Tangu Jumatatu ya wiki hii, gumzo kubwa mitandaoni ni kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kuwataka wamiliki wa mabasi ya abiria yanayotoka Dar kwenda mikoani kuanzia safari zao Stendi Kuu ya Magufuli iliyopo Mbezi Louis wilayani Ubungo.
Lakini pia, mabasi hayo yanapotoka mikoani kuingia Dar, breki yao iwe ndani ya Stendi hiyo inayofanya kazi kwa saa ishirini na nne huku akiwataka kuachana na matumizi ya stendi binafsi.
Baada ya tamko hilo, wadau wa usafiri na wananchi mbalimbali wametoa maoni yao huku wengi wakitaka serikali kutumia 'jicho la tatu' kwa kuangalia tabu zinazowakuta wananchi kwa kulazimishaa mabasi hayo kubaki Stendi Kuu ya Magufuli.
Wananchi waliyo wengi waishio pembezoni mwa jiji la Dar wameliona tamko hilo la Chalamila kama kuwakandamiza abiria kwa namna moja au nyingine.
Wengi wamesema kuwa, miundo mbinu ya kuifikia stendi hiyo kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa jiji hilo ambao ni maelfu ni mibaya sana kuliko wanaokwenda Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere uliyopo Kipawa.
Sasa, kikubwa ambacho kimeongezeka ili kukazia maoni ya wananchi, baadhi ya watu wamezama mitandaoni na kuibua video inayomwonesha mmiliki wa mabasi ya Shabiby Line, Ahmed Makhbut Shabiby akiongelea ishu hiyo.
Baada ya video hiyo ya mjengeo kubandikwa mtandaoni, wananchi wengi wametoa maoni yao wakijua mfanyabiashara huyo ambaye pia ni Mbunge wa Gairo (kupitia CCM) ameyasema maeneo hayo siku mbili hizi akijibu tamko la Chalamila.
Hata hivyo, mmoja wa watu wa karibu na mfanyabiashara huyo amesema mheshimiwa hajatoa tamko lolote kwa sasa na kwamba video mjengeo inayosambaa mitandaoni ni ya miaka minne hadi mitano nyuma.
"Ni kweli hiyo video ni mheshimiwa Shabiby anaongea kuhusu mabasi kuishia Stendi ya Magufuli. Lakini hiyo video mbona ni ya kitambo sana. Nadhani miaka minne au mitano iliyopita. Kwa hili tamko la safari hii alilolitoa Chalamila, mheshimiwa hajatoa neno lolote," alisema mshirika huyo.
Akaongeza: "Kama wewe ni mtaalam wa kuangalia video, utajua ile ni ya miaka ya nyuma sana."
Katika video hiyo, Shabiby alitolea mfano wa tabu iliyopo kwa abiria anayeishia Stendi ya Magufuli wakati makazi yake ni Toangoma. Alisema wapo abiria wanaotumia nauli ya Dodoma-Dar sawa na nauli ya kutoka Stendi ya Magufuli kwenda Pugu.
Wakati huohuo, baadhi ya wadau waliyobahatika kusafiri nje ya Tanzania walisema zipo nchi nyingi Afrika stendi kuu za mabasi zipo katikati ya miji yao mikubwa.
Soma Pia: Wamiliki wa mabasi wapewa wiki moja kurejea stendi ya Magufuli
Mzee Kibwana Shekimweri mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, alisema: "Serikali ijipange sasa. Ijenge stendi kuu tatu. Mbagala moja na Kigamboni moja. Na hii ya Magufuli zitakuwa tatu. Hapo tabu ya abiria itapungua.
"Mimi nimetambea baadhi ya nchi hapa barani Afrika. Wenzetu wao katikati ya miji mikubwa ndiyo kuna stendi za mabasi. Sisi tunazikimbiza nje ya jiji. Serikali inaogopa nini kwani?" Alihoji Shekimweri.