C-C Digital Pro
JF-Expert Member
- Mar 15, 2026
- 361
- 532
Mtunzi: CIVILIAN-COIN N.K
Tamthilia: "MJI WA MAPOYOYO"
©2026, Kahama, Tanzania.
Haki zote za Kitabu hiki zimehifadhiwa.
UTANGULIZI NA LENGO LA MWANDISHI/MTUNZI..
Mwandishi wa tamthilia ya "Mji wa Mapoyoyo" ni Civilian-Coin Nalimi Kisandu kwa kifupi CIVILIAN-COIN N.K au CIVILIAN-COIN Kama anavyojitambulisha, anatokea kabila la Wasukuma na mzawa na mkazi wa Manispaa ya Wilaya ya Kahama, Mkoa.wa.Shinyanga,Tanzania.
Yeye ni mwandishi, mwanahabari, mtafiti, na msanii wa muziki kutoka nchini Tanzania.
Tamthilia ya "Mji wa Mapoyoyo"
iliyoandikwa na Civilian-Coin ni kazi ya kifasihi, mwandishi anatumia tamthilia hii kama kioo cha jamii ili kuweka wazi uozo uliopo na kuchochea mabadiliko ya kifikra kwa wananchi dhidi ya mifumo inayowadhalilisha. Pia ambayo inalenga kuikosoa na kuamsha jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayoharibu maadili na mfumo wa uongozi.
SEHEMU ya 1.
Anaingia kwenye Kikao Cha Kamati ya Kutengua viapo, anajiona amechelewa Sana, alipoingia tu ukumbini, kelele na vificho na alipokaa kwenye kiti, makofi yakaanza kupigwa, ndipo Mshehereshaji wa sherehe akamkaribisha Bwana Hatari awasalimie waliomo ukumbini.
Hatari akapokea kifaaa Cha kusemea yaani Microphone akasema" Nawasalimu kwa jina la Uvurugaji mipango SUGU, KAZI mliyonituma kuwafanya watu mapoyoyo ni ngumu sana ila ninambinu nyingi Sana, bajeti ya Pesa za kutosha iandaliwe ili kufikia maadhimio, Asanteni" akakaa Chini.
SEHEMU YA 2.
Ndugu Hatari kabla hujafika tulipendekeza majina manne ukiwemo wewe Ila kura zote zimekuangukia wewe kuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati hii na Mtemi wa Mji huu wa Mapoyoyo na hivyo kuanzia Sasa wewe ndio Mtemi wetu na Mwenyekiti wetu, je uko tayari? Aliuliza Madam Kimeo mmoja wa wajumbe. Naye Hatari alijibi kwa ufupi tu "Mimi ndio bosi wenu kuanzia Leo".
Ukumbi ukalipuka vigeregere vya furaha Kama ishara ya kumkubali. Basi Mwenyekiti Kaa sehemu Yako ya cheo chako na Kikao kiendelee, alisema Mshehereshaji. Katibu tunaomba ajenda za Kikao Cha Leo, aliagiza Mwenyekiti.Katibu alianza kusoma ajenda: Ndugu wajumbe wa Kamati hii ya Kutenguas Viapo ajenda za Kikao Cha Leo ni 1. Kuzuia Ushoga na Usagaji au tuache waendelee, 2. Kuzuia Ukahaba Kama ajira, 3. Mimba za utotoni na mimba za uzeeni, 4. Wazee nao wanahitaji mapenzi, 5. Michepuko ruksa, 6. Sadaka ni mtaji 7. UKIMWI nao upo hai na mwisho ni kufunga Kikao. Asante Sana. Katibu japo ajenda ya kwanza inakugusa Sana wewe maana nakujua fika huna Malinda na Manisha wewe ni shoga na tunakujua hivyo utatupa uzoefu wako Kama Vijana wa Mji huu wa Mapoyoyo waige mfano wako au wasiige. Alisema Mwenyekiti na akaendelea kusema: Sasa nafungua Kikao rasmi na karibuni kwa hoja za msingi ila Mimi sio shoga. Madam Kimeo anadakia nakusema: Wewe Mwenyekiti acha kutupumbaza bwana, najua fika mme wangu ni Basha wako kabisa na mkeo anajua hilo. Mimi ndio naongoza Kikao kwanini Tena mnanichafua? Aliuliza Mwenyekiti.
SEHEMU ya 3.
akaendelea, unajua Madam Kimeo nakuheshimu Sana, Ukahaba wako tumeuficha halafu unaropoka tu hapa na Mimi ndio nilikuwa mteja wako kwenye danguro lenu mpaka nikakuokoa nakukupatia mmeo au ni mwambie mmeo ulikuwa kahaba uone Kama ndoa Yako haivunjiki, alihoji. Mzee wa BUSARA nimeona mkono wako labda una hoja aliuliza Mwenyekiti.
