Jamani hii michezo ya kuigiza na tamthilia za magharibi katika runinga zetu hapa bongo zimekuwa nyingi hadi zinawachanganya wapenzi/wafuatiliaji wake na mara nyingine inakuwa kero kwa watu wengine wasio wapenzi wa vipindi hivyo. Mbaya zaidi wapenzi wa vipindi hivi ni wanafunzi hasa mabinti wanaokaa macho hadi saa tano au sita usiku kufuatilia michezo hiyo badala ya kusoma, na stori zao shuleni mara nyingi huwa juu ya tamthilia hizo.
hahaha na hivo vitoto navyo tamthilia zenyewe zinaanza saa tatu au saa nne fungia watoto wote room wakasome hawajui elimu ni ufunguo wa maisha
dah ila kweli tamthilia zimezidi
First lady
We huwa unaangalia ipi?
Hii kweli kabisa wazazi wanatakiwa wawe wakali kwa watoto wao, kama haiwezekani wawapangie vipindi vya kuangalia.Kwa ujumla uangaliaji wa TV ni sumu mbaya sana kwa maendeleo ya watu especially wanafunzi.zinaharibu Academic life ya mtu.Ni vizuri wazazi wawe wakali kwa hili kwa watoto wao.Jaribuni kuwazuia wasiangalie badale yake wasome.Mtoto ukimuendekeza unamuharibu.acheni kuwapa upendo wa kijinga watoto.
Hili pia ni hata watu wazima,tupunguze jamani kupoteza muda kuangalia tv zinadumaza akili,badala yake tusome vitabu jamani vinalipa!
Kwa ujumla uangaliaji wa TV ni sumu mbaya sana kwa maendeleo ya watu especially wanafunzi.zinaharibu Academic life ya mtu.Ni vizuri wazazi wawe wakali kwa hili kwa watoto wao.Jaribuni kuwazuia wasiangalie badale yake wasome.Mtoto ukimuendekeza unamuharibu.acheni kuwapa upendo wa kijinga watoto.
Hili pia ni hata watu wazima,tupunguze jamani kupoteza muda kuangalia tv zinadumaza akili,badala yake tusome vitabu jamani vinalipa!