Msitarajie kitu "Mimi na JPM ni kitu kimoja" miradi ya maendeleo kwanza
Hiyo miradi utekelezaji wake unafanywa na wafanyakazi Wa umma,binafsi na wananchi wazalendo.
Hakuna Kazi inayoweza kuendelea kama wanaotakiwa kufanya hiyo Kazi hawashibi,watakosa morality,bidii na wanaweza geukia wizi na rushwa kwa sababu hakuna bouncer mbele ya njaa.
Hivi kama mpiga meza na kusema ndiyo analipwa milioni 12 lakini Muuguzi anayekesha na wagonjwa alipwe laki tano,kuna Kazi hapo?
TUCTA pia wameendelea kuwa wanyenyekevu(Down to earth) mbele ya waajiri na kuacha kudai Haki za wanachama wao-Wafanyakazi.
Nchi hii tumezidi Hofu na kutokufahamu au kushindwa kudai HAKI.
Siyo wakulima,wafanyakazi,wafugaji,wavuvi,wafanyabiashara na makundi yote ya kijamii hawathubutu kudai HAKI zao za msingi dhidi ya watawala na watunga Sera na sheria kandamizi ama Katiba Mpya.
Adui anafahamu kutugawa nasi tumesalimu amri.
Uvunjifu Wa HAKI ya mojawetu no uvunjifu Wa HAKI zetu sote na siyo vinginevyo.
Tujitafakari upya.Je,sisi Watanzania in wanyonge mbele ya watawala waliojipa madaraka hata kwa dhuluma za kiuchaguzi/kimfumo!
Je,sisi Watanzania ni watu Huru mbele ya serikali na wanaojiita viongozi?
Hatuna uwezo Wa kudai katiba ambayo mchakato tuliuanza,ukazimishwa na wahuni wachache ambao tokea Uhuru wanatujengea matundu ya vyoo vya shule zetu kwa Hisani ya Watu Wa America au kwingineko?
Inaumiza vichwa vinavyofikiri!