Ndio na hoja bosi, basi karibu. Inamaana humu ukumbini wajumbe wote hawana Malinda mpaka wanawake Tena Cha kushangaza Maafisa ni Makahaba na mashoga. Duh!! Huu mfumo mkali kweli. Mwenyekiti anacheka na kumwambia Mzee wa BUSARA: utaikubali tu SYSTEM YETU huwezi kufanikiwa mpaka tukutoe Malinda au uende kwenye madanguro yetu ukawe Changudoa. Mjumbe mmoja anainuka bila kibali Cha Mwenyekiti. Naomba twende kwenye ajenda nasio kudhalilishana.
SEHEMU YA 4.
Sawa sawa mjumbe, tuanze na ajenda ya kwanza na tunaanza na wewe uliyesema twende kwenye ajenda, tafadhali toa hoja Yako, tufanyeje hii jamii iwe ya mapoyoyo, alisema Mwenyekiti. Mjumbe alianza kutoa hoja: ndugu Mwenyekiti, sisi wanawake mmezoea kutupachikia tu mnafikiri hatuchokagi? Sasa ni zamu yenu Wanaume kushika ukuta ili mjue Radha ambayo wanawake huwa tunafaidi au lah, Mimi naona ushoga uendelee ili Wanaume msitutawale na Wala msiwe na sauti ili tuwafanye mapoyoyo maana bila kuwashogesha kuwa mashoga mtatupelekesha Sana Bora mtoane tu Malinda ili muwe sawa na sisi wanawake. Swala la kusagana kiendelee maana Wanaume wengine hawajui mapenzi na pia sisi wanawake ni Bora tusagane ili tusiwasaliti waume zetu kwa mahawala zetu.
Asante mtoa hoja, alisema Mwenyekiti. Mjumbe mwingine akaunga mkono hoja' Mwenyekiti naungana na mjumbe aliyepita ni kweli Wanaume tukiwa mashoga hata kiongozi akiwa mwanamke basi Wanaume watamnyenuekea kwa kuhofia ushoga wao, hata kwenye mapenzi mwanaume akiwa shoga anakuwa Hana sauti maana na yeye anakuwa Kama mwanamke tu maana sianashika ukuta.Pia Mimi ni shoga Ila Binti wa Mwenyekiti ni demu wangu kabisa na ananipenda Sana, alisema mjumbe, Mwenyekiti alipoga meza na kusema, aisee, hii ni aibu ya mwaka yaani Binti yangu anampenzi shoga, Leo nikitoka kikaoni naenda kufukuza nyumbani siwezi kuwa na mkwilima shoga. Ukumbi ukalipuka vicheko. Madam Kimeo akaongezea; unajua Binti Yako Mwenyekiti ni kahaba hapa mjini na hawezi kuolewa kwa uchangudia wake ndio maana amemng'gang'ania huyu shoga na huyu shoga hawezi kupata mke kwa ushoga wake ndio maana kamchukua Binti Yako maana anajua fika ni kahaba. Mwenyekiti anamjibu Madam Kimeo kwa kusema "kwenda zako huko, usinichafulie Binti yangu".
Lakini Mwenyekiti na wazo hapa, alisema Mzee wa BUSARA na kuendelea; Hawa Mashoga na Makahaba ni watoto wa Mji huu wa Mapoyoyo nao ni watu Ila changamoto za kimaisha zimewafanya kuwa hivi na wengine imekuwa Kama utamaduni wao, Mimi naona tuwaingize kwenye ajira za Mji wetu, tufanye nao KAZI tu maana ni watoto wa Mji wetu, mtoto akinya utazoa tu mavi yake, tuwasafishe kwa kuwapatia KAZI za kufanya hata za ulinzi au vyovyote kuliko kuwaacha waangamie, alisema Mzee wa BUSARA. Madam Kimeo naye anadakia, Bwana Hatari nachojua Mimi ajira Sasa ni ngumu sana na elimi hatujasoma na wengine Wazazi maskini Sana, wengine waume zao kula kulala na hicho kinasababisha wanawake tuwe Makahaba tupate Pesa za kujikimu Ila sisi sio Malaya ni njia ya kujiokoa pia hii ni miili yetu Tena msitujadili wanawake hata nyinyi mna makalio mkiamua kushikanisha ukuta mpate Pesa za kujikimu ni maamuzi yenu. Mwenyekiti anawauliza wajumbe: Sasa tuendelee na Maisha haya ya ushoga na Ukahaba au tuzuie maana naona Kama mnapenda Sana kuishi haya Maisha ya kipoyoyo, basi tupige kura. Mzee wa BUSARA akasema: Haina haja ya kura hapa ni kuzuia tu huu mfumo. "Hamna kuzuia, Kama tunazuia basi tuhamie kwa Mwenyekiti nyumbani kwake tuwe tuna kula Bure, Mimi naona acha tupoyoyoke".
