Tanapa na wizara ya mali asili na utalii mna mpango gani na biashara ya utalii?

Upekuzi101

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2020
Posts
221
Reaction score
542
Salamu kwa wote.
Kutokana na kuporomoka kwa dollar, wafanyabiashara ya utalii wamejikuta wakipata hasara kubwa kutokana na exchange rate ya Tanapa kubaki kuwa 2609 Tzs huku thamani ya dollar sokoni ni 2300$.

Pamoja na serikali kusisitiza matumizi ya shillingi bado kwenye biashara ya utalii dollar ndio hutumika kumchaji mgeni.

Mgeni lazima amlipe tour operator kwa exchange rate inayoonekana mtandaoni hasa rate inayotangazwa na BOT, kinyume chake Tanapa wao wamebaki palepale kwenye rate yao ya 2609Tzs.

Kama Tanapa hawatakuwa wasikivu na kutembea na rate ya BOT kama inavotangazwa kila siku, basi mtaua utalii wenyewe kwa kuifanya kuwa biashara isiyokuwa na faida tena.

Tatizo dogo kama rate isirudishe nyuma juhudi za Rais Samia za kukuza utalii. Au pendekezo jingine ni kuweka viwango vya park fees kwa shillingi za kitanzania Ili kuepusha kukimbizana na exchange rate za kila siku ukizingatia dollar inazidi kuporomoka kwa kasi na hatujui huenda ikafika hadi 1500tzs kwa dollar 1 ya kimarekani.
 
Mama Samia alishakataa biashara za dhulma. Wajirekebjshe
 
Kwani bado malipo yanafanyika kwa dollar za marekani?
Iko hivi: Malipo yote yanafanywa kwa shilingi za Kitanzania. Unapataje basi hayo malipo. Mf kama kuingia ndani ya baadhi Hifadhi zetu kwa Mgeni ni USD 60 plus 18% VAT basi utalipia kiwango hicho kwa Tshs (60×2609) +18%. Sasa tatizo linakuja pale ambapo exchange rate ya Wizara ya Maliasili haviendani na ile ya BOT. (Mnrt ni 1 USD = Tshs 2609/= wakati BOT ni 1 USD = 2330/=) na bado inaendelea kuporomoka.
 
Sasa hapa mbona bado matumizi na malipo ni kama yanafanyika kwa dollar. Nilitarajia waweke kwa shilingi. Hata kama naenda jan nikute bei hiyo. Maana ake exchange zoteziafanyika bank ama maduka ya kubadili fedha na malipo kuanza kufanyika.

Lakini hilo kama linafanyika Tanapa sio sahihi kabisa ni kuwaumiza wateja wao. Hizo diff za unit 300 unazifidia vipi?

Labda nao tour operators wana namna wanachaji wateja wao.
 
Yes, that's how it is
 
Hakuna namna ya kuchaji wageni kitofauti yaani tour operator wanalia sana ni kama Serikali na Tanapa wameziba masikio
 
Back
Top Bottom