Naima Ernest
Member
- Apr 5, 2013
- 41
- 22
Kashfa kubwa imelikumba shirika la hifadhi la Taifa(Tanapa)na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) baada ya baadhi ya maofisa wake wenye vyeo vya juu kukubali rushwa ya dola 20,000 Kutoka kwa Mkurugenzi wa Mbugani Camps Ndugu Barnaba Molel.
Mkurugenzi huyu ambaye anaswaka na vyombo vya ulinzi na usalama,na inahisiwa ametoroka nchi kupitia njia za panya na kwa msaada wa maofisa hao wa Tanapa wasiokuwa waaminifu.
Barnaba ni mtuhumiwa namba moja wa kesi namba 6/2021 Economic crimes Daniel Ndorosi and others,kesi hii inafuatia askari wanyamapori kukamata nyama pori aina ya Pofu ambayo ni nyara ya serikali na ambayo iliwindwa kinyume cha sheria.Nyama hiyo ilikamatwa ndani ya jambo yake iliyopo eneo la Ndutu upande wa Ngorongoro,mwanzoni mwa mwaka huu 2021.Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka kwa baadhi ya wafanyakazi wa kambi hiyo umekuwa utaratibu wao wa kila siku kula nyama pori wanazowinda ndani ya hifadhi kinyume cha sheria.
Utaratibu wao huko husaidiwa na baadhi ya watu wa Tanapa,kwa takribani miaka mitatu mfululizo tumekuwa tukiwinda na kula nyama pori kwa msaada wa Tanapa na NCAA ambao hulipwa kiasii cha hela na tajiri yetu Barnabas..amenukuliwa mfanyakazi ambaye ameomba kuficha jina lake.
Barnaba ambaye ni mkurugenzi wa mbugani camps amejificha au kutoroka nchi kupitia maeneo ya Ngorongoro ili kukwepa mkono wa sheria,hata hivo inaaminika amekuwa na mawasiliano na baadhi ya vigogo wa Tanapa kwa lengo LA kutoa rushwa ambayo wamekubaliana uwe USD 20,000 ili asinyanganywe site yake iliyopo Serengeti Turner river.
Kwa mujibu wa sheria ni kosa kwa mmiliki au mfanyakazi wa hotel kuwinda mnyama, adhabu yake hotel hufutiwa kibali cha kufanya shughuli zake ndani ya hifadhi husika na hifadhi nyingine.Kwa kuwa nyama imekamatwa tena ya mnyama ambaye ni nyara ya serikali Tanapa walipaswa kuchukua uamuzi wa kisheria badala yake wanafanya mazungumzo ya rushwa!
Huyu mkurugenzi alikuwa diwani wa Chadema katika Halmashauri ya Longido hadi mwaka 2020,lakini kuna tetesi kuwa sio RAIA wa Tanzania