SEHEMU YA 5.
Katibu naona Kama unajambo hebu Nena tukusikie, anasema Mwenyekiti. Katibu anaanza kuongea; mwisho wa Kikao Bwana Hatari atatoa mwelekeo wa agenda zote hivyo twende ajenda zingine na muda nao hauko nyuma yetu. Wajumbe kwa sauti Moja "Tuendelee". Nimeona humu Ndani Kuna Mwalimu hebu atupe hoja, eeeh, safi Sana, nimemuona Mwalimu, hebu Mwalimu karibu, amesema Mwenyekiti. Asante Sana, Mwalimu anaendelea; Mimba za utotoni si nzuri kwa gharama za Maisha japo ni nzuri, tatizo mtoto anazaa mtoto mwenzake na aliyemzalisha ni mtoto mwenzake, Sasa nani mlezi na mtoa matumizi maana watoto wamezaa mtoto mwenzao na hawana KAZI Wala ajira na hawajajitambua bado kujua majukumu ya Baba au Mama na mwisho wa siku mtoto inabidi alelewe na Babu au bibi yake, Sasa wameingiza gharama mpya kwenye familia. Tuwaambie ukweli Wana wa Mji huu wa Mapoyoyo. Madam Kimeo anasimama nakusema; siungi mkono hoja', huo ni ushenzi mtupu, ina maana huyu Mwalimu hajui Raha ya mahaba, au anataka watoto watue sisi? watoto wetu wanapenda Sana michezo ya Siri ya Baba na Mama. Wanafunzi ukiwazuia kucheza baba na mama wanaugua Chekelea. Huyu Mwalimu ni POYOYO kabisa hata watoto wake wanaakili kuliko yeye labda alisoma Mgugumbaru. Rabia una jambo hapo? aliuliza Mwenyekiti. Rabia anasema; Huyu Mwalimu ni shoga mwenzio, hivyo Mimi naendelea na ajenda ya wazee. Karibu Sana, alisema Mwenyekiti.
Rabia akaendelea; Mimba za uzeeni ni nzuri Sana maana baba anakuwa mtu mzima hata mtoto akikua vipi hatalingana bado itaonesha baba au mdogo mtu au mtoto, hii ni nzuri Sana maana baba mtu mzima na mkewe ni Binti mdogo tu wakipata mtoto yaani safi hata malezi yanakuwa poa Sana maana baba ni mtu mzima na anajitambua na anajua majukumu ya mkewe na mwanaye. Mwalimu anaingilia kati nakusema; wajumbe kumbe huyu Rabia ni Kahaba kabisa mbona ameongea pumba Sanaa, Bora twende ajenda ingine. Mwenyekiti anasema; haya Mwalimu tupe uzoefu wako Sasa kwa sisi Wazee, kwanini Vijana wanadhani wazee hatuna mihemko ya mapenzi wakati Babu yangu ana miaka 102 lakini tukimpelekea mwijukuu wake kumfariji, eeeeh, acha kusema weweeee, anapiga mashine kweli kweli, Sasa kwanini Hawa mabinti hawatutaki baba zao, Kuna msemo wa kibongo unasemaga hivi; mtoto wa mwenzio mkubwa mwenzio maana mkipeana baba na mama mnazoeana na kuwa sawa, lakini Si kwa mtoto wako. Je, wewe Mwalimu unalionaje hili. alisema Mwenyekiti. Mwalimu anaongea; Hata tu kutoka mtoko au viwanja na mtu mzima inapendeza Sana kuliko kutoka mtoko au viwanja na mtoto mwenzio. Madam Kimeo Kama ada yake anasimama nakudakia, japo huyu Mwalimu ni shoga lakini kwa hili, jamani ameongea vizuri, nimekupenda Sana Mwalimu basi tu umechelewa nimeolewa ila hakijaharibika kitu, mme wangu ni Basha mzuri Sana, nikimusimulia haya lazima atakubali kuwa Basha wako maana Mimi nimechoka, Kila siku kushika ukuta, hebu nisaidie mwenzangu.
Mwalimu anafura kwa hasira "hivi wewe Madam Kimeo unanichukuliaje Mimi, Mimi ni msomi wa Chuo kikuu, acha kejeli", wajumbe wanacheka, Madam Kimeo anamjibu Mwalimu; Sasa wasomi ndio wenyewe Sasa, wanamaliza vyuo wasomi Milioni Moja Kila mwaka na ajira hakuna, huwezi amini wengine tunakutana nao anga za Mji huu wa Mapoyoyo, Mzee wa BUSARA ana digrii saba lakini lakini mme wangu Basha wake. Mwenyekiti anainuka nakusema; naomba kumtoa kwenye Kikao hiki huyu madam Kimeo maana Hana utu kabisa Ndani mwake, anaongea ujinga ujinga tu, wajumbe mnasemaje? anauliza Mwenyekiti. Wajumbe " utoke wewe Mwenyekiti". Mwenyekiti anapigwa na butwaa, Mara anasema: hakika huu ndio Mji wa Mapoyoyo.
