1. UTG inatilia shaka ukweli wa taarifa ya mawasiliano ya mwisho ya Ben. Mawasiliano yaliyowasilishwa jeshi la polisi kitengo cha uhalifu wa kimtandao (Cyber crime) ambayo tumeweza kuyaona, yanaonesha kuwa Ben aliwasiliana mara ya mwisho kupitia simu yake mnamo 16/11/2016 saa 2:01 asubuhi.
Lkn Ben aliondoka nyumbani kwake tar 18/11/2016. Hii inamaanisha Ben hakuwasiliana kbs tar 17 na 18 jambo ambalo UTG tunaamini si kweli. Kama Ben aliondoka nyumbani kwake 18/11/2016 iweje mawasiliano yake ya mwisho yawe 16/11/2016? UTG tunaamini mawasiliano ya Ben ya siku mbili za mwisho (tar 17 na 18) yamefichwa kwa sababu maalumu.
2. Katika mawasiliano yanayoishia tar 16/11/2016, zipo namba ambazo tunazitilia mashaka, ambazo si za ndugu, marafiki wake wala jamaa wa Ben. Namba hizo zinaonesha kuwasiliana na Ben siku za mwishomwisho kabla ya kupotea na hazijawahi kuwasiliana nae kbs ktk kipindi cha awali.
UTG kwa kushirikiana na familia ya Ben, tumelitaka Jeshi la Polisi kufuatilia namba hizo ili kuwabaini wahusika na wahojiwe juu ya mawasiliano yao na Ben. Lkn hadi sasa hatujapata taarifa rasmi kutoka polisi kuhusu kukamatwa kwa watu hao.
3. Tangu Ben amepotea hadi sasa tumefanya mawasiliano na jeshi la polisi mara 21. Mara zote hizo Polisi wamekua wakituambia kuwa wanaendelea na uchunguzi. Lkn hawajapata kusema wamefikia wapi katika uchunguzi wao huo.
Tunaheshimu utaratibu wa jeshi la polisi kufanya uchunguzi lakini tunaomba watujulishe hatua waliyofikia. Majibu ya mkato kwamba wanaendelea na uchunguzi hayaridhishi hasa kutokana na suala hili kugubikwa na sintofahamu kubwa.
4. Mkuu wa Jeshi la polisi nchini Ernest Mangu akihojiwa na gazeti la RaiaMwema la wiki hii alisema Ben anatafutwa kama "missing person" yani kama ambavyo watu wengine walioripotiwa kupotea wanavyotafutwa.
Tunamshukuru IGP kwa kukiri kufahamu suala la Ben. Lkn kutokana na suala hili lilivyo tunaamini si sahihi kumtafuta kama missing person.Ben hakuwa mtoto, wala mgonjwa wa akili, iweje atafutwe kama missing person? Ben amewahi kutoa taarifa Polisi juu ya kupigiwa simu na sms za vitisho. Mtu wa aina hii hawezi kutafutwa kama missing person.
[HASHTAG]#BringBackBenAlive[/HASHTAG]