TANESCO: Ajali ya moto Lindi haijaathiri upatikanaji wa umeme

TANESCO: Ajali ya moto Lindi haijaathiri upatikanaji wa umeme

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
TANESCO MAKAO MAKUU, S.L.P. 453, DODOMA, TANZANIA. SIMU 0748550000


TAARIFA KWA UMMA


TUKIO LA AJALI YA MOTO KATIKA OFISI YA TANESCO MKOA WA LINDI



Jumapili, 20 Julai, 2025.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linawataarifu wateja wake na umma kwa ujumla kuwa asubuhi ya leo, majira ya saa 3:00 asubuhi, kulitokea ajali ya moto katika chumba kimoja cha Ofisi ya TANESCO Mkoa wa Lindi.


Tukio hilo liliripotiwa mapema na hatua za haraka zilichukuliwa ambapo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Lindi lilifika kwa wakati na kufanikwa kudhibiti moto huo majira ya saa 5:30 asubuhi.


Mpaka sasa, chanzo kamili cha ajali hiyo hakijafahamika, na tayari taratibu za uchunguzi wa kina zimeanza ili kubaini chanzo cha moto huo pamoja na tathmini ya athari zilizotokana na tukio hilo.


TANESCO inapenda kuwatoa hofu wateja wake na wananchi wote wa Mkoa wa Lindi kuwa pamoja na kutokea kwa ajali hiyo hakujathiri hali ya upatikanaji wa umeme kwa wateja wake na huduma zinaendelea kutolewa kama kawaida.


Imetolewa Na:


KURUGENZI YA MAWASILIANO NA HUDUMA KWA WATEJA
TANESCO MAKAO MAKUU
DODOMA

1753005675936.png
 
Back
Top Bottom