Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 3,984
- 13,760
Aidha, amezitaka Bodi hizo kuhakikisha wanaendelea kusimamia miradi ya ujenzi ikiwemo barabara, madaraja na majengo na kuhakikisha wajenzi na wasimamizi wa miradi hiyo wanafanya kazi kwa kuzingatia miiko na maadili ya taaluma zao.
Waziri Bashungwa anatoa pole kwa majeruhi na familia iliyopoteza mpendwa wao na anatoa wito kwa Wakandarasi, Wahandisi na wamiliki wa majengo kuhakikisha wanatumia wataalam waliosajiliwa na Bodi za CRB, ERB na AQRB ili kuepusha kutokea kwa madhara yanayoweza kusababisha majeruhi na vifo, na hivyo kupoteza nguvu kazi ya Taifa.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi
=========================
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Ujenzi
=========================
Mwanaume mmoja ambaye ni Fundi wa ujenzi aliyefahamika kwa jina moja la Omary maarufu Mwarabu amefariki dunia na Mafundi wenzake wanane wamejeruhiwa baada ya jengo la ghorofa mbili ambalo walikuwa wanaendelea kulijenga kuporomoka leo April 17,2024 katika Mtaa wa Magogoni Wilayani Kigamboni Mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Halima Bulembo amefika eneo la tukio ambapo ameagiza Vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya uchunguzi ili kujua chanzo cha ghorofa hilo kuporomoka na pia kujiridhisha kama ujenzi ulifuata sheria na taratibu za ujenzi huku akitoa rai kwa Wananchi wote wanaojiandaa na ujenzi kupata vibali kabla ya kuanza kwa ujenzi ikiwemo kibali kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ili kuepusha ajali zinazoepukika.
Kwa upande wake Afisa Zimamoto Wilaya ya Kigamboni, Mkaguzi Innocent Kirway Ingbertus ameiambia @AyoTV_ kwamba ghorofa liliporomoka wakati Mafundi wengine wakiwa juu na wengine chini hivyo kupelekea kufunikwa na mmoja ambaye alikuwa eneo hatarishi lenye shimo alifunikwa na zege na kufariki
“Mkandarasi wa ujenzi aliondoka eneo la tukio na hajarudi hadi sasa, Mmiliki wa jengo pia hajafika eneo la tukio”
Chanzo: Millard Ayo