Tamthilia ya Bibi Titi Mohammed na Prof. Emmanuel Mbogo

Maalim Faiza,
Umeeleza vyema sana hali ya watu kuukubali ukweli baada ya kulishwa
uongo kwa muda mrefu.

Kuna barua ya Kleist Sykes anajibu barua ya Mzee bin Sudi mwaka wa
1933, Kleist akitabiri kuwa kazi hii ya African Association walioianza wao
itakujwa kumalizwa na watakaokuja baada yao.

Hebu tustaladhi na kipande hiki hapo chini:

Abdulwahid sasa akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa amekamilisha lile
lengo lake kubwa katika maisha yake, lengo ambalo lilianza kwa marehemu
baba yake ambaye miaka 21 iliyopita alitabiri kuendelea kwa mapambano
kati ya Waafrika wa Tanganyika na serikali ya kikoloni.

Kleist Sykes alikuwa halikadhalika ametabiri jukumu la kizazi kijacho. Katika
barua aliyomwandikia Mzee bin Sudi, rais wa African Association, mwaka
wa 1933, Kleist katika umri mdogo wa miaka 29, akiwa kijana mdogo sana
aliandika maneno haya:

‘’Tupambane kwa nguvu zetu zote kuelekea njia ya ustaarabu kama vile watu
wa makabila mengine wanavyofanya.

Haidhuru kitu ikiwa hatukamilishi kila kitu.

Wale watakaokuja baada yetu watakamilisha yatakayobakia.’’

Kwa hakika Kleist alikuwa mtu wa fikra.

Alizungumzia kuhusu ''ustaarabu,'' ambao hivi leo ungemaanisha ''kujitawala,''
na kuhusu, ''makabila,'' ambayo TANU imeyageuza kuwa ''taifa.''

Katika mwaka wa 1954 robo karne baadaye katika jengo lilo hilo, 25 New Street
ambalo Kleist alisaidia kulijenga kwa njia ya kujitolea, kizazi kipya nchini
Tanganyika kilikuwa kikiigeuza African Association aliyoiunda katika mwaka 1929
kuwa chama cha siasa.


Lengo lake lilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kujitawala.

Miongoni mwa waliokuwa wakiongoza harakati za kudai uhuru zilizokuwa zikiibuka
walikuwa watoto wake watatu, Abdulwahid, Ally na Abbas.


Kushoto: Kleist Sykes, Abbas nyumna ni Ally na Abdul
picha hii ilipigwa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam
kutoka Kabete Kenya alipokuwa akifanya mafunzo ya kijeshi
katika KAR kabla hajaondoka kwenda Burma katika Vita Vya
Pili Vya Dunia.



Kutoka Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York

Hii ndiyo historia ya TANU.
 
kwa sababu alijiaminisha , kuwa yeye ndiye yeye
 
Kujiaminisha hakuibadilishi historia. Au?
no, kwasababu alikuwa mbinafsi na kutaka kutukuza , leo hii wanaimba kama sio juhudi zakee............na uhuru tungepata wapi..je hauoni huu ni umimi ambao yeye alijijengea mazingira?
 
no, kwasababu alikuwa mbinafsi na kutaka kutukuza , leo hii wanaimba kama sio juhudi zakee............na uhuru tungepata wapi..je hauoni huu ni umimi ambao yeye alijijengea mazingira?


Nimekuelewa.

Huko ndiko nnakokuita kuwajaza watu ujinga.
 
Nimekuelewa.

Huko ndiko nnakokuita kuwajaza watu ujinga.
Yaaah!! tena huu ujinga na kushindwa kujenga hoja kwa watanzania ,na unafiki ulokithiri yeye ndo muasisi wake..... leo hii somo la historia linafunzwa ,kuhusu uhuru yupo yeye mpaka inakosa mvuto.....watu wanashindwa kuijua nchi yao na kukosa uzalendo , madini yanaondoka tuu...mpaka hua nina wasi kuwa kuna mkataba ameingia huko na jamaa kuhusu mali zilizopo ardhin..haiwezekani tuna kila kitu tunakosa dira
 


AlhamduliLlah, leo tunayajuwa hayo.
 
una Kila haja sasa, kuona tulikosea wapi, ....kujipanga upya tunahistaji raisi mzalendo asiye endekeza ubinafsi na mtengano miongoni mwa jamii....hasa katika kupiga hatua madhubuti...
 
Aksante sana,maalimu kwa kutuletea historia hii mwanana hasa wakati huu wa mwisho wa mwaka.Nataman nikipate nikisome wakati huu wa mapumziko.
 
Wakati wa sherehe ya Mwalimu Nyerere kutimiza miaka 75,bibi Titi alimsifu sana Mwalimu na akasema ,mwalim akifa hautakuwa msiba wa familia bali msiba wa taifa.Baada ya kumpamba sana Mwalimu,Bibi Titi alisogeleana na mwalimu wakabusiana deeply.Bond yao nadhan ilikuwa strong sana.
 
Wakati wa sherehe ya Mwalimu Nyerere kutimiza miaka 75,bibi Titi alimsifu sana Mwalimu na akasema ,mwalim akifa hautakuwa msiba wa familia bali msiba wa taifa.Baada ya kumpamba sana Mwalimu,Bibi Titi alisogeleana na mwalimu wakabusiana deeply.Bond yao nadhan ilikuwa strong sana.
 
Sidhani kama kuna jambo jema lolote lile ambalo umewahi kulisema kuhusu Nyerere na members wengine wa TANU hasa waislam!! Mtu yeyeto akiamua kufanya utafiti kwa basis ya kutafuta negativity ya binadamu tambua kuwa haiwezi kukosekana kamwe!!

