TANAPA yafufua ujenzi hoteli ya kitalii Chato

TANAPA yafufua ujenzi hoteli ya kitalii Chato

Ndiyo inajengwa sasa, nenda kajinyonge
😄 🤣 😂 hahaahaha Mobutu pia alijenga hotel Gbadolite na international Airport kama mwendazake leo ni magofu poleni kwa wanyama wote waliohamishwa kufa Burigi
 
Nyota 5 chato???

Ujinga hautaisha nchi hii.

Shida kubwa nchi hii watu hawana uchungu na mali ya Taifa. Nina imani kabisa hao Maboss wa Tanapa waliopitisha huo ujenzi ukiwaambia wakajenge chochote kwa hela zao binafsi toka mfukoni hapo chato watakataa ila kwa sababu ni hela ya serekali wanaona hata isipokuwa na tija poa tu. Wao wanaangalia 10% watakazopata kwa wakandarasi
Watu watapigaje pesa?
 
[emoji1] [emoji1787] [emoji23] hahaahaha Mobutu pia alijenga hotel Gbadolite na international Airport kama mwendazake leo ni magofu poleni kwa wanyama wote waliohamishwa kufa Burigi

Inajengwa tena ya nyota 5
 
Ma- Chadema mnajishusha sana hadhi yenu kupingana na maendeleo ya CCM, kutoka mwaka 2015 mlipoinuliwa na Lowasa kisha mkaangukia pua mmebaki na maweweseko tu, nakuhakikishia Historia ya CHUMA JPM hata ungefanyaje hauwezi kuifuta na vizazi vingi vijavyo vitamsoma kama Rais aliyethubutu kufanya mambo yaliyowashinda wengi . wewe baki na maweweseko yako hamna mvuto wowote. kwishinei.
 
Wateja watakuwa kina nani?
Vipi airport kwa siku ndege ngapi zinatia Chato aka Gbadolite airport?

Wateja watakuwa ni nyumbu wa ufipa, wakiachiwa ufipa wataenda hiyo hoteli
 
Ma- Chadema mnajishusha sana hadhi yenu kupingana na maendeleo ya CCM, kutoka mwaka 2015 mlipoinuliwa na Lowasa kisha mkaangukia pua mmebaki na maweweseko tu, nakuhakikishia Historia ya CHUMA JPM hata ungefanyaje hauwezi kuifuta na vizazi vingi vijavyo vitamsoma kama Rais aliyethubutu kufanya mambo yaliyowashinda wengi . wewe baki na maweweseko yako hamna mvuto wowote. kwishinei.

Uko sahihi
 
Wateja watakuwa ni nyumbu wa ufipa, wakiachiwa ufipa wataenda hiyo hoteli
Hahahaha kumbe nyumbu wa ufipa walijengewa airport chato 😄 🤣 😂 wale nyumbu wa Burigi walikufq wote au watapanda meli?
 
Nyota 5 chato???

Ujinga hautaisha nchi hii.

Shida kubwa nchi hii watu hawana uchungu na mali ya Taifa. Nina imani kabisa hao Maboss wa Tanapa waliopitisha huo ujenzi ukiwaambia wakajenge chochote kwa hela zao binafsi toka mfukoni hapo chato watakataa ila kwa sababu ni hela ya serekali wanaona hata isipokuwa na tija poa tu. Wao wanaangalia 10% watakazopata kwa wakandarasi
Kwa hiyo mama kizimkazi kwenda na wasanii korea kusini kusaini mkopo wa trilioni 6.51 ndo kuna tija?
 
Chadema waendelee na rushwa za uchaguzi wa kanda maana wametudhihirishia watanzania kwamba hawana sifa tena ya kuongoza ndani ya nchi hii.
 
Nyota 5 chato???

Ujinga hautaisha nchi hii.