SEHEMU YA 6
Ndugu wajumbe naomba utulivu japo kidogo naona Kama Kikao hakiko sawa, Rabia naona Kama una jambo la ghafla hebu sema lolote, Sasa nimechoka na mipasho yenu, yaani Mimi Katibu natumia akili yangu kuandika mhtasari wa Kikao hiki kwa kuandika mipasho mwanzo mwisho, Mimi siwezi kuandika Mapoyoyo yenu hayo, aje mwingine awe Katibu. Wajumbe; mchague wewe umtakaye. Katibu akasema; namchagua Rabia mmbeya Kama bajaji za kwenda busoka inyembe, na kuanzia Sasa nakabizi ofisi kwa Katibu mpya. Katibu mpya anaanza KAZI huku Mwenyekiti akiwa anasinzia kwa mipasho ya wajumbe, Ndugu wa jumbe wa Kamati ya Kutengua viapo naomba Sasa tupige kura ya kutokuwa na Imani na Mwenyekiti maana hatukuja hapa kulala, ona Sasa Mwenyekiti ana domo BAYA Kama la ng'ombe akiwa usinguzini. Tulitumbueni kwa kura,.halina lolote lipoyoyo tu Kama mlivyo ninyi wajumbe. aaah,aaah, mwalimu alishangaa nakusema tumekupa ukatibu Sasa hivi tu halafu unatuita sisi POYOYO, kweli wewe Binti, kweli. akadakia Katibu mpya anasema; tupo tunaishi kwenye Mji wa Mapoyoyo hivyo wewe ni POYOYO, na ukiulizwa ulizaliwa wapi, siutajibu POYOYO, unatokea wapi? siutajibu POYOYO, kwa hiyo wewe asili Yako ni wapi? siutajibu POYOYO. Basi wajumbe ninyi ni Mapoyoyo. Sasa tupige kura, naona Mwenyekiti ameamka na sura Kama parachichi na maharage ya mchina. ghafla, heeeee, hivi nilipitiwa na usingizi, hebu niambieni mmefikia wapi? Mwenyekiti anauliza. Katibu mpya anajibu, tulipofikia Mimi Rabia ndiye Katibu mpya baada ya Katibu wa zamani kujiudhuru na pia Sasa tunapiga kura ya kutokuwa na Imani na Mwenyekiti. Pia mkeo kafumaniwa ananyengwa. Haaah, Mwenyekiti anashangaa na kuendelea;Rabia mtoto mzuri kweli, mke wangu kanisaliti, nimemleta mjini mwenyewe, basi nakunywa sumu.
Rabia anamjibu Mwenyekiti; nyoka Wana sumu mwilini na wewe ukinywa sumu utakuwa na sumu Kali Sana mwilini kuliko hata ya nyoka Ila usitugonge tu. Aaaayah, huyu mwanamke kichaa ninini! anaongea mambo gani haya, anafikiri Mimi sipendi kuishi, anasema Mwenyekiti. Katibu wake mpya anamjibu; wewe siumesema unakunywa sumu, Sasa unaogopa Tena kufa, kwenda zako huko, POYOYO wewe. Wajumbe tayari kwa kura? wajumbe wanaitika; tuko tayari. Basi Sasa mpendekeze jina la mwenyekiti mwingine ili tuyashindanishe na hili zuzu la kulala fofofo hata vikaoni. Nesi anasimama anasema; tunataka mwanamke na sisi tujaribu kuwatawala walau kidogo hawa.mapoyoyo wa Mji wa Mapoyoyo, Madam Kimeo ndio chaguo letu. Katibu mpya anauliza; mnasemaje wajumbe?; imepita hiyo, nani Kama mama! Bwana Hatari Chali Chali Chali kabisa mpaka awe POYOYO. Asanteni wajumbe na ujumbe umepokelewa na hivyo Mwenyekiti mpya wa Kamati ya Kutengua viapo na Mtemi wa Mji wa Mapoyoyo Mheshimiwa Sana Madam Kimeo, pita uje uchukue nafasi Yako ili tuendelee na Kikao, basi Madam.Kimeo alikaa kwenye kiti chake na kumuomba Mwenyekiti mstaafu kusema machache naye Bwana Hatari anasema Sasa; Bora mapoyoyo mmenitoa maana najisikia aibu Sana KUINGIA Mji huu wa kifahari wa Mapoyoyo na kuwaongoza mapoyoyo mpaka na wewe uwe POYOYO ndio watakuelewa. Nesi anamjibu Hatari; acha wehu, unataka Kila kitu tukukubalie hata Kama jambo la kipoyoyo, kafie MBELE huko, POYOYO mkubwa Sana wewe, Sasa na wewe umekuwa mtawaliwa, tulia tukulee, huna lolote Tena. Mwenyekiti mpya anasema; nilifikiri labda litang'gang'ania kiti kumbe Lina BUSARA japo POYOYO. Mwenyekiti anaendelea: ajenda mezani, tuendelee, muda unakimbia Sana masela.