Sidhani kama unatambua madhara ya mbegu na nguvu kubwa unayowekeza katika maandishi yako kuhusiana na uhuru wa Tanganyika!

Unajidanganya na kujinasibu eti unajaribu kurekebisha makosa, lakini huo ni unafiki wa mchana kweupe!!

Ukweli ni kwamba unapandikiza chuki hadharani dhidi ya pande mbili kwa sababu unazozijua mwenyewe!!

Mtu mwenye busara hujikita kueleza mambo mazuri yanayofaa kuigwa vizazi na vizazi kuliko unavyofanya wewe!!

Nadhani una mengi unayoyafahamu kuhusu wapigania uhuru wetu, je, haitoshi kutupa historia yao pasipo kuhusianisha na ugomvi au misuguano na Nyerere!?

Ni busara kutumia maarifa yenu kujenga nyumba imara (pande zote) kuliko kujaribu kupandikiza chuki dhidi ya pande fulani!
 
Uncle...
Umenita mnafiki.

Nitashukuru endapo utanithibitishia hilo kwa maana ya unafiki kama inavyokubalika
kwa wasemaji wa Kiswahili.

Pili hili la chuki nipe ushahidi katika maandishi yangu kama kuna chuki.
Tatu ujenzi wa nyumba imara inahitaji msingi imara.

Msingi imara unakuja kwa kuwa na haki sawa kwa wote.
Sikiliza tunayosema:
Mohamed Said: WAISLAM WA TANZANIA NA TATIZO LA UDINI KATIKA WIZARA YA ELIMU
 
Wakati wa udogo wangu wazazi na walezi wangu waliniasa sana kutobishana na wakubwa. Mara nyingi kijana anapofanya hivyo huonekana kupungukiwa adabu!!?

Nakuheshimu sana, itoshe mimi kuamini ujumbe umekufikia kwani mimi si wakwanza kukwambia hayo!

Kwa umri, uzoefu na elimu uliyonayo ni dhahiri kwamba maana nzuri ya neno uliloomba nikupe maana yake unaifahamu tena hata asili ya na matumizi ya mwanzo ya neno lenyewe (mnafiki) naamini unajua.

Kuhusu mbegu ya chuki, narudia tena waweza kuwa unatambua kabisa na unafanya makusudi au unaandika na hupimi madhara ya maandishi yako kwa upande wa pili katika jamii.

Maandishi yanaishi, sidhani kama watoto na wajukuu zako wangependa kuona huko mbeleni maandiko yako yakitumika kuhamasisha na kuchochoe kelele za hapa na pale badala ya kutumika kutuliza kelele zinapoibuka!!

Si dhambi baadhi ya mambo yaliyofanywa na wakubwa na yanayoonekana yakiwekwa hadharani huenda yakachochea minong'ono isiyo mizuri kubaki huko huko yalipo!

Ndio maana hata kama babu wa babu alikuwa mchawi au mwanga katika familia fulani, baba mwenye busara hawezi kujihangaisha kuelezea watoto wake namna babu huyo alivyokuwa maarufu kwa uchawi labda kama anataka watoto warithi uchawi huo!

Nchi nyingi zina siri kubwa kubwa na viongozi wengi wana siri na wanafahamu mengi kuhusu waliowatangulia

Vijana wana tamani kufahamu siri za ushindi wala sio nani alimnyang'anya nyumba nani na alikuja kurudishiwa na nani!

Kuna mengi mazuri ya kujifunza kutoka kwa kina Bibi titi, familia ya Skyes, Nyerere na wengine wengi sana walioshiriki kuikomboa Tanganyika!

Lakini kwa namna unavyowasilisha mada zako, kuna mengi mazuri unayaacha ambayo pengine ndo ya msingi sana na watu wangejifunza kitu kuliko kujaza hadithi za migogoro Kati ya fulani na fulani!

Aidha nikutakie heri ya Krismas na baraka tele tunapoelekea kuupokea mwaka mwingine tena!
 
Kuna watu waliipigania nchi yetu kwa jasho lakini kuna wasiotaka wajulikane kwa vizazi vya sasa na vijavyo, na hapo suala la udini limehusika. Hongera yake Bibi Titi Mohamed. Mkuu Mohamed Said hicho kitabu kinapatikana wapi?
Ukisema hivyo utakuwa unakosea mwanajukwaa
Tofauti ni kawaida ktk dunia hii
Katika kila harakati kunakuwa na mtu wa kuzipamba hizo harakati
Ni kweli mtupu kuwa uhuru uliletwa na watu wengi na kuwataja wote haiwezekani
Ni katika kumfuatilia huyo aliyeleta uhuru ndio tunajua ni akinanani alishirikiana nao
Kwa mfano Mwl alisema kuwa bila wazee wa dar es salaam ambao wengi walikuwa waislam asingefanikiwa ktk harakati zake
Bibi Titi ni shujaa na vizazi vitaendelea kumkumbuka milele
 
Betony,
Tatizo la historia ya Tanganyika iliingia kasoro pale baada
ya uhuru zilipotengenezwa njama za kuwafuta baadhi ya
wazalendo na kujaribu kuibadili historia nzima.

Ndiyo maana ikawa historia nzima inazunguka kwa mtu
mmoja.

Hili nililitambua nilipokuwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam
na nilibishana sana na walimu wangu kuhusu hili.

Walikuwa wabishi na ilhali hawana moja walilokuwa wanalijua
kuhusu historia hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…