Shida kubwa nchi hii watu hawana uchungu na mali ya Taifa. Nina imani kabisa hao Maboss wa Tanapa waliopitisha huo ujenzi ukiwaambia wakajenge chochote kwa hela zao binafsi toka mfukoni hapo chato watakataa ila kwa sababu ni hela ya serekali wanaona hata isipokuwa na tija poa tu. Wao wanaangalia 10% watakazopata kwa wakandarasi
Actualy kwenye hili nitawatetea, hii ilikuwa order ya aliekuwa mkuu wakati huo. Haukua mpango wao, na ujenzi ulianza mkuu akiwanbado yupo madarakani
 
Tanapa inamiliki hoteli ngapi za kitalii Tanzania? Tangu lini taasisi ya serikali iliweza kufanya biashara kwa ufanisi? Hayo ni matumizi mabaya ya kodi zetu .
Tanapa haimiliki hoteli basicaly, but hii ilikuwa order kutoka juu wakati wa mtu yule, hawakuwa na namna
 
Alhamisi, Aprili 25, 2024

Shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa) linajenga Hoteli ya Kitalii ya nyota tano wilayani Chato, mkoani Geita, yenye lengo la kuvutia watalii katika hifadhi za mwambao huo zikiwemo za Burigi-Chato na ile ya Kisiwa cha Rubondo.

Chato. Ujenzi wa Hoteli ya Kitalii ya nyota tatu katika Kijiji cha Rubambagwe, Wilaya ya Chato, Mkoa wa Geita uliokuwa umesimama kutokana na ukosefu wa fedha, unatarajia kuendelea baada ya Serikali kutoa Sh480 milioni.

Hoteli hiyo inajengwa na Suma JKT ikiwa na lengo la kuchochea utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo na Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato.

Akizungumza na waandishi wa habari katika eneo la mradi hivi karibuni, Mkuu wa Wilaya ya Chato, Said Nkumba alisema tayari fedha hizo zimeingia kuendelea ujenzi huo, ikiwa ni ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan, aliyoitoa kwenye mazishi ya Rais wa tano, Hayati John Magufuli kuwa angeendeleza miradi iliyoanzishwa na mtangulizi wake ikiwemo Hoteli hiyo.

Katika mazungumzo hayo, Nkumba amesema miradi kama Bwawa la Kuzalisha Umeme la Julius Nyerere, Reli ya Kisasa (SGR) na Daraja la la JPM maarufu daraja la Busisi na mingine imeendelea kutekelezwa kwa ufanisi.

Nkumba amesema miongoni mwa miradi hiyo inayoendelezwa imo ya wilayani Chato ambayo ni Hospitali ya Rufaa ya Kanda na Hoteli hiyo ya kitalii inayotarajiwa kukamilika Desemba 2024.

“Ahadi anakwenda kuendeleza miradi iliyoachwa na mtangulizi wake ameendelea nayo na hapa kulikuwa na tatizo la kuendelea na mradi huu wa hoteli. Tulikwisha kupokea Sh700 milioni na tayari Sh480 milioni zimeingia ili kuuendeleza.

“Jitihaza za Serikali zinajidhihirisha kuwa tunaikuza sekta ya utalii na kufanya utalii kwa maeneo mbalimbali kwenye Hifadhi ya Burigi-Chato na Rubondo. Hapa kutakuwa na kila kitu kinachojitosheleza na mradi huu tunausimamia vizuri kuhakikisha unakamilika kwa wakati.”

Mkuu huyo wa wilaya amesema hadi kukamilikwa kwake, mradi huo unatarajia kugharimu takribani Sh11 bilioni na wao kwa niaba ya wilaya watahakikisha wanausimamia kikamilifu.

“Lakini mradi huu ni kichochea tu, kuna miradi mingine ya kitalii na watalii wanatembelea hifadhi zetu lakini wakifika hapa wanakosa maeneo ya kulala, sasa wataweza kulala hapahapa na kuchochea maendeleo ya maeneo haya,” alisema.

