Tamu na chungu ya wauza maziwa barabarani

Tamu na chungu ya wauza maziwa barabarani

MrKanteChelsea

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2019
Posts
203
Reaction score
237
Wanachelewa kulala lakini wanawahi kuamka, ni kina mama wauza maziwa katika Kituo cha Nyichoka Kata ya Kyambahi Wilaya ya Serengeti ili kuwahi wateja kwenye mabasi yanayopita saa 12 kuelekea Musoma,Bunda na Mwanza.

Kwa kuwa wengi wao hukamua wenyewe ,huwalazimu kuanza saa 10 alfajiri muda ambao unatajwa kuwa ni hatari kwa kuwa wanyama wakali kama Simba na Tembo hurandaranda katika maeneo yao ambayo yanapakana na maeneo yaliyohifadhiwa.

Ili kujua undani wa shughuli yao ikiwemo kukamua,maandalizi hadi kuingia Sokoni,timu ya Serengeti Media Centre inalazimika kutinga Kitongoji cha Songambele saa 10 alfajiri na kubahatika kukutana na akina mama hao..

Tazama Hapa Makala Haya >>>>



makala hii nikeipenda wana jukwaa wenzangu kama kuna mtu ashawahi kupita hapo ataelewa hadi huruma
 

Attachments

  • FB_IMG_1654575330987.jpg
    FB_IMG_1654575330987.jpg
    25.4 KB · Views: 18
Hiyo ni fursa watu wakafungue viwanda vya maziwa ili kuwapa soko la uhakika na kuongeza tija sijui neno huruma linaingiaje katika tasnia ya ujasiriamali biashara ni suala la demand & supply, markerting
ndio nimeona huruma vile ambavyo wanapambana kweli wanatakiwa kusaidiwa
 
Kama pesa inapatikana hakuna uchungu wowote, >jambo baya ni kuwalaumu waliosababisha kiwanda kikafungwa mf, Mara Diaries ilikuwa ni mkombozi kwa ukanda huo ila sababu mnaijua wenyewe why?.

Alafu mnajiita Serengeti Media Center 😂😢!, Kama wadau wa habari kwenye makala yenu mlipaswa muwe na segment tatu as, why, whom and solution.

Hapo mngeweza hata kutanabaisha uundwajibwa viwanda vidogo vidogo kwa usindikajibwa maziwa, although nafahamu kule kisii Kenya ni jirani na hapo so bado kuna uwezekano wa kuwauzia wakenya maziwa.
 
Back
Top Bottom