Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 778
- 1,592
Wakili Mwabukusi ambaye pia ni Rais wa TLS (Chama cha Wanasheria Tanganyika), akizungumza na Wakili TV leo, amesema TLS inachukulia suala la polisi kuzunguka katika ofisi zao kwa uzito mkubwa sana. Amesisitiza pia kuwa TLS si wahalifu bali ni chombo cha kisheria kinachotekeleza majukumu yake kwa mujibu wa sheria, na yeyote anayehisi TLS inakosea anayo haki na wajibu kisheria ya kuwasilisha hoja zake ili hatua stahiki zichukuliwe. Kwa lugha nyingine, TLS inatetea haki yake ya msingi ya kusikilizwa kabla ya kuchukuliwa hatua zozote.
Kauli hiyo ya Rais wa TLS imetolewa ikiwa ni muendelezo wa miongozo ambayo chama hicho tayari kimekwisha kutoa kwa wanachama wake, ikiwemo kuwataka mawakili wote nchini kusitisha huduma za msaada wa kisheria (Legal Aid) . Vilevile TLS katika tamko lake la 18/09/2025, TLS ilisisitiza kaamba kwamba iwapo matakwa yake hayatatekelezwa, chama hicho kitapanga maandamano ya amani ya kitaifa yatakayoshirikisha mawakili wote Tanzania nzima kwa lengo la kushinikiza utekelezaji wa matakwa hayo.
Pia, Mwabukusi ameeleza kuwa jeshi la polisi linafanya vitendo vinavyochochea vurugu, kwa sababu wanazozijua wenyewe. Ameeleza zaidi kuwa vitendo vinavyofanywa na polisi dhidi ya TLS ni shambulio moja kwa moja dhidi ya uwakili na huduma za uwakili, pia ni shambulio dhidi ya uhuru wa mahakama na utawala bora, na hatimaye ni shambulio dhidi ya haki za wananchi. Hata hivyo, japo matendo haya yanayofanywa dhidi ya TLS ni ya kuudhi, TLS yenyewe imesisitiza kutumia hekima katika kukabiliana nayo. Tayari TLS imeanza kuyashughulikia suala hili kwa njia ya mazungumzo, lakini ni tamko wazi la TLS kwamba hawatishwi, hawaogopi, wala hawababaishwi na vitisho vya jeshi la polisi. Hivyo, Kutumia njia ya mazungumzo si udhaifu bali ni ishara ya hekima na usimamizi makini.
Hali ilivyo sasa, kwa picha rahisi, inaonyesha kwamba hatua za polisi kuzingira ofisi za TLS Makao Makuu Dar es Salaam, pamoja na ofisi za TLS Mbeya na Kagera, ni kama jitihada za kuzuia maandamano hayo ya amani yaliyotangazwa. Hata hivyo, Rais Mwabukusi amewataka mawakili kote nchini wasikubaki kuchokozeka au kuingia kwenye mtego wa vitendo vya kichokozi vinavyofanywa na jeshi la polisi, na waendelee kusimama imara kwa mujibu wa mwongozo wa TLS.