Mhandisi wa Jengo kutoka Suma JKT, Abdul Kobeza amesema wanajenga hoteli ya hadhi ya nyota tatu itakayokuwa na vyumba 30 kati yake kumi vya kawaida na 20 vya hadhi ya juu vikiwa na kila kitu ndani.

Amesema kutakuwa na kumbi za mikutano nne na kati yake tatu zinaweza kukodishwa kwa watu mbalimbali.

Kobeza amesema kutakuwa na mighahawa na kutajengwa viwanja vya mipira na mabwawa ya kuogelea pamoja na nyumba za watu mashuhuli, akiwemo Rais iwapo atambelea eneo hilo na kuhitaji kulala, ili kuifanya kwenda na hadhi ya nyota tatu.

Amesema kutoka hotelini hapo kwenda Kisiwa cha Rubondo si mbali ni takribani kilomita 20 na kupita majini ni karibu zaidi.

Mhandisi huyo amesema kwa sasa mradi huo umefikia asilimia 67 na wanatarajia kukamilika Desemba mwaka huu.

Wenyeji wachekelea

Mkazi wa eneo hilo, Katarina Charles alisema kukamilika kwa hoteli hiyo itakuwa ni fursa za kuchochea maendeleo yao binafasi na wilaya.

“Yaani sisi kama majirani wa eneo hili tutaneemeka kwa vitu vingi, tutapokea wageni wa kila aina na maendeleo tutayatapa kwani tutatengeneza vitu vya kuwavutia watalii. Hata kuuza miwa na karanga.”

Naye Mariam Rusangija alisema kukamilika kwa ujenzi huo wananchi wanaweza kupata ajira na kufanya biashara: “Najua ujenzi ukikamilika hatuwezi kukosa hata ajira. Unajua mpaka sasa hakuna hoteli kama hii na hii itakuwa ya kwanza, hivyo tunasubiri tu ikamilike.”

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Kisiwa cha Rubondo, Dk Immani Kikoti amesema tangu Rais Samia alipozindua filamu ya Royal Tour kumekuwa na mwitikio mkubwa wa watalii wa kutoka nje na ndani kutembelea vivutio vilivyopo nchini.

Dk Kikoti amesema mikoa ya kaskazini imejipanga vizuri kwa kuwa na hoteli nyingi, tofauti na maeneo mengine ikiwemo hifadhi hizo za Burigi- Chato, Rubondo na hifadhi zingine ambazo ziko mkoani Kagera zinazohitaji kuwa na maeneo mazuri ya kufikia wageni.

“Eneo hili ni maarufu sana kwa ajili ya utalii, jinsi utalii unavyopanuka na Serikali kutangaza vivutio kutakuwa na wageni wengi wanaohitaji kupata sehemu nzuri za kufikia,” amesema
Ujinga mzigo.

Tanapa ina mbuga zaidi ya kumi na tano,ipo Serengeti,Kilimanjaro,Tarangire,Manyara,Ibanda Kyerwa,Ruaha,Mkomazi,Saadani,Mikumi,Gombe,Mahale,Nyerere,Udzungwa,Rubondo......Hifadhi zote hakuna hotel inayomilikiwa na TANAPA!.

Biashara za hotels & lodges serekali ilishajiondoa siku nyingi.

Watanzania sijui kwanini ujinga na upumbavu umekuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku.

Magufuli kupitia mamlaka yake ya uRais aliyatumia vibaya kujipendelea sehemu aliyozaliwa Hili lipo wazi wala hakuna ubishi.

Ujenzi wa hiyo Hotel,Hospital ya rufaa,CRDB,TANESCO,Zimamoto,VETA,Mahakama,Airport........yalikuwa matumizi mabaya ya fedha umma.

Magufuli aliwakosea heshima,uaminifu,uadilifu Watanzania wote wenye akili sawa sawa.

Wajinga kama wewe kamwe hawawezi kuona ubadhilifu wa Magufuli.Kwa akili zao mbovu wabadhilifu ni wezi wa kuku.
 
Back
Top Bottom