Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #41
Maalim Faiza,Naam, na ndiyo maana tunapeana darsa.
Kwa hakika uongo ukisemwa sana mwishowe huwaingia watu na kuuona ni ukweli na hata anafundishwa ukweli bado haumuingii akilini.
Kuna watu chungu nzima humu wakiambiwa TANU haikuasisiwa na Nyerere na hata jina la TANU hajalitowa yeye, basi hiyo kabisa haiwaingii akilini kwa kuwa tu wameshajazwa ujinga.
Nyerere alikuwepo wakati TANU inaundwa 1954 lakini hakuwa muasisi wala hakuwa mtoa wazo, wazo lilikuwepo kabla hajajiunga na waasisi wa kupigania Uhuru wa Tanganyika waliokuwepo Dar.
Of course Nyerere alikuwa msomi wa kutokea Ulaya na alikuwa ni nguzo kubwa alipojiunga na wapigania Uhuru wa Dar lakini hakuwa muasisi.
Hilo ni ngumu sana watu kulikubali, kwanini?
Umeeleza vyema sana hali ya watu kuukubali ukweli baada ya kulishwa
uongo kwa muda mrefu.
Kuna barua ya Kleist Sykes anajibu barua ya Mzee bin Sudi mwaka wa
1933, Kleist akitabiri kuwa kazi hii ya African Association walioianza wao
itakujwa kumalizwa na watakaokuja baada yao.
Hebu tustaladhi na kipande hiki hapo chini:
Abdulwahid sasa akiwa na umri wa miaka 30, alikuwa amekamilisha lile
lengo lake kubwa katika maisha yake, lengo ambalo lilianza kwa marehemu
baba yake ambaye miaka 21 iliyopita alitabiri kuendelea kwa mapambano
kati ya Waafrika wa Tanganyika na serikali ya kikoloni.
Kleist Sykes alikuwa halikadhalika ametabiri jukumu la kizazi kijacho. Katika
barua aliyomwandikia Mzee bin Sudi, rais wa African Association, mwaka
wa 1933, Kleist katika umri mdogo wa miaka 29, akiwa kijana mdogo sana
aliandika maneno haya:
‘’Tupambane kwa nguvu zetu zote kuelekea njia ya ustaarabu kama vile watu
wa makabila mengine wanavyofanya.
Haidhuru kitu ikiwa hatukamilishi kila kitu.
Wale watakaokuja baada yetu watakamilisha yatakayobakia.’’
Kwa hakika Kleist alikuwa mtu wa fikra.
Alizungumzia kuhusu ''ustaarabu,'' ambao hivi leo ungemaanisha ''kujitawala,''
na kuhusu, ''makabila,'' ambayo TANU imeyageuza kuwa ''taifa.''
Katika mwaka wa 1954 robo karne baadaye katika jengo lilo hilo, 25 New Street
ambalo Kleist alisaidia kulijenga kwa njia ya kujitolea, kizazi kipya nchini
Tanganyika kilikuwa kikiigeuza African Association aliyoiunda katika mwaka 1929
kuwa chama cha siasa.
Lengo lake lilikuwa kuwatayarisha Watanganyika kujitawala.
Miongoni mwa waliokuwa wakiongoza harakati za kudai uhuru zilizokuwa zikiibuka
walikuwa watoto wake watatu, Abdulwahid, Ally na Abbas.
Kushoto: Kleist Sykes, Abbas nyumna ni Ally na Abdul
picha hii ilipigwa 1942 Abdul aliporudi Dar es Salaam
kutoka Kabete Kenya alipokuwa akifanya mafunzo ya kijeshi
katika KAR kabla hajaondoka kwenda Burma katika Vita Vya
Pili Vya Dunia.
Kutoka Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York
Hii ndiyo historia ya TANU.