Tamko la Tume ya Haki za Binadamu (THBUB) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee Juni 15, 2025

Joined
Sep 17, 2024
Posts
27
Reaction score
28
THBUB inaungama na Wadau wote katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani.

Tamko la Tume Haki Binadamu (THBUB) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili Dhidi ya
Wazee Juni 15, 2025


Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) inaungana na wadau wote katika kuadhimisha Siku ya Wazee Duniani. Kauli mbiu ya maadhimisho mwaka huu ni "Wazee ni Hazina kwa Taifa, Tuwalinde, Tuwatunze." ambayo inaikumbusha jamii umuhimu wa kuwaenzi, kuwasikiliza wazee sambamba na kuacha vitendo vya ukatili, manyanyaso na udhalilishaji dhidi ya wazee.

THBUB inatambua jitihada na mchango wa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha maisha ya wazee hapa nchini.

Jitihada hizo ni pamoja na kuwapatia wazee huduma jumuishi na stahiki kwa ajili ya ustawi na maendeleo yao, kuongezeka kwa kiwango cha chini cha pensheni, utoaji wa huduma za afya kwa wazee, ujenzi wa makazi ya wazee katika maeneo 13 nchini, kuunganishwa kwa wazee katika mfuko wa TASAF, kuorodheshwa katika makundi maalum ya namna ya kupata zabuni za Serikali na hivi karibuni Serikali imeanzisha vikundi 395 vya uzalishaji Mali vya wazee kwa wazee 10,926.

Aidha, THBUB inatambua jitihada na mchango wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuweka utaratibu wa kuwapatia pensheni na vitambulisho vya kupatiwa huduma mbalimbali wazee wenye umri wa kuanzia miaka 70 na kutunga Sheria ya Masuala ya Wazee Na. 2 ya mwaka 2000;

Pamoja na jitihada hizo, bado wazee wanakabiliwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo kutokuwepo kwa sheria mahsusi ya wazee, upatikanaji wa madawa na vifaa tiba kwa wazee. Kupitia siku hii, THBUB inapendekeza yafuatayo:

i. Serikali iharakishe mchakato wa kutunga sheria maalum ya wazee ili kulinda haki za wazee kisheria;
ii. Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuendelea kuhudumia wastaafu;
iii. Serikali kuongeza jitihada kutatua changamoto za upatikanaji wa dawa katika hospitali na zahanati ili wazee wafaidi huduma hizo kama ilivyokusudiwa;
iv. Kuanzisha Dawati la kuratibu huduma za afya kwa wazee katika ngazi ya halmashauri;
V. Serikali ishirikiane na wadau mbalimbali kutoa elimu kwa jamii kuachana na ukatili dhidi ya wazee; na
Serikali na wananchi wote kwa ujumla kulinda na kutetea haki za wazee ikiwemo kuthamini mchango, uzoefu na ushiriki wao kwa maendeleo ya taifa.

Tume inatoa wito kwa wananchi wote kwa pamoja tutekeleze wajibu wetu kwa wazee kwa kuhakikisha tunawalea, tunawaheshimu, tunawapatia ulinzi, usalama, chakula, mavazi na malazi.

​
 
Hongereni wazee....kwani jamii bila wazee hukusa busara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…