayefuga mbwa kwa kutegemea makombo ya jirani.
 
Ni maoni yao....
Hakuna kitu kama hicho waache ngonjera,
labda kama wanataka wagawa tako wasibughudhiwe....lkn sisi tuna sheria ya bunge Sura 16 kf cha 154 ambacho kimekataza ....ufirauni....
Ngoja tuone tu.
Waanze Kwanza Siria na wakifanikisha ndio waje, anachowafanya Trump wamenyamaza hee, Kwanza hata hao haki za binadamu kaminya luzuku, wanatapatapa tuu, huyo jiwe Hana time ya kuwaabudu hao na ndio maana hata huko kwao hang'ai anajua hawana jipya, Jana jiwe kasema hao wakija kwako wanahesabu zao. Hawawezi kukujengea nchi yako. Watajifanya hivi na vile lakini wakifanikisha lengo lao wanatembea. Binafsi hata wakihaha Kama nyoka huo ujinga wa kutetea urawiti haupo. Wataongea mwishowe watanyamaza maana wataona jamaa hatikisiki. Lazima ifike wakati Jambo ambalo hamlitaki kama nchi na utamaduni wake na Sheria ya Hilo mmeitunga mseme hatutaki Tena kwa herufi kubwa bila kujali Nani. Kwani hao wanaotoa eti tamko ni watanzania hao. Hawajasoma katiba yetu kuwa ushoga haturuhusu? Kwahiyo Hilo tamko lao wanataka tupingane na tulochokiamua kabla na tukakiweka kwenye katiba?? Ndio maana jiwe Jana akasema wakati mwingine tuwe na maamuzi, woga woga hautufikishi popote, tutaishia kupangiwa pangiwa tuu na kucheleweshwa kupiga hatua. Na akasema anamkubali hata kiongozi anayeamua hata Kama akiwa wrong lakini walao anakuwa na maamuzi na sio mwoga. Sasa aliyeamua kuhusu ushoga kakosea wapi na katiba inazuia? Tusiwe bendera fuata upepo, Tusimamie nchi yetu bila kujali jirani anasema nin kwani huyo jirani hawezi kukufikisha pazuri, anaangalia masilahi yake na ukifunguka akili lazima atakuwa adui kwako. Kumbuka jiwe baada ya kuongia madarakani, ni misaada mingapi ilikatishwa kwa nchi?? Kisa wanataka tuenende na matakwa yao, je alipotangaza tenda ya ujenzi wa reli kwa fedha za ndani hawakujileta Tena wenyewe na kuomba kutukopesha fedha katika baadhi ya miradi?? Ndipo utajua hao huwa wanajaribu kutuchezea akili zetu waone Kama bado ni mambumbumbu, La ziada usitegemee kwa jirani, akiacha kukusaidia utapoteza uwelekeo, jifunze kusimama wewe pekee, Hapo ndipo akili ya JPM ilipo,
 
Hawana hatua wanayoweza kuchukua, Israel, Palestine,Iraq , Libya, Afghanistan, Somalia, South Sudan,China, bila kusahau Rwanda, Burundi ,DRC etc kote huko wameshindwa kufanya chochote, hawana lolote hao ni wanafiki tu. Na km ndiyo unawategemea waje huku basi huna tofauti na mtu anayefuga mbwa kwa kutegemea makombo ya jirani.
Muulize maa yako kama makombo ya jirani hayasaidii
 
Kinachoumiza zaidi Tvs local channels, taarifa za habari na bunge live....
 
Nyumba inafuka moshi, walioko nje wanaona kuwa hali ya watu waliomo ndani ya hiyo nyumba ni mbaya. Lakini cha kushangaza waliomo ndani ya hiyo nyumba ndo wanatetea kuwa hali ni swali. Below 70 Iq ni vichaa!
Naendelea kuthibitisha kuwa ni kweli watanzania wengi ni below 70 IQ
 
Back
Top Bottom