aaah aaah, Mwenyekiti mpya samahani Sana, Tena Sana, tunaomba usituongozee Kikao chetu kihuni, tumia lugha rasmi, tafadhali, alisema mjumbe. Kwenda huko, huwezi kwenda na Kasi yangu, alijibu Mwenyekiti nakuendelea; haya Sasa Nesi tupe uzoefu wako wa kuchepuka tuone Kama tuendelee kuchepuka au tupunguze maana nje nako kumenoga Babu weee, Nesi akasimama, anaanza kuongea; kuchepuka mtaani kwetu sisi ni fasheni, ukiwa huchepuki unaonekana umepitwa na wakati, sisi hospitalini akija mgonjwa mwenye mihela hela kulazwa, heeeh lazima nishike ukuta aniache hata na msimbazi, wajumbe wanacheka, kumbe na ninyi manesi mpo Mji huu kupoyoyoka. Hatari Sana, aliongea mwalimu. Sawa,.naomba kumsikia Mwanasaikolojia akichangia, mtaalaam karibu Sana, Mwenyekiti mpya anamkaribisha mwanasaikolojia naye anaanza kuongea; Iko hivi wajumbe, michepuko ni halali kisaikolojia kutokana na maumbile ya mwili kubadilika. kikawaida Kila mwanamke ana mme wake rasmi na si Kila mtu, Iko hivi, mwanamke ameondolewa usichana wake na mwanaume mwenye bamia kwa hiyo hiyo bamia inakuwa saizi ya huyo mwanamke. Na mwanamke akimsaliti mpenzi wake mwenye bamia kwa mwanaume mwenye Ndizi au mhogo basi maumbile ya mwanamke yanaongezeka kutanuka na hivyo mpenzi wako mwenye bamia atapwaya au ataogelea na atamsaliti mmewe kule aliko panuliwa upya. Kwa mantiki hiyo, michepuko tunaitengeneza sisi wenyewe kwa kukosa viongozi wazuri wa jadi na Mila.
Asante Sana mwanasaikolojia, Leo nakupa offa maalum, baada ya Kikao hiki, nikute chumba namba 5 Pale Mapoyoyo Hotel and Lodge ili ni kubembeleze mtoto wa kiume, halafu ni Mtanashati Kama jini mahaba, aliongea Mwenyekiti. ndugu Mwenyekiti, huyu sio Mwanasaikolojia ni tapeli Fulani tu hapa mji wa Mapoyoyo, Lina swaga tu Kama lisomi vile, Tena usilione hivyo ni likahaba la kiume ndio maana limekunasa viziri, limejua fika likiongea jambo Fulani litakupata na linajua Mwenyekiti mpya ni lipoyoyo, weee lione hivi tu, kwenye harusi Lina kula mpaka ukoko, lilafi Kama mme wa Rabia. Alisema mjumbe mwingine wa benchi la nyuma. Mwenyekiti anamkaribisha Mwanasiasa kuchangia hoja, Mheshimiwa Papara una lipi kwa michepuko? baelezee bhana Mji wa Mapoyoyo bhana kusikiliza sana, Mwasikitoko ipo mingi Sana pigia kura bhebhe, Mwenyekiti akitumia rafuzi ya kilingala kumpamba Mwanasiasa. Mheshimiwa Papara anasema; sisi Wanasiasa swala la michepuko hatuna tofauti na madereva wa magari ya malori yanayokwenda.Burundi, Kongo, Zambia yaani Kila kituo mchepuko. sisi kwa kweli Kama nazungukia mitaa ya wapiga kura Kila mwanaume mwenye ushawishi wa watu mtaani kwake na mkatikia tu maumo, mauno si ya kwetu, mbona kwenye miziki mnakata mauno hadharani, sisi tunawakatikia mauno wapiga kura wetu SEHEMU za fargha ili watupigie debe tuendelee kula Bata na kuku, tatizo lenu ninyi ni Mapoyoyo Sana mnaona Kama sisi Maboya fulani hivi, kumbe si hivyo.
