Tamko la wafanyakazi wagusia mishahara, maslahi bora kuelekea Mei Mosi 2022

Tamko la wafanyakazi wagusia mishahara, maslahi bora kuelekea Mei Mosi 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limekuja na kauli mbiu kuelekea Mei Mosi 2022 ambapo humo nani wamegusia kuhusu mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi.

Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa TUCTA ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Cde.Hery H.Mkunda.

Kauli mbiu hiyo inasema: “MISHAHARA NA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NDIYO KILIO CHETU: KAZI IENDELEE”

Bado namtafuta Katibu Hery H.Mkunda tujadiliane kidogo kuhusu hili suala.

318659ce-f982-4b43-9e46-becde8f244f6.jpg
 
Msitarajie kitu "Mimi na JPM ni kitu kimoja" miradi ya maendeleo kwanza
Tuwe na mifumo na taasisi imara kupitia Katiba Bora, sio hisani ama hisia na mtazamo wa Mwenyekiti wa CCM/ Rais
 
Ee Mungu wa mbinguni mguse mama tozo atamke jambo juu ya mishahara hasa sekta binafsi
 
Msitarajie kitu "Mimi na JPM ni kitu kimoja" miradi ya maendeleo kwanza
Hiyo miradi utekelezaji wake unafanywa na wafanyakazi Wa umma,binafsi na wananchi wazalendo.

Hakuna Kazi inayoweza kuendelea kama wanaotakiwa kufanya hiyo Kazi hawashibi,watakosa morality,bidii na wanaweza geukia wizi na rushwa kwa sababu hakuna bouncer mbele ya njaa.

Hivi kama mpiga meza na kusema ndiyo analipwa milioni 12 lakini Muuguzi anayekesha na wagonjwa alipwe laki tano,kuna Kazi hapo?

TUCTA pia wameendelea kuwa wanyenyekevu(Down to earth) mbele ya waajiri na kuacha kudai Haki za wanachama wao-Wafanyakazi.

Nchi hii tumezidi Hofu na kutokufahamu au kushindwa kudai HAKI.

Siyo wakulima,wafanyakazi,wafugaji,wavuvi,wafanyabiashara na makundi yote ya kijamii hawathubutu kudai HAKI zao za msingi dhidi ya watawala na watunga Sera na sheria kandamizi ama Katiba Mpya.

Adui anafahamu kutugawa nasi tumesalimu amri.

Uvunjifu Wa HAKI ya mojawetu no uvunjifu Wa HAKI zetu sote na siyo vinginevyo.

Tujitafakari upya.Je,sisi Watanzania in wanyonge mbele ya watawala waliojipa madaraka hata kwa dhuluma za kiuchaguzi/kimfumo!

Je,sisi Watanzania ni watu Huru mbele ya serikali na wanaojiita viongozi?

Hatuna uwezo Wa kudai katiba ambayo mchakato tuliuanza,ukazimishwa na wahuni wachache ambao tokea Uhuru wanatujengea matundu ya vyoo vya shule zetu kwa Hisani ya Watu Wa America au kwingineko?

Inaumiza vichwa vinavyofikiri!
 
Sekta binafsi? Kweli akili ni nywele
Wafanyakazi Wa CCM wameongezewa 80+%.

CCM imeweza lakini serikali yake haiwezi kuongeza hata 50% mishahara ya wafanyakazi wake kwa miaka zaisi ya 7,haiajiri kufuatana na ikama kwenye sekta nyeti kama elimu,afya,kilimo/mifugo(wagani) huku wakijisifia kuivusha nchi kuingia uchumi wa kati chini,kwa kudhulumu jasho la wafanyakazi?

Nasikia hata kwa wastaafu hali siyo hali.

Wajuzi tuambieni,tuendelee kuisifia CCM na Serikali yake ili watukubalie kuandika katiba mpya baada ya 2025?
 
CCM iliyoamiji amini haki za wafanyakazi haipo tena.
 
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) limekuja na kauli mbiu kuelekea Mei Mosi 2022 ambapo humo nani wamegusia kuhusu mishahara na maslahi bora ya wafanyakazi.

Tamko hilo limetolewa na Katibu Mkuu wa TUCTA ambaye pia ni Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa, Cde.Hery H.Mkunda.

Kauli mbiu hiyo inasema: “MISHAHARA NA MASLAHI BORA KWA WAFANYAKAZI NDIYO KILIO CHETU: KAZI IENDELEE”

Bado namtafuta Katibu Hery H.Mkunda tujadiliane kidogo kuhusu hili suala.

Hovyo kabisa !!!!
KUSOKOTWA KWA FAO LA KUJITOA ....MLIUNGA JUHUDI
 
Wafanyakazi Wa CCM wameongezewa 80+%.

CCM imeweza lakini serikali yake haiwezi kuongeza hata 50% mishahara ya wafanyakazi wake kwa miaka zaisi ya 7,haiajiri kufuatana na ikama kwenye sekta nyeti kama elimu,afya,kilimo/mifugo(wagani) huku wakijisifia kuivusha nchi kuingia uchumi wa kati chini,kwa kudhulumu jasho la wafanyakazi?

Nasikia hata kwa wastaafu hali siyo hali.

Wajuzi tuambieni,tuendelee kuisifia CCM na Serikali yake ili watukubalie kuandika katiba mpya baada ya 2025?
Miaka 7 serikali ilikua haiajiri? Huu uongo mnautoaga wapi?
 
Kumbuka pia kila mmoja na zake,hivyo kama wewe unafyeka majani pale halmashauri,na wengine pia tuko kwenye haya makampuni ya urusi tunasogeza maboxsi
Ndio maana nimekuambia akili ni nywele, Sasa raisi anapangaje mshahara wa sekta binafsi? Sekta binafsi ni makubaliano kati yako na anayekuajiri hata akiamua kukulipa bil 1 kwa mwezi ni wewe na yeye, hata ukiamua kumfanyia kazi bure ni ww tu
 
Back
Top Bottom