Katavi
Platinum Member
- Aug 31, 2009
- 42,023
- 12,811
Jamani hii michezo ya kuigiza na tamthilia za magharibi katika runinga zetu hapa bongo zimekuwa nyingi hadi zinawachanganya wapenzi/wafuatiliaji wake na mara nyingine inakuwa kero kwa watu wengine wasio wapenzi wa vipindi hivyo. Mbaya zaidi wapenzi wa vipindi hivi ni wanafunzi hasa mabinti wanaokaa macho hadi saa tano au sita usiku kufuatilia michezo hiyo badala ya kusoma, na stori zao shuleni mara nyingi huwa juu ya tamthilia hizo.