Tamthilia ya Siri ya mtungi (wahapahapa) ndio filamu bora kuwahi tokea Tz

Ipo haja serikali pia kupitia kitengo husika kutafuta wafadhili na kushirikiana na nchi wahisani kwa ajili ya mambo kama haya ni namna nzuri sana ya kujitangaza huko duniani..
 
Niliwahi kuongea na mtengenezaji filamu mmoja miaka ya 2010, akaniambia kuna wakati msambazaji anakwambia atatoa 25m kwa movie nzima. Hiyo hela ulipe wasanii, location, mavazi, chakula, script writers, usafiri etc. Ndio maana movie zinakuwa za kipumbavu, hata translation ni za ajabu ajabu; movie inafanywa haraka haraka bila umakini kabisa.

Itoshe kusema, Siri ya mtungi ilikuwa na ufadhili wa kutosha.
 
Niseme tu kwa upande wangu ile filamu ilikuwa bora sana. Waigizaje wake walivaaa uhusika vema pia director alijitahidi.

Ile kwa mm ndio project na tamthilia bora toka nchini kwetu. Huwezi fananisha na uchafu wa saluni ya mama kimbo
ivi nitaipataje hii tamthilia maana ata sijui iliishia vip? nimejaribu kuitafuta youtube lkn wapi ?
 
Niseme tu kwa upande wangu ile filamu ilikuwa bora sana. Waigizaje wake walivaaa uhusika vema pia director alijitahidi.

Ile kwa mm ndio project na tamthilia bora toka nchini kwetu. Huwezi fananisha na uchafu wa saluni ya mama kimbo
Hii waigizaji walifanyiwa hadi aptitude test,kuna msanii mmoja maarufu marehemu kwa sasa alikosa nafasi ya kuuliza mule baada ya kuleta ustaa na kushinda kujibu maswali
 
Lakini kwanni asiandaw kitu bora ili ajihakikishie soko lake?
 
Hii waigizaji walifanyiwa hadi aptitude test,kuna msanii mmoja maarufu marehemu kwa sasa alikosa nafasi ya kuuliza mule baada ya kuleta ustaa na kushinda kujibu maswali
Safii ndo sanaa inapaswa kuwa natamani sana director kama wale waje kisha kitabu cha hadithi ya mwandishi hussein tuwa kinaitwa mkimbizi akitengenezee filamu
 
Yes uhalisia upo sana kwenye hizi tamthilia kama Jua Kali
 
Lakini kwanni asiandaw kitu bora ili ajihakikishie soko lake?
Finance hakuna mkuu.

Unajua hata kwa wenzetu, movie zinagharimu pesa nyingi sana lakini mara nyingi sio pesa za mfukoni, ni uwekezaji. Movie kama Titanic, hakuna mtu anaweza kutengeneza, mara nyingi ni mabenki makubwa na wawekezaji binafsi wanaotoa pesa.

Kwa mfano kazi ya kutafsiri Kiswahili kwenda Kiingereza; kwa wanaofanya kazi professionally, inalipiwa kwa kila neno. Sasa imagine movie ya Saa 1.30 ina maneno mangapi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…