Mwalimu anadakia; ona hopulesi kabisa hili jeshimiwa halina hata haya, sura Kama chapati za Bharesa, mbuzi wa kike wewe, kumbe ndio michezo yenu Wanasiasa, kwa hiyo mmoja akiwa na ngwengwe simtatuambukiza Mji mzima wa Mapoyoyo na hivi mnaitwa Waheshimiwa kumbe nyuma Kuna magendo ya mahaba nirubuni, hii kiboko. Kaa kimya Mwalimu hiki Kikao Kama hatujaenda choo Cha kike basi tumeenda chaka, kwa maelezo ya Mheshimiwa Papara, hawa Wanasiasa na watu maarufu wapimwe Ngwengwe na watakaobainika watangazwe hadharani au wajitolee wao kujitangaza ili wajulikane wasije wakaambukiza wengine kwa lazima au kwa hiari au kwa rushwa au kwa upendo wa dhati, na wapimwe akili kwanini wanauana wakati wa chaguzi au wakizidiwa hoja wanatekana, Mara wanapigana Mara wanafungana Kama maigizo hivi Ila nafurahi maana nao kumbe wapo Mji huu wa kifahari wa Mapoyoyo. Samahani wajumbe tupate breki kidogo tunywe chai naona gari la chai limewasili, hivyo Kikao kitarejea baada ya kumaliza kupata chai. alisema Mwenyekiti.
SEHEMU YA 7
Basi Sasa tuendelee na Kikao baada ya breki fupi, Mzee wa BUSARA tupe uzoefu wako wa kuvuta bangi, je ni sawa au sisawa, aliongea Mwenyekiti. Mzee wa BUSARA anaanza kutoa hoja; ndugu wajumbe kuvuta bangi kisheria ni kosa Ila kikatiba hakuna kosa maana ni Moja ya haki za binafamu, Kuna miji Watemi wao wameruhusu uvutaji wa bangi na bangi wameitoa kwenye kundi la madawa ya kulevya, wamejipima na kufanya experiment (majaribio) na kuona Haina madhara hata kidogo kwa binadamu, bangi inatumika Kama ganzi mahospitalini, bangi wengine hutumia Kama mboga Tena tamu Sana, bangi wengine hukoroga kwa maji na kunywa Kama dawa na bangi wengine huvuta Kama sigara ili kuongeza nguvu za kufanya KAZI nzito, unapofanya KAZI nzito Sana ukivuta bangi inakuwa nyepesi Sana ila ukivuta bila kufanya KAZI inakulewesha hiyo ndio husema bangi ni dawa za kulevya. Pombe zinaleweshwa na kushindwa kufanya KAZI lakini bangi ukivuta inakupa morali wa KAZI, Sasa kipi ni Bora, tunywe pombe tuwe maskini au tuvute bangi tupate Pesa, jibu ni jepesi tu, hebu wajumbe toeni jibu, alisema Mzee wa BUSARA, wajumbe wakaitikia; Bora tuendelee kula bangi. Mzee wa BUSARA akaendelea: Hilo ndio jibu sahihi naomba mpigie mstari, na pia mateja ni wale wa unga sio bangi.
Mimi naona Mji wetu huu wa Mapoyoyo bangi iendelee na Kama hamtaki Mimi nitahamia Jamaika nyumbani kwao Bob Marley huko poa Sana. Mwenyekiti akadakia; sawa kabisa Mzee wa BUSARA, kumbe unakula wida almaarufu ganja, msuba, Cha Arusha aiseee, ndio maana unaona mbali Sana, usijali Mzee wa BUSARA, Mimi ndio Madam Kimeo Mtemi wa kwanza wa kike kwenye huu Mji wa Mapoyoyo, nasema bangi ruksa, jiachieni tu na Wala hakuna dhambi hata MBELE za Mungu, hio ni mimea ametupa Mwenyezi Mungu tuitumie kwa chakula, dawa na kivuli. Bangi kwetu marastafara wa Mji wa Mapoyoyo ina matumizi mengi Sana na hivyo tukitoka hapa anzeni kula wida ila isiwe hadharani Sana maana wengine wanaamini ni dhambi kumbe wao ndio wenye dhambi, safi Sana Mzee wa BUSARA. Mwalimu ameshasimama na anaanza kufoka; Mwenyekiti mpya kumbe boya kabisa yaani unaunga mkono matumizi ya bangi wakati Sheria za Mji wetu wa Mapoyoyo haziruhusu, hivi mnacheza na Sheria au Mimi sijijui, ngoja kesho na Mimi nionje bangi nione huu upuuzi wenu Kama ni kweli. Mwalimu unachekesha tu, alisema.mjumbe. Katibu mpya anasema; Mimi bangi huwa inanipa Raha kwenye mapenzi hasa nikipata dume la kweli.
Mwenyekiti anamkaribisha Hatari kuchangia, Bwana Hatari karibu, alisema Madam Kimeo, Bwana Hatari anaanza kuongea; Bangi marufuku kwenye Mji wetu, nawaambieni kutakuwa na VICHAA wengi na vurugu Kila Kona Kama mkiruhusu huu upuuzi wenu wa bangi, shauri yenu. Nesi anaingilia kati nakusema; Bwana Hatari ni hawala yangu kabisa na huwa anavuta bangi kwa maelezo aliyotoa hapa Sasa hivi, nimegundua Hatari ni likichaa ndio maana tumemnyanganya Uenyekiti wetu. Lipotezeeeeni tu.
