TANAPA yanyakua tuzo 6, hifadhi za taifa zazidi kutikisa ramani ya utalii duniani

TANAPA yanyakua tuzo 6, hifadhi za taifa zazidi kutikisa ramani ya utalii duniani

TANAPA

Govt Institution
Joined
Jul 6, 2026
Posts
16
Reaction score
43
Na. Jacob Kasiri - Zanzibar

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limeendelea kung’ara katika ulingo wa sekta ya utalii Duniani baada ya kushinda tuzo sita za World Travel Awards (WTA) 2026, ushindi uliotangazwa Agosti 28, 2026 katika hafla maalumu iliyofanyika usiku ndani ya Hotel ya Diamond Bijoux Bwejuu - Zanzibar.

Ushindi huo ni ishara ya kuidhihirishia Afrika na dunia kwa ujumla ubora wa vivutio vya utalii, uhifadhi kuntu wa maliasili na huduma bora zinazotolewa kwa watalii ndani ya Hifadhi za Taifa nchini.
7D0A8270.jpg
Wakati wa hafla hiyo almaarufu Africa Gala Ceremony, Mwanzilishi na Rais wa taasisi ya World Travel Awards Bw. Graham Cooke alisema kuwa ni heshima kubwa kwa mwaka huu 2026 kuona Zanzibar akiwa mwenyeji wa hafla hiyo.
7D0A8038.jpg
Bw. Cooke aliongeza, “Tanzania ni miongoni mwa nchi za Afrika zinazokua kwa kasi sana katika sekta ya utalii na inayoendelea kuweka rekodi ya watalii wengi katika maeneo ya fukwe za Zanzibar na katika Hifadhi za Taifa na mchango wa watalii hao huenda moja kwa moja kwa mtu mmoja mmoja na kuimarisha uchumi wa Taifa kwa ujumla.”

Akipokea tuzo hizo, Kamishna wa Uhifadhi TANAPA Massana Mwishawa alisema kuwa ushindi huo unaifanya TANAPA kuendelea kuwa mdau muhimu katika uhifadhi wa rasilimali ambazo ndio msingi wa vivutio vya utalii na kukuza utalii endelevu, huku tuzo hizo zikitajwa kuwa ni kielelezo cha kutambulika kwa Tanzania katika soko la kimataifa la utalii.
7D0A8315.jpg
“Kupitia tuzo hizo, Hifadhi za Taifa Tanzania zimeendelea kuvutia watalii wengi na wawekezaji ambao huchagiza katika ongezeko la mapato yanayotumika katika ujenzi wa miundombinu mbalimbali zikiwemo barabara, huduma za maji safi na salama na afya".

Aidha, Kamishna Mwishawa aliongeza, “Mafanikio hayo pia yanaakisi jitihada za makusudi zinazofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuboresha miundombinu ya watalii, kutangaza vivutio kupitia filamu za “Tanzania the Royal Tour na Amazing Tanzania” sanjari na kuvutia uwekezaji kupitia sera zake za Diplomasia ya Uchumi”.
7D0A8080.jpg

Hifadhi za Taifa Tanzania zilizoibuka kidedea ni pamoja na “Tarangire National Park as Africa’s Leading Elephant Paradise National Park, Nyerere National Park as Africa’s Leading Scenic National Park 2026 na Ruaha National Park as Africa’s Leading Cultural National Park 2026”. Nyingine ni pamoja na Serengeti National Park ambayo imenyakua tuzo mbili ambazo ni “Africa’s Leading National Park 2026 na Africa’s Leading Big Five National Park 2026” huku Kilimanjaro National Park as “Africa’s Leading Mountain National Park 2026”.

Kwa TANAPA, ushindi wa tuzo sita unatoa fursa ya kuendelea kuitangaza Tanzania katika masoko ya ndani na kimataifa, kuvutia watalii zaidi na kuongeza uelewa wa umuhimu wa uhifadhi wa rasilimali za Taifa. Ushindi wa tuzo hizo sita si ushindi wa TANAPA pekee, bali ni tunu kwa Taifa na unapeleka ujumbe kwa dunia kuwa maliasili tulizo nazo zinaendelea kukonga mioyo ya watalii na wawekezaji katika majukwaa ya kikanda na kimataifa.
7D0A8050.jpg
World Travel Awards, ambayo ni miongoni mwa taasisi za kimataifa zinazotambua ubora katika sekta za usafiri wa anga, hoteli na utalii Afrika na dunia, hutumia mchakato wa upigaji kura na washindi hupewa tuzo hizo za kimataifa.
 
Hongera sana TANAPA.
Ongezeni juhudi kuboresha huduma kwa wataje ili watalii waendelee kukumbuka Tanzania kwa huduma nzuri.
 
Back
Top Bottom