Je Pinda alisema nini katika kuomba msamaha? Wakati mwingine Kuhani anakuwaga na point yaani hata kusikiliza hotuba yenyewe inakuwa ngumu? Sikiliza alichosema Pinda uamue mwenye kati ya hizo version tano ni NINI HASA pinda alisema
Mwanakijiji,
Naona, for once, ume-appreciate baadhi ya ninavyovisema kuhusu press ya Tanzania. Ahsante.
Katika hotuba ya Pinda, kwa hisani ya media outlet yako, na kwa hapa ahsante tena, kuna makorokosho mengine ya kizushi kutoka press yenu. Classic example:
PINDA: Kiliniumiza sana mimi nilipoona Bunge la Jumuiya ya Ulaya eti ndio linatoa azimio kujaribu kulaani mauaji ya albino. Sikulipenda sana. Ingawa tulisema wamefanya jambo jema. Sikulipenda tu kwa sababu walionekana kana kwamba wao wanaelewa vizuri zaidi juu ya tatizo hili kuliko sisi wenyewe Watanzania.
MWANANCHI: Alielezea pia kuhuzunishwa zaidi na tamko la Bunge la Jumuiya ya Ulaya (EU) la kulaani mauaji hayo, kana kwamba wao wanaguswa sana na suala hilo kuliko Serikali ya Tanzania.
Tafsiri ya gazeti ukiisoma utadhani Pinda kasema wa-Ulaya wanajifanya wanaumizwa kuliko sisi na wamemhuzunisha. Kumbe kasema walichofanya European Union ni sawa, ila hapendi hii state of affairs inayooneka kana kwamba wao wanayajua haya kuliko sisi. Tatizo ni sisi! Sasa jamani mtu kweli unashindwa kutafsiri kisentesi kimoja cha Pinda hapo kweli? How kilaza can you be yani? How mtupu ?
Lakini na wewe Mwanakijiji kabla hujakosoa huo msamaha wa Pinda wa "kama nimekosea," inabidi uanze kwa kusema kwamba taarifa uliyoileta hapa kwamba kuna unconditional apology on the way inapotosha, vinginevyo usingerudi kwenye ile original sham apology.
Ile taarifa uliyoweka hapa imechota watu kibao, Pinda heko, Pinda ka-apologize, Pinda hivi na vile, halafu sasa unarudi kwenye original qualified apology ya "kama nimekosea." Na wewe unachangia confusion ama upotoshaji wa putrid news outlets za Tanzania.