Anasimama Mchungaji; samahani Mwenyekiti Mimi nataka kuwahi kwenye Ibada naomba niondoke. Mwenyekiti anajibu; Bora umejiinua, kabla hujaondoka hebu tueleze sadaka zetu kanisani tunazotoa huwa mnapeleka wapi? Asante Mwenyekiti, anaendelea Mchungaji wa Kanisa la Mapoyoyo Church Ministry; kwanza sisi Wachungaji ni watu maskini Sana na hivyo ajira yetu ni Kanisani, tunawahamasisha kutoa michango mbalimbali, yote ni mbinu tunaitumia kupata Pesa kutoka kwa waumini, tunaitumia maeneo nyeti ya Maandiko Kama kutoa fungu la kumi kanisani Kila KAZI unayofanya Kama zaka kwa Mungu, kwa hiyo kwa kuwa watu ni Mapoyoyo na wanatuamini Sana, basi wanatuletea fungu la kumi, jioni sisi na wake zetu tuko viwanja tunatanua tu kwa mahela yenu, tunajenga majumba, tunanunua magari ya kifahari, halafu mnatuheshimu mpaka basi. Watu walivyo Maboya tukiwaambia KAZI ya Mungu haihojiwi basi mnatuamini na sisi tunaendelea kupeta tu uswahilini, hivi hamuoni Kila Mtaa siku hizi Kuna viji Kanisa na Mziki mnene, sisi ndio watu wa Imani aiseeee, Kila mtu atakula kwa urefu wa kamba yake na Mchungaji atakula madhabahuni. Swala la kwenda mbingini wataenda waumini, sisi KAZI yetu Wachungaji ni kusaka Pesa na mazingaombwe yetu ya miujuza ili mtutajirishe, tuna mbwembwe sisi, acha tu. Shombo anadakia; Mwenyekiti na Mimi niongee kidogo; huyu Mchungaji kanifungua kitu Fulani kizuri Sana, watu wanakalia kusali Kila siku kanisani Ila kufanya KAZI hawataki wao wanataka kusali tu, Sasa nani awafanyie KAZI wao wale tu. Basi Mungu wao awatendee mujiza wa kuletewa chakula Kila siku. Mimi sitatoa sadaka Wala fungu la ugoko wa Mchango kwenye kanisa.lolote, yaani Bora wafe njaa tu. Asante Mchungaji japo nakuona Kama Jambazi hivi. Wajumbe wanacheka.
Mwenyekiti anauliza Kama Kuna swala la nyongeza maana ajenda za msingi zimeisha. Daktari Bingwa wa DNA anapewa nafasi ya hoja ya nyongeza na anaanza kusema; tuna changamoto ya watoto kwenye Mji wa Mapoyoyo wasio fanana na sura na baba zao. Wanaume wengi wanalea watoto wasio wao bila kujua na wengi waemefungwa akili kwa malimbwata. Hainiingilii akilini Yani demu wangu anazaa mtoto hafanani na Mimi halafu anadai ni mtoto wangu huku sura hazifanani kabisa. Huu ni utapeli wa Wanawake maskini Sana ili uendelee kulea watoto wake bila wewe kujua huku akishirikiana na mzazi mwenzie ambaye naye ni maskini mwenzie, hii ni staili ya kuponea migongoni mwa watu wenye ahueni wa Maisha. Sasa ukitaka kujua mtoto ni damu Yako, Cha kwanza; jikumbushe sura yako ya utotoni na angalia sura ya mtoto wanayesema ni wako, ukiona zafanana, basi huyo ni mwanao na Kama sura hazioani kabisa basi hapo umeliwa chekundu, hivyo nenda kapime maabara DNA na mtoto ili kuzibitisha, hapo mwanamke lazima akukimbie maana anajua DNA itamuumbua vizuri Sana. Tabia hii chafu ife hapa Mji wa Mapoyoyo ya wanawake kuwabambika mimba za mahawala zenu watu wengine, komaa na aliyekupa mimba na sio kumtelekezea mwingine. Asante Daktari Bingwa wa DNA anasema Mwenyekiti mpya na kuendelea; Sasa Daktari unataka kuharibu Dili za wanawake, hebu mambo yetu wanawake tuachieni wenyewe mbona mambo yenu ya ushoga hatuingilii, alisema Mwenyekiti mpya naye Katibu anasema; hii hoja nimeiandika Ila mtoa hoja anatabia ya ushoga Fulani hivi, Tena na mjua vizuri maana mkewe ni shosti wangu huwa ananisimulia jinsi hili lidaktari lilivyodata.
