Tamu na chungu ulizopitia wakati unaanza biashara yako

Mnamo tar21 mwez wa tisa mwaka huu nlifungua wakala (mpesa, tigo, airtel, na halotel) kariakoo nakumbuka cku hyo ckufanya muamala hata mmoja. Nliwaza nkamwambia Mungu n nini hiki sasa. Daah wateja wakawa kidogo wanakuja mwanzo wa mwez wa kumi ka kamishen kakaja hakafiki hata elfu hamsini daah kweli nkavunjika moyo sana.

Leo namshukuru Mungu kidogo wateja wanakuja japo nnaamini hadi mwakani nitasmama kwa kudra za mwenyezi Mungu. Sitaki kabisa kuajiriwa kwakuwa nishaajiriwa miaka miwili skuambulia chochote zaid ya kulipa kodi na kununua vitu vya ndani bas
 
Mwaka Jana nilizichanga sana kwa kusave mshahara wangu mwezi wa tatu mwaka jana nikaamua pesa yangu kuiongezea samani(kuiwekeza)nililima nyanya heka moja tukiwa na dogo baada ya kumaliza chuo cha ualimu,wazoefu wakatwambia "tutafute watu wengine 2 tuwe wa 4" Nilikataa kata kata tukijiamini kazi ya kuhudumia nyanya heka moja haitotushinda(tumekulia familia za wakulima wale wa kutumia nguvu).Tukapambana ikafika mda tukawa hatuongeleshani mpaka mda wa kula,nyanya zilikuja iva huku zingine hazijafungia fito.Mwanzoni tenga tukawa tunauza 40,000/= lakini kila kukicha bei ilizidi kushuka (mwezi wa sita mwishoni),mbaya zaidi shamba likavamiwa na vipepeo huku wateja hawapo(ukifika shambani shamba zima limekuwa jekundu) baada ya wiki mbili shamba zima wakaibuka funza wakatobowa nyanya zote.Nashukuru kila pesa niliyokuwa nauza niliandika mwisho wasiku nikapata 700,000/= baada ya kutumia 1,600,000/=.

Kumbuka mwaka huo huo nilikuwa nimelima heka 3 za pamba maana kila niamkapo asubuhi nilikuwa nakigongagonga kifua changu na kunuia "mke wangu mtarajiwa nikija kukuoa lazima ufikie kwenye nyumba yako tena nzur". Pamba ilianza kunishangaza kwenye mwezi wa NNE ikawa inarefuka tu Hata haizai kwa ufupi pamba haikuzaaa (WAZIRI WA MIFUGO NA KILIMO Mungu anakuona kwa ulichonifanyia 2017/2018).kwa ufupi mbegu tulioletewa ilikuwa mbovu.Mwisho wa siku nilipata 240,000/= baada ya kutumia 600,000/=.Huo mwaka ulikuwa mwaka wa shetani kwangu.Sahivi silimi tena huwa nawasubilia tu wakiivisha nanunua mazao naweka stock nashukuru now day pesa yangu haipotei.
 
Icho kitu kingne ulichoamua kukiwekeza tupe mwaga nacho nikipi
 
Mzigo gani huo mkuu[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Tuotee fursa
 
Why uliacha mkuu??? Samahani kwa maswali lakini
 
kitu pekee nilichoambulia ni kuitwa bossi na wale vibarua,

asee huwa naumia sana moyo unakuta unaitwa boss,mkuu,mheshmiwa lakn moyon unaujua ukweli kwamba hata chai hujanyww
Hatari sana mkuu.
 
Hapo sawa mkuu...!! So kwa sasa hiyo biashara huwezi mshauri mtu aifanye ausio???
 
King999 umenichekesha sana tena sana.Binafsi kwa sasa baada ya kuteleza mara kadhaa katika biashara ikabidi nitulie na niwaze kwa kina nikaibuka na hitimisho biashara/kilimo ni taaluma kama taaluma zingine za ualimu/udaktari/uanasheria n.k, hivyo ili uifanye kwa uhakika na ufanikiwe kwa unachokifanya huna budi kuisomea hiyo taaluma hata kwa mfumo usiorasmi kwa kufanya utafiti ili ukusanye taarifa za kina zenye mbivu na mbichi kabla ya kuanza.
 
Daah we jamaa mwepesi sana kupiga chini vitu
 
ahahaa , nilidhani peke yangu tu
 
huenda wife sio jambaz ila matumizi yake yalizid margin/profit mana mwanamke akiona mavitu yamejaa dukan anahan kama kuna faida lundooo kumbe faida ni mia mya mbili tu
yani aliposema mkewe ni mlokole, bila shaka alikuwa anapeleka mauzo yote kanisani na sadaka mbalimbali alikuwa anatoa, mavuno, fungu la kumi, malimbuko, wajane, yatima, ujenzi wa kanisa, ahadi nk.... makanisa yetu ya siku hizi haya ni mufilisi
 
safi sana mkuu, nami nafanya biashara hizo pia, na nilitamani siku moja nami nipate goli town k/,koo
 
nami kuajiriwa nimekataa kabisa baada ya kupitia msoto wa ujob less, nikaona nijiajiri.
 

Safi sana chief ulijua kufanya kitu kimoja kikubwa cha kujivunia (close deal) afu sasa biashara ilivyo ya ajabu unaweza leta awamu ya pili isiwe kama ulivyotegemea
 
Mkuu hao mbwa wa kisasa ni kweli wanafugwa au msemo tu?
Mkubwa salama

huwa napenda kuyasemea mambo ambayo nayaishi
fanya utafiti mtaani kwako kwa watu wanaofanya hizi mambo.

labda nikupe hints kidogo

ukiwa na dume la pure breed ya gs (giant) kupandisha majike mengine siyo chini 1m
puppies wa pure breed ya gs wanauzwa 1.5 kwa mmoja, kashuka sana bas 1.2

chotara yaani cross puppies wanauzwa 500k umeshuka sana basi 450k kwa mmoja.

kwanini nihangaike na kuku wa kisasa ambao ni stress tu.
 
Daah we jamaa mwepesi sana kupiga chini vitu
Na ndo alifeli hapo pale kwenye nguruwe angekomaa napo maana alishakuwa mzoefu maana changamoto huja ili Upate Uzoefu

japo na Mimi ninachangamoto ila sikati tamaa
 
n sahh mkuu biashara ukiivaa kichwa kichwa unaweza kuta inakupiga za uso
yaan knowledge is the basic of any bussness
 
yani aliposema mkewe ni mlokole, bila shaka alikuwa anapeleka mauzo yote kanisani na sadaka mbalimbali alikuwa anatoa, mavuno, fungu la kumi, malimbuko, wajane, yatima, ujenzi wa kanisa, ahadi nk.... makanisa yetu ya siku hizi haya ni mufilisi
na wanawake wa sku hz wanamsikiliza pastor kuliko mme wake
 
Hizo mbao gani mkuu ulikuwa unachukulia wapi
 
Kwahiyo hauna biashara/mradi wowote pembeni mbali na ajira yako kwa mantiki hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…