Tanapa yadhibitisha taarifa za moto kuwaka mlima Kilimanjaro na kusema shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida

Tanapa yadhibitisha taarifa za moto kuwaka mlima Kilimanjaro na kusema shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida

Ndagullachrles

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2023
Posts
256
Reaction score
259
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa )limetoa taarifa za kuwepo moto mlima Kilimanjaro na kuwatoa hofu wananchi na wadau wa uhifadhi kwamba licha ya tukio hilo shughuli za utalii zinaendelea kama kawaida .

Taarifa iliyotolewa jioni ya Leo na kamishna msaidizi wa uhifadhi kitengo Cha mawasiliano Tanapa,Catherine Mbena imesema kuwa moto huo umeripotiwa kuwaka eneo la kikerelwa ndani ya hifadhi ya Taifa Kilimanjaro katika maeneo yanayopakana na wilaya ya Rombo mkoani kilimanjaro .

"Shirika la hifadhi za Taifa Tanzania (Tanapa )linautaarifu umma kuwa Leo septemba 3,2026 saa 9:30 Alasiri moto umeibuka katika eneo la kati ya kikerelwa ndani ya hifadhi ya Taifa kilimanjaro katika maeneo yanayopakana na wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro "

"Juhudi za kuudhibiti moto huo zinaendelea ambapo Tanapa imepeleka timu ya wazimaji moto ya jeshi la uhifadhi kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi na utalii pamoja na wananchi wa vijiji vya jirani ili kuudhibiti moto huo "

"Chanzo Cha moto huo bado hakijajulikana na uchunguzi unaendelea kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulinzi na usalama ,shughuli za utalii katika hifadhi ya Taifa Kilimanjaro zinaendelea kama kawaida "

"Tanapa inapenda kuwahakikishia watalii,wananchi na wadau kwamba usalama wa hifadhi na watalii unaendelea kupewa kipaumbele "

Imehitimisha taarifa ya Tanapa kuhusiana na tukio hilo la moto mlima kilimanjaro ambao ni mrefu kuliko milima yote barani Africa na moja ya vivutio vinavyoliingia Taifa fedha za kigeni kutokana na shughuli za utalii

IMG-20260903-WA0002.jpg
 
Hiyo mida ya saa 10 chopa ilipita usawa wa chini natumaini ilikua inaelekea eneo la tukio
 
Back
Top Bottom