SEHEMU YA 8
Muda wetu umeisha Sasa tunafanya majumuisho ya Kikao hiki, anaongea Mwenyekiti. Mjumbe mmoja anasimama na kusema; mbona ajenda ya UKIMWI iliyoletwa mezani haijajadiliwa? Mwenyekiti anajibu; ina maana hujui maana ya ngwengwe, tafsida ya UKIMWI ni ngwengwe, tumetumia tafsida maana ukitaja neno UKIMWI wengi wanaogopa, hivyo tumesha jadili na Sasa ni majumuisho, tuanze na Mwenyekiti mstaafu Bwana Hatari, Bwana Hatari anasema; Sasa wote twende tukairekebishe jamii kuwa na Maadili safi na kuepuka Mila na tamaduni mbovu ili kujenga jamii mpya. Asante Hatari, Katibu zamu Yako Sasa,anasema Madam Kimeo. Katibu Mpya anaanza kuongea; sisi inatakiwa tuonekane Bora Sana kuliko wananchi wetu, hivyo twendeni tukawageuze watu kuwa Mapoyoyo yetu. Asante Rabia, zamu Yako Mzee wa BUSARA, anasema Mwenyekiti. Mzee wa BUSARA anaongea; naunga mkono hoja' na mwelekeo wa Bwana Hatari. Asanteni wote, anasema Mwenyekiti na kuendelea, Mimi ndio msemaji wa mwisho, hapa tumepata makundi mawili tofauti, kundi la Kwanza twende tukawafanye wananchi Mapoyoyo na kundi la pili twende tukajenge jamii mpya yenye Maadili safi. Hivyo sipingani na makundi yote, wote mko sawa, Sasa hapa tupo wajumbe 100, wajumbe 50 mkatengeneze jamii mpya yenye Maadili safi na wajumbe wengine 50 twende mkaifamye jamii kuwa ya mapoyoyo, baada ya mwaka mmoja tutaitisha Kikao kingine kuja kufanya tathimini ni kundi gani limeonesha mwanga na mafanikio ya Ajenda zetu. Asanteni Sana, niwatakie siku njema na Kikao kimefungwa rasmi. Makofi yanapigwa na wajumbe Kama ishara ya kukubaliana na Mwenyekiti mpya na Mtemi wa Mji wa Mapoyoyo.
...........MWISHO.........
TAFSIRI YA MANENO:
MAPOYOYO: Jina lenyewe la mji, "Mapoyoyo," kiasili linamaanisha watu waliochanganyikiwa, wajinga, au wasiojitambua, jambo linaloashiria kuwa mji huo unaongozwa au umejaa vurugu za kifikra.
MIPASHO: Katika utamaduni wa Kiswahili, mipasho ni usemi, maneno, au nyimbo zenye mafumbo, vijembe, na usiri uliowazi ambazo hutumika kumsema au kumkanya mtu fulani bila kutaja jina lake moja kwa moja. Lengo kuu la mipasho huwa ni kuelimisha, kuonya, kusuta, au kukosoa tabia na mwenendo usioridhisha katika jamii.
BASHA: Mwanaume anayemuingilia mwanamke kinyume na maumbile ya mapenzi au anayemuingilia mwanaume mwenzake kinyume na maumbile.
SHOGA: Mwanamme anayejihusisha na mapenzi ya jinsia Moja au mwanamke anayetumia SEHEMU ya haja kubwa Kama SEHEMU ya mapenzi.
MTOKO; matembezi.
VIWANJA; eneo la starehe.
MWASIKITOKO; Mrembo kwa lugha ya Kilingala.
MASELA; watu wa karibu.
DEMU; mpenzi.
DNA; vina saba vya kuthibitisha uhalisia kisayansi au kibaiolojia.
NYENGWA; Fanya mapenzi.
SHOSTI; rafiki.
NGWENGWE; ina maana ya UKIMWI.
MAUDHUI YA TAMTHILIA HII:
Katika tamthilia mpya ya "Mji wa Mapoyoyo" iliyoandikwa na mtunzi Civilian-Coin N.K (2026), lengo kuu au dhamira ya mwandishi katika jamii ni kukemea mifumo inayowafanya wananchi wasijitambue (kuwafanya 'mapoyoyo') na kufichua hila zinazotumiwa na viongozi laghai ili kuendelea kutawala na kulaza jamii akili. Kupitia wahusika kama Bwana Hatari na Kamati ya Kutengua Viapo, mwandishi anaakisi uhalisia wa changamoto za kiutawala na kijamii.
Umuhimu wa Mabadiliko:
Kwa kuweka wazi uovu huo, mwandishi anatoa wito wa mabadiliko ya kifikra ili jamii ijikomboe kutoka kwenye pingu za uongozi dhalimu na ulaghai.
Tamthilia hii ya "MJI WA MAPOYOYO" pia inapatikana katika mfumo wa google na mitandao mingine online Kama jamiiforums, ccdigitalpro.com.free n.k, [email protected].
0790 368046 namba ya mtunzi.