Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Vyama vya siasa wilayani makete mkoani Njombe vinavyoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa vimetakiwa kufanya kampeni za kistaarabu kwa kunadi sera zao kwa wananchi badala ya kutoa matusi au kufanya fujo
Rai hiyo imetolewa Novemba 19, 2024 na Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Makete William Makufwe wakati akizungumza kwenye kikao cha kamati ya ushauri ya wilaya ambapo pia amesema wilaya hiyo imejipanga vizuri kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani
Kadhalika amewahamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura siku ya jumatano Novemba 27, 2024 kwa wingi ule ule waliojitokeza wakati wa kujiandikisha kwa sababu siku hiyo imetangazwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa ni ya mapumziko
Naye Mkuu wa wilaya ya Makete Juma Sweda amesema vyombo vya ulinzi vipo imara kufanya kazi yake ili kuhakikisha zoezi hilo la kampeni linafanyika kwa mujibu wa ilivyopangwa kwa jeshi la polisi kuimarisha ulinzi hasa kipindi hiki cha uchaguzi wa serikali za mitaa
Amevisihi vyombo vya habari kutoa taarifa zenye manufaa kwa wananchi na taifa kwa ujumla na visijiingize kutoa habari zinazowesha kupelekea uvunjifu wa Amani hasa wakati huu wa uchaguzi.
Kupata mijadala ya